Watu wawili wanaodaiwa kutaka kumuua Ali Kiba wasema walitumwa na TID

naumbu

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
4,718
8,062
Mnyama ana tuhuma ya kumtumia msichana ili amuue ali kiba,amehojiwa na clouds fm akiwa kituon na kukanusha madai hayo na kusema hajui chochote na he has nothing against ali k,hawajawah kugombana na anashangaa sana. Source:U heard ya clouds fm
 
Kwa hiyo ray kufumaniwa,dj fetty kumiliki vogue,diamond kumrudia wema etc ndiyo sio gossip!!nishakujua ni mtu wa aina gani am out,unanitafutia ban!!!wewe najua unatafuta bahasha ukaandike barua na kaz yako ni kutoa mbwa bandani if u know what I mean, by the way mpelekee TID yale makitu yenu central!!!
 
[h=1][/h]



Kwenye U heard ya XXL Clouds Fm August 28 2012 Gossip Cop Soudy Brown aliripoti kwamba kuna mwanamke aliekamatwa na Polisi na kuhojiwa kwa masaa nane wakati akiwa kwenye mipango ya kumuua msanii wa bongo fleva Ally kiba.



Baada ya kuhojiwa na polisi kwa masaa nane, mwanamke huyo alikiri kwamba alitumwa na T.I.D kwenda kumuua Ally Kiba.



Alipohojiwa na Soudy Brown, T.I.D alifunguka na kusema “kwa nini nimuue Ally Kiba bwana, si mtu wangu nampenda kabisa bwana, kweli sasa hivi niko polisi kwa ajili ya kuhojiwa, nilikua safari, nimerudi sasa sijui mwanamke gani anaweza kufanya hivyo, siwezi kufanya hivyo, kwa sababu gani?



Toka nimezaliwa sijawahi kugombana na Ally Kiba, ukibisha muulize mwenyewe kama ameshawahi kukorofishana na mimi, nia ya hao watu ni kuniangusha mimi nionekane ni mtu mbaya nisiuze mziki wangu nisipendwe.”



Soudy alipomtafuta meneja wa Ally Kiba alijibiwa “hakuna taarifa zozote ambazo ziko tayari kutolewa kwenye vyombo vya habari sasa hivi lakini ikiwa tayari utakua wa kwanza kujua.
 
Da ninatamani kupata more news about that issue coz it is interesting.Lakini kama kweli hawa wanamuziki wa kizazi kimya wanaenda wapi? badala ya kuendeleza mziki wa kizazi kimpya wao wanaleta mabo mengine! dah!
 
Mbona haya mambo hayana mantiki yoyote? Mtu atake kuua halafu ukutwe kwenye tukio. Haiingii akilini. Inawezekana madai ya TID ni ya kweli.any way tusubiri tuone.
 
haya sasa naona mods wapo kazini ,mapost yako yote wanayaondoa thanks for that,wait for ban @nanyumbu
 
kilichonifurahisha katika thread hii ni hiki hapa chini tu.


user-online.png
nziriye

Today 22:02
#6
Banned Array


Join Date : 23rd January 2011
Posts : 633
Rep Power : 0

Likes Received19
Likes Given6



[h=2]
icon1.png
Re: Tid azungumza kuhusu tuhuma za yeye kutaka kumuua Ali Kiba...!!![/h]
haya sasa naona mods wapo kazini ,mapost yako yote wanayaondoa thanks for that,wait for ban @nanyumbu
 
TID.jpg

TID

Jana kumevuma habari kuwa mwanamuziki wa Bongo Flava Khalid Mohamed aka Top In Dar, anashikiliwa na polisi baada ya kushutumiwa kuwa alipanga njama za kumuua msanii mwenzie Ali Kiba.

Leo kupitia XXL ya Clouds FM, meneja wa Ali Kiba amezungumza kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa hizo.

ALI+KIBA+GETS+SHAVED.jpg

Ali Kiba

Anasema ni kweli walipata ujumbe unaosema kuwa kuna watu waliokuwa wametumwa kwenda kumuua Ali Kiba.


"Baada sasa ya taarifa hizo kuifikia familia, iliamua kuripoti jambo hilo polisi, polisi walifika eneo lile na kulikuwa kuna watu wawili, mwanaume na mwanamke ambao walifika maeneo jirani na pale Ali Kiba anaishi wakawa wameweka kambi pale kwa muda wakijaribu kuchunguza hili na lile. Sasa baada ya watu wa karibu kuwaona na kutowatambua vizuri waliamua kuwafuatlia na kuwaweka chini baada ya kuwakamata.

Walipowahoji vizuri wakasema kwamba ni kweli wao wametumwa kuja kufanya jambo hlo hapo kwa Ali Kiba na wao sio wenyeji wa Dar es Salaam wametoka mikoani. Walipoulizwa ni nani ambaye amewatuma kuja kufanya hilo jambo wakawa wamemtaja TID Kwamba moja kwa moja yeye ndo anahusika. Basi moja kwa moja gari la jeshi la polisi likaenda kumkamata TID na hatimaye kumfikisha kwenye kituo cha polisi cha kati ambapo yupo mpaka hivi sasa anashikiliwa."

Ameongeza kuwa TID na watu hao walikutana katika maeneo ya Mtoni Kijichi kupanga mpango huo wa kumuua Ali Kiba.

AUDIO:

[JFMP3]http://cdn10.hulkshare.com/dev10/0/005/356/0005356069.fid/tid.mp3[/JFMP3]

Meneja wa Ali Kiba akizungumza kuhusu Tuhuma za Tid kupanga njama za kumuua Ali Kiba

Kwa hisani ya LEOTAINMENT BLOG
 

Attachments

  • TID.jpg
    TID.jpg
    34.9 KB · Views: 613
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom