Watu wawili Watakaomkwamisha Rais Magufuli

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Baada ya Kufikiria sana, Na Bado Nikiendelea Kutunza Ahadi yangu, ya Kutosema tena Neno hata Moja Kinyume na Mh. Magufuli. Sidhani Kama Nitakuwa Nimesema Kinyume naye, Nikisema, Katika jitihada zake za Kujenga Tanzania anayoitaka, Watakaoweza kumkwamisha Ni Viongozi wawili waliomtangulia.

Bila Kuwataja Majina Niseme Kuwa, Ni Ukweli mgumu kwa Magufuli Kuwa hisia za Kwamba Watu au Viongozi hawa Ndio waliompa Fursa ya Kuonekana Katika Siasa. Na Kwa Loyalty aliyonayo itamsuumbua sana kuamini pamoja na fursa waliompa, yeye alijijenga mwenyewe. Zaidi Kwa Kuonyesha Mfano wa Kutumikia Taifa na Wananchi kwa Nguvu na Moyo wake wote. Nasema Hivi kwa Kuwa sio yeye pekee aliyepewa fursa, wapo wengi walipewa fursa lakini hawakuitumia kufikia upeo wake.

Kadhalika Maoni yangu Ni Kuwa Badala ya Kuangalia Tu alipewa Fursa, Jambo ambalo Ni kweli, bado na yeye Alisaidia sana Administration zao angalau kuonekana zinafanya Kazi Nzuri, Kwa Pale yeye alipohusika. Wakati anapoomba wananchi Wamuombee, Ni Vizuri ajenge Ujasiri wa Kuamua kukataa Mashinikizo yoyote kwa Mantiki ya Loyalty. Kwa Hili Mungu hatashuka Kutoka Mbinguni Kumsaidia. Sio Nia yangu Kusema kuwa akatae ushauri Mzuri, Ila Kwa Madudu aliyoyakuta, Nadiriki Kusema waliomtangulia wana machache sana ya Kumshauri. Let him Be, ya'll had your time! Ni matumaini yangu Kuwa Kama Mlikuwa na Mawazo ya Kumtumia Ili mrudi tena Madarakani, Mumtumie Kama lift katika safari ya Uonzo uleule. Itakuwa Mumemsaliti, Na Sio Kumsaliti yeye tu bali Taifa na Watanzania pia.
 
Hivi w

Hivi wewe ndio mgunduzi wa neno jipu?..ila mbona na wewe ni jipu?achana na siasa za kichawichawi...kupiga ramli...kuomba mtu ashindwe!...
e
 
Ni vyema ukamjibu kwa kujenga hoja, otherwise wewe ndio huna lolote.
tumia akili na wewe
wakati wa kuchangia kwanza angalia mchangiaji hasa ID na avartar yake utagundua mengi Member anaanza na jina
  1. TL Marandu
  2. Mrema
  3. lowassa team
  4. babatovu
  5. lema, mbowe, mrombo
hao ni wote wasiomtakia mema Magufuli
wao wapo hapa kupinga tu chochote cha mtawala
sasa hapo kuna hoja gani unataka mtu apinge wakatu wenzako wanataka Magufuli ashindwe uchaguzi urudiwe,
Kwa akili tu Jakaya na Mkapa wana nia ya kuingia madarakani kweli
sasa wanaowania ndio wanaleta vipost vya namna hii
 
Ni vyema ukamjibu kwa kujenga hoja, otherwise wewe ndio huna lolote.

Analo tena sana. Wewe ndie uliemjibu kishabiki tena ushabiki wa kichama zaidi ingawa kwa hao aliowataja huna unaloweza kufaidi toka kwao sana sana ni fuata upepo tu. Nasema ni kweli kutokana na ushikaji hatamu wa chama chao(supremacy) ya chama chao kuwa ndicho kinachoiongoza serikali kuna mambo wanaweza kumshinikiza raisi aliepo madarakani kuyatekeleza hata kama hayana manufaa kwa wananchi na taifa.Zipo kamati kwenye chama ambazo m/kiti wa chama taifa kabla hajakabidhi madaraka kwa raisi alieshinda uchaguzi akiwa vizuri na wajumbe wanaweza kupitisha madudu fulani yatekelezwe na raisi haswa kwenye teuzi za viongozi wa serikali.Raisi hatakuwa na ubavu wa kuyakataa hadi atakapokabidhiwa kofia ya m/kiti taifa. Sasa Magufuli ana mungu kwani ni keshokutwa mwezi June mwaka huu atakabidhiwa madaraka hayo. Kuanzia hapo atawachambua huko ccm kwenyewe ambako ndiko kimbilio la mafisadi na hatakuwepo tena mtu wa kumshinikiza kutekeleza tofauti na anavyofikiri inafaa kwa maslahi ya wananchi na taifa.Hivi kwa yeyote anaeona mbali ni vigumu kungamua hata baraza lake wako wachache alionganganizwa? Hayo ni mawazo yangu wala sio lazima yawe kweli na nisiulizwe ushahidi.
 
Hivi w

Hivi wewe ndio mgunduzi wa neno jipu?..ila mbona na wewe ni jipu?achana na siasa za kichawichawi...kupiga ramli...kuomba mtu ashindwe!...
e

Ingawa naheshimu haki yako ya Kujibu vyovyote Upendavyo, Sidhani Kama Uko sahihi, Unadhani Mimi Mchawi au Mpiga Ramli, Au namtakia Magufuli Kushindwa? far be from it!
1) Magufuli akitaka Kusaidia afya ya Kina Mama, Na kuwapatia mazingira Mazuri ikiwa ni pamoja na kupata Vitanda wawapo hospitalini Kwanini Nimtakie Kushindwa
2) Magufuli anayepambana na Wakwepa Kodi Kwanini Nimtakie Kushindwa,
3) Magufuli akizuia safari za Kipuuza zinazofuja fedha za serikali Kwanini Nimtakie Kushindwa,
4) Magufuli Akiwajibisha Viongozi wazembe, Kwanini Nimtakie Kushidwa
5) Magufuli akitaka kusaidia Elimu ya Watoto wetu iwe Bure kutusaidia wazazi, Kwanini Nimtakie Kushindwa.
6) Magufuli Akitaka Kupanga Mipango Mizuri ya Uchumi itakayoleta Ajira kwa Vijana na Kusaidia wakulima, Kwanini Nimtakie Kushindwa.
7) Magufuli akitaka Kuboresha Miundo mbinu ya Mijini, Pamoja na Kufufua Viwanda Kwanini Nimtakie Kushindwa.

Angelikuwa Mfujaji Kwa Kuzurura duniani, akitumia Matrilioni ya Fedha za Wananchi Ningemtakia Kushindwa,
Angepindisha Sheria/Katiba ili Kukibeba Chama chake au Kikundi cha watu isivyo halali Ningemtakia Kushindwa
Angelitumia Familia yake Kushiriki katika kuwezesha Ukwepaji wa Kodi, Na Kujihusisha na Biashara Zenye Maswali Ningemtakia Kushindwa.
Angejihusisha Kuweka Mikataba Michafu ya Madini Gesi na Mafuta yetu Kujinufaisha yeye na baadhi ya Watu Ningemtakia Kushindwa.
Angelitumia Uwezo wa Dola Kukandamiza Uhuru wa Kidemokrasia na Habari Ningemtakia Kushindwa.

Isitoshe, Kwa aina ya Mtu ambaye Wote Tunamjua, Kukwamishwa Ninakozungumzia, Sio Kumkwamisha Kuwa Rais Mwenye Mafanikio Modest, Hilo halina Mjadala ameshafanikiwa. Ila Akitaka awe Rais wa Mfano, Mwenye Mafanikio yatakayobadilisha kabisa sura ya Tanzania, Kisiasa , Kijamii na Uchumi. Mwenye Mafanikio yatakayomweka Katika Historia ya Great Leaders wa Africa Miaka Karne Zijazo. Ndipo Nasema Hana Njia ya Mkato bali Kuwa Myoofu, Na Mweupe Kama Theluji, Na Independent. Kama Utanitukana Kwa Kusema Hivyo, Unakaribishwa.
 
Analo tena sana. Wewe ndie uliemjibu kishabiki tena ushabiki wa kichama zaidi ingawa kwa hao aliowataja huna unaloweza kufaidi toka kwao sana sana ni fuata upepo tu. Nasema ni kweli kutokana na ushikaji hatamu wa chama chao(supremacy) ya chama chao kuwa ndicho kinachoiongoza serikali kuna mambo wanaweza kumshinikiza raisi aliepo madarakani kuyatekeleza hata kama hayana manufaa kwa wananchi na taifa.Zipo kamati kwenye chama ambazo m/kiti wa chama taifa kabla hajakabidhi madaraka kwa raisi alieshinda uchaguzi akiwa vizuri na wajumbe wanaweza kupitisha madudu fulani yatekelezwe na raisi haswa kwenye teuzi za viongozi wa serikali.Raisi hatakuwa na ubavu wa kuyakataa hadi atakapokabidhiwa kofia ya m/kiti taifa. Sasa Magufuli ana mungu kwani ni keshokutwa mwezi June mwaka huu atakabidhiwa madaraka hayo. Kuanzia hapo atawachambua huko ccm kwenyewe ambako ndiko kimbilio la mafisadi na hatakuwepo tena mtu wa kumshinikiza kutekeleza tofauti na anavyofikiri inafaa kwa maslahi ya wananchi na taifa.Hivi kwa yeyote anaeona mbali ni vigumu kungamua hata baraza lake wako wachache alionganganizwa? Hayo ni mawazo yangu wala sio lazima yawe kweli na nisiulizwe ushahidi.

Ni Kweli, Muhongo Alitakaswa Kabla hata Magufuli hajawa Mgombea. Nani anaamini Kuwa Magufuli ambaye huwa hataki Kashifa angeamua Mwenyewe Kumrudisha Tena Muhongo, au Kumpa tena Madaraka Eliakimu Maswi? Hata Kama Hawana, "hatia" Bado Bunge Liliagiza wawajibishwe! Huoni Kuna Kitu Hapo. Hudhani Kama yale Mabilioni ya ile Kashfa ya Stanbic, Magufuli angedeal Nayo jana asubuhi ingekuwa Rahisi?
 
Bwana Marandu kama nilivyoeleza kwenye mchango wangu nawe ukakiri kuwa kwa akili ya kawaida tu isingetegemewa Magufuli kumteua Sospeter Muhongo katika baraza lake huku akielewa yapo maazimio ya bunge kwa Muhongo na wengine ambaya hayajatekelezwa.Hayo ndio niliyosema ni mashinikizo toka kwenye chama.Wapo kama watatu au wanne mbali ya waliopendekezwa kupelekwa kwenye balozi. Lakini bw.Marandu sio mbali ni mwezi June tu Magufuli anakabidhiwa hiyo kofia ya uenyekiti wa chama taifa na si ajabu July akafanya reshuffle ya baraza akawaengua wote alioshinikizwa kuwateua. Uzuri ni kuwa wakishaenguliwa na mahakama ya mafisadi itakuwa imeshakamilika hivyo wanaanza nao. Nakushukuru kwa uelewa wako kuliko wanaojibu kiushabiki wa chama kama wachangiaji wengine.
 
alivoshindwa kuwataja watu wenyewe thamani ya alichokiandika imeondoka, sisi hatutaki mafumbomafumbo
 
Ingawa naheshimu haki yako ya Kujibu vyovyote Upendavyo, Sidhani Kama Uko sahihi, Unadhani Mimi Mchawi au Mpiga Ramli, Au namtakia Magufuli Kushindwa? far be from it!
1) Magufuli akitaka Kusaidia afya ya Kina Mama, Na kuwapatia mazingira Mazuri ikiwa ni pamoja ya kupata Vitanda wawapo hospitalini Kwanini Nimtakie Kushidwa
2) Magufuli anayepambana na Wakwepa Kodi Kwanini Nimtakie Kushidwa,
3) Magufuli akizuia safari za Kipuuza zinazofuja fedha za serikali Kwanini Nimtakie Kushidwa,
4) Magufuli Akiwajibisha Viongozi wazembe, Kwanini Nimtakie Kushidwa
5) Magufuli akitaka kusaidia Elimu ya Watoto wetu iwe Bure kutusaidia wazazi, Kwanini Nimtakie Kushidwa.
6) Magufuli Akitaka Kupanga Mipango Mizuri ya Uchumi itakayoleta Ajira kwa Vijana na Kusaidia wakulima, Kwanini Nimtakie Kushidwa.
7) Magufuli akitaka Kuboresha Miundo mbinu ya Mijini, Pamoja Kufufua Viwanda Kwanini Nimtakie Kushidwa.

Angelikuwa Mfujaji Kwa Kuzurura duniani, akitumia Matrilioni ya Fedha za Wananchi Ningemtakia Kushidwa,
Angepindisha Sheria/Katiba ili Kubeba Chama chake au Kikundi cha watu isivyo halali Ningemtakia Kushidwange
Angelitumia Familia yake Kushiriki kuwezesha Ukwepaji wa Kodi, Na Kujihusisha na Biashara senye Maswali Ningemtakia Kushidwa.
Angejihusisha Kuweka Mikataba Michafu ya Madini Gesi na Mafuta yetu Kujinufaisha yeye na baadhi ya Watu Ningemtakia Kushidwa.
Angelitumia Uwezo wa Dola Kukandamiza Uhuru wa Kidemokrasia na Habari Ningemtakia Kushidwa.

Isitoshe, Kwa aina ya Mtu ambaye Wote Tunamjua, Kukwamishwa Ninakozungumzia, Sio Kumkwamisha Kuwa Rais Mwenye Mafanikio Modest, Hilo halina Mjadala ameshafanikiwa. Ila Akitaka awe Rais wa Mfano, Mwenye Mafanikio yatakayobadilisha kabisa sura ya Tanzania, Kisiasa , Kijamii na Uchumi. Mwenye Mafanikio yatakayomweka Katika Historia ya Great Leaders wa Africa Miaka Karne Zijazo. Ndipo Nasema Hana Njia ya Mkato bali Kuwa Myoofu, Na Mweupe Kama Theluji, Na Independent. Kama Utanitukana Kwa Kusema Hivyo, Unakaribishwa.
pokea like yangu Mkuu, niambie tu kadgree umepata chuo gani hongera.

Lakini usiache kusema Magufuli aache kutusaliti kwa kuwa sasa tunafata maadili, K na Ben wasimzunguke. kwa mfn mramba na yona pekee Ndo wanastahili kupewa offer ya kifungo cha nnje??

Wafungwa wangapi wanakaa gelezani bila sabb. Nadhan Magufuli ni mwelewa sana. Tunamkubali sana, ajue bado tunakichukia chama chake, kilichojaa laana za Mwl Nyerere
 
Bwana Marandu kama nilivyoeleza kwenye mchango wangu nawe ukakiri kuwa kwa akili ya kawaida tu isingetegemewa Magufuli kumteua Sospeter Muhongo katika baraza lake huku akielewa yapo maazimio ya bunge kwa Muhongo na wengine ambaya hayajatekelezwa.Hayo ndio niliyosema ni mashinikizo toka kwenye chama.Wapo kama watatu au wanne mbali ya waliopendekezwa kupelekwa kwenye balozi. Lakini bw.Marandu sio mbali ni mwezi June tu Magufuli anakabidhiwa hiyo kofia ya uenyekiti wa chama taifa na si ajabu July akafanya reshuffle ya baraza akawaengua wote alioshinikizwa kuwateua. Uzuri ni kuwa wakishaenguliwa na mahakama ya mafisadi itakuwa imeshakamilika hivyo wanaanza nao. Nakushukuru kwa uelewa wako kuliko wanaojibu kiushabiki wa chama kama wachangiaji wengine.
Safi saa Ana Mkuu nchi hii wastaarabu mpo. Hakuna anaechukia yafanywayo na Mzee Dr Magufuli. Mungu ampe nguvu.

Lkn kabla ya mei amuonye Bwana kipara na Nape waache unazi wa ccm. wananchi hatuna chama kwa sasa ni kazi tu. Nape ananiudhi uccm wake. na kibajaji natamchukia daima
 
inaonyesha wengi wanaopinga hawajasoma hii mada hadi mwisho na kuielewa.......
mkuu @TL.marandu
umegusa point sana mkuuuu..
naunga mkojo hoja
 
Safi saa Ana Mkuu nchi hii wastaarabu mpo. Hakuna anaechukia yafanywayo na Mzee Dr Magufuli. Mungu ampe nguvu.

Lkn kabla ya mei amuonye Bwana kipara na Nape waache unazi wa ccm. wananchi hatuna chama kwa sasa ni kazi tu. Nape ananiudhi uccm wake. na kibajaji natamchukia daima

Mimi nikuite tu Mussa maana bila kuwa mfungisha ndoa wa bomani anaekutana na majina mengi halitamkiki kirahisi hata hivyo kama nilivyomsifu Marandu na mzee Mwanakijiji kwa uelewa wao pia sifa hizo zikufikie nawe. Unafahamu kila jambo hutekelezwa kwa kutumia mamlaka aliyo nayo mtekelezaji.Kwa utaratibu wa kugombea nafasi za kiuongozi nchini hapa ni lazima uombe kupitia chama cha kisiasa chenye usajili wa kudumu.Hatuna sheria ya mgombea binafsi na raisi Magufuli alipitia chama cha ccm ingawa atawaongoza raia wote wenye vyama na wasio navyo.Kwa utaratibu wa chama chao serikali itaongozwa na chama chako hivyo kwa kuwa bado tuna m/kiti aliestaafu chama kinaweza kupendekeza na hata kushinikiza raisi kutekeleza yatakayokubaliwa na vikao vya juu vya chama hata kama hayana maslahi kwa wananchi na taifa. Ndipo niliposema June mwaka huu Magufuli atakabidhiwa huo uenyekiti wa taifa.Hapo ndipo anapoweza kuwaonya hao uliopendekeza na yeyote yule kutoingilia yale anayoamini ni kwa maslahi ya wananchi na taifa letu.Nikwambie jinsi anavyoijua ccm na viongozi wake atarekebisha huko hadi chama kirudishe hadhi yake ya wakati wa Nyerere. Ukikumbuka vizuri hata kwenye kampeni zake alikuwa akijiweka mbali sana na matumizi ya jina la chama chake. CHAGUA JOHN POMBE MAGUFULI. NCHI YANGU HII TANZANIA. Nakushukuru tena.
 
Mkapa na kikwete awaweke mbali kwa kila jambo,hawana chochote cha kumshauri zaidi ya kupiga deal na wizi wa kura.
 
Bwana Marandu kama nilivyoeleza kwenye mchango wangu nawe ukakiri kuwa kwa akili ya kawaida tu isingetegemewa Magufuli kumteua Sospeter Muhongo katika baraza lake huku akielewa yapo maazimio ya bunge kwa Muhongo na wengine ambaya hayajatekelezwa.Hayo ndio niliyosema ni mashinikizo toka kwenye chama.Wapo kama watatu au wanne mbali ya waliopendekezwa kupelekwa kwenye balozi. Lakini bw.Marandu sio mbali ni mwezi June tu Magufuli anakabidhiwa hiyo kofia ya uenyekiti wa chama taifa na si ajabu July akafanya reshuffle ya baraza akawaengua wote alioshinikizwa kuwateua. Uzuri ni kuwa wakishaenguliwa na mahakama ya mafisadi itakuwa imeshakamilika hivyo wanaanza nao. Nakushukuru kwa uelewa wako kuliko wanaojibu kiushabiki wa chama kama wachangiaji wengine.
hivi katika akili yako unategemea hiyo mahakama ya mafisadi itaweza kuwafunga mafisadi waliojazana ccm?
 
Hiyo kuwafunga au kuwaachia huru ni majukumu ya mahakama ila sema inataka serikali ya Magufuli nao wawe na waendesha mashtaka wenye uwezo mkubwa zaidi ya tunaoshuhudia wakipoteza kesi nyingi kirahisi haswa pale wanapokutana na magwiji waliobobea kama kina Lissu n.k.
 
hata sasa tunao ila tatizo la nchi hii ni wanasiasa kuingilia taaluma za watu na wao kuwa waelekezi
 
Back
Top Bottom