Watu wazima wengi hawana pete za ndoa

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
11,320
3,475
Hili nimeliona na kulifanyia utafiti kidogo. Inafika wakati ukimwona mtu mzima mke au mume miaka kuanzia 50 ana pete unashangaa kiasi. Wanaona noma au wamepoteza au wamepiga bei? Tufahamishane katika hili
 
si watu wote imani zao zina ruhusu uvaaji wa pete....
 
Hili nimeliona na kulifanyia utafiti kidogo. Inafika wakati ukimwona mtu mzima mke au mume miaka kuanzia 50 ana pete unashangaa kiasi. Wanaona noma au wamepoteza au wamepiga bei? Tufahamishane katika hili

- wewe unaivaa?
- na kama umeshafikisha umri wa kuoa/kuolewa kwa nini hujaoa au kuolewa?
 
Lecturer wangu mmoja pale UDSM miaka hiyoo yeyealikuwa mtu wa misifa sana na kila mara alipenda kuelezea mambo binafsi darasani, siku moja alieleza kwanini havai pende ya ndoa, akasema yeye haoni sababu ya kuvaa pete ya ndoa kwasababu halazimika kumtangazia kila mtu kama ana ndoa, akasema alipokuwa kijana aliona ni ufahari na pia ilikuwa kama pambo, lakini sasa amekuwa mtu mzima anaona ni kitu cha kawaida.

My take: Nahisi pia kuna ka-element kakuchokana kati ya wanandoa waliofika umri huo kwahiyo mtu anaona mzigo tu hata kujivunia kama ana ndoa.
 
- wewe unaivaa?
- na kama umeshafikisha umri wa kuoa/kuolewa kwa nini hujaoa au kuolewa?

nikisoma jina lako linanipeleka mbali kweli. Slang yetu sie kwa utingo ni zile hisia za mwanamke pale kati! Halafu sijaoa ila nadhani nitaipenda pete yangu
 
Ukiona wanandoa kama hao ujue wameshapigana vita vingi kuanzia vya kimwili, kiakili na vya kihisia
 
Labda na mazoea yanachangia kwa namna flan, kwamba mtu kabla ya ndoa amezoea kuishi bila pele hivyo akishaingia ndani ya ndoa anaona pele ya nini tena wakati niliyemtaka tayari ninaye, Katika hili elimu ya ndoa inaitajika zaidi toka kwa wafungishaji wa hizo ndoa.
 
nakubali mada husika, mwenyewe nimeshuhudia watu hawa! Lakini kwa kina mama wanazipenda pete zao na wameongezea na zile za engagement kuonesha msisitizo. Hata hapa ofisini kwetu kuna mwana mama alikuwa na marriage ring na sasa ana engament ring hapo ndo najiuliza amevishwa na mumewe au kanunua na kujivisha mwenyewe au?! nahisi hii ya kutokuvaa pete ipo kwa wanaume zaidi ya wanawake
 
Ha haaa wengine pete zime wabana wengine zimepotea, wengine walitaka kuingia kwa ndoa baada ya hapo ndoa zimekua chungu hata pete zinawatia hasira hawazivai, wa baba wana ziweka ndani ya magari yao wa mama kabatini, wengine walitaka kingia ndani wengine wanataka kutoka haina haja ya uchunguzi sababu kuu ni hizo. Si kwamba wanaficha kitu manaake watu siku hizi wanawapenda hao wenye pete mradi vurugu tu. JESUS IS MY HOME BOY.
 
Nimeshuhudia mdada mmoja akitamani kutupa mipete ya ndoa. Mara atazivaa kidole gumba, mara ataziweka kwenye pochi, ilimradi zisikae kidole husika. Kumbe mchakato wa kutovaa pete huanzia mbali
 
labda swali hili ndo lina wafanye wasivae........."nitapataje kama nikivaa"????
 
nyie bado hamjajua nini maana ya ndoa watu wengi wanaingia kwenye ndoa wakiwa nalengo si mapenzi ndio maana inakua ishu kudumu kwenye ndoa
 
Inawezekana wamezivalia kwenye mioyo yao hivyo hilo pambo la kidoleni hilina maana tena!
 
ila cahakushangaza watu wengi wanapenda sana wanandoa kwanini wakati kuna watu wengi wanatafuta kuolewa hawaolewi?
 
Back
Top Bottom