Watu watatu wapoteza maisha kutokana kukosekana kwa usafiri wa kuwapeleka hospitali ya rufaa mkoani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
MBULACE.jpg


Kituo cha afya cha Muhukuru kilichopo wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa dereva wa kuendesha gari la wagonjwa la kituo hicho ambapo imepelekea watu watatu kupoteza maisha kutokana na ukosefu wa usafiri wa kupelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa-Songea.

Hayo yamebainishwa katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani cha Halmashauri ya wilaya ya songea na diwani wa kata hiyo,Simon Kapinga ambapo ameelezea kusikitishwa na vifo hivyo na kwamba vimetokana na ukosefu wa dereva katika kituo hicho baada ya dereva wa awali kukumbwa na sakata la vyeti feki na kufukuzwa kazi.

Kufuatia kauli hiyo Rajabu Mtiula, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo anachukua hatua za haraka za kunusuru maisha ya wananchi wanaohudumiwa katika kituo hicho,na hapa anamuuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,simon bulenganija kuhakikisha anapeleka dereva ndani ya siku saba.


Chanzo; ITV
 
Kuna watu hawako serious kabisa na maisha ya watu...Daah

Wapumzike kwa amani ndugu zetu na pole kwa wafiwa
 
Back
Top Bottom