Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,569
- 9,429
Kituo cha afya cha Muhukuru kilichopo wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa dereva wa kuendesha gari la wagonjwa la kituo hicho ambapo imepelekea watu watatu kupoteza maisha kutokana na ukosefu wa usafiri wa kupelekwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa-Songea.
Hayo yamebainishwa katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani cha Halmashauri ya wilaya ya songea na diwani wa kata hiyo,Simon Kapinga ambapo ameelezea kusikitishwa na vifo hivyo na kwamba vimetokana na ukosefu wa dereva katika kituo hicho baada ya dereva wa awali kukumbwa na sakata la vyeti feki na kufukuzwa kazi.
Kufuatia kauli hiyo Rajabu Mtiula, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo anachukua hatua za haraka za kunusuru maisha ya wananchi wanaohudumiwa katika kituo hicho,na hapa anamuuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,simon bulenganija kuhakikisha anapeleka dereva ndani ya siku saba.
Chanzo; ITV