Watu watatu walioiba Tausi wa Ikulu wahukumiwa kulipa fidia ya Sh. Mil 6

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Watu watatu waliokutwa na ndege watatu aina ya Tausi waliokuwa Ikulu wamehukumiwa kulipa fidia ya Sh. Mil 6 baada ya kupatikana hatia katika kesi ya Uhujumu Uchumi kwa kujihusisha na nyara za serikali bila kuwa na kibali.

Pia, washtakiwa hao wameachiwa huru kwa masharti ya kutofanya makosa kwa kipindi cha miezi sita na ndege watatu aina ya Tausi wataifishwe na wapelekwe serikalini.

Washtakiwa hao ni David Graha, Mohamed Hatibu na Mohamed Ally ambao wamehukumiwa ikiwa ni siku tano tangu wafikishwe mahakamani hapo.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi, Salum Ally ambapo amesema mahakama hiyo imezingatia masharti ya makubaliano ya washtakiwa hao wamekubali kuilipa Serikali fidia ya zaidi ya Sh.Mil 6.8.


 
Sijui wale tausi wetu waliotolewa ikulu na kupelekwa Chato walikuwa na kibali cha nani? Na wale waliogawiwa kwa Uhuru?
 
Back
Top Bottom