Watu watatu wapandishwa Kisutu wakikabiliwa na njama za Ugaidi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,189
4,103
Ugaidi.jpg

Watu watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka saba, yakiwemo ya kushiriki vikao vya kutengeneza mikakati ya ugaidi pamoja na kukutwa na vifaa vya vilipuzi.

Mashtaka mengine ni kukutwa na silaha pamoja na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania( JWTZ), pamoja na dawa za kulevya aina ya Heroin.

Washtakiwa wao ni Halifa Hassan, Adam Kasekwa, maarufu (ADAMO) na Mohamed Lingwenya.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao, Agosti 19, 2020 na jopo la Mawakili watatu wa upande wa mashtaka, wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Shadrak Kimaro akisaidiana na Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon na Tulimanywa Majigo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Akiwasomea mashtaka yao, Wakili Simon alidai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na uhujumu uchumu namba 63/2020.

Simon amedai washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa yao kati ya Mei mosi 2020 na Agosti mosi, 2020 katika hotel ya Aishi iliyopo wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Washtakiwa kwa pamoja na wenzao ambao hawajafikishwa mahakamani wanadaiwa siku hiyo, waliongoza genge la uhalifu kwa kupanga, kushiriki vikao vya kutengeneza mikakati ya kigaidi.

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote mahakamani hapo kutokana na mashtaka yanayowakabili likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kutokuwana dhamana kwa mujibu wa sheria.

Upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi haujakamilika, hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 2, 2020 itakapotajwa
 
CCM ina miaka zaidi ya 48 babu zako wameshabikia CCM mpaka wamekufa maskini badala ya kukurithisha mali wamekurisisha chama cha CCM funguka kichwa hicho acha upimbi CCM ina miaka zaidi ya 48 babu zako wameshabikia CCM mpaka wamekufa maskini badala ya kukurithisha mali wamekurisisha chama cha CCM funguka kichwa hicho acha upimbi huo
 
Ndio mjue Kuna watu wanafanya kazi zao wakati wengine tukila maharage ya nazi na baada ya kuvimbiwa tunaingia JF na kuitusi serikali.

Just imagine hao jamaa wangefanikiwa azama yao,

Watu wangapi wangedhurika??
Kudhurika na nini? Kwani si ni tuhuma tu au wamekutwa na hatia?
 
Back
Top Bottom