Watu watano wafariki dunia katika ajali iliyohusisha basi la Kyela Express na Coaster

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya, Diodes Ngaiza amesema, watu watano wamethibitika kufariki kutokanana na ajali kati ya basi la Kyela Express na basi dogo aina ya Toyota Coaster, huku majeruhi wakifikia 31.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu leo Jumanne Oktoba 11, Dk Ngaiza amesema kuwa kati ya majeruhi hao, 14 walikimbizwa katika hosptali ya Mission Igogwe, huku 17 katika hosptali ya Wilaya ambapo watatu walipoteza maisha wakipatiwa matibabu na wanne wamepewa Rufaa katika hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya (MZRH) kwa matibabu zaidi.

Chanzo: Mwananchi

Ajali.PNG
 
Dah
poleni wafiwa, badala ya binadamu kuendesha vyombo vya mote, vyenyewe vinatupa kiburi na kutuendesha
 
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dk Vincent Anney aliyetembelea eneo la ajali, amesema kuwa taarifa za awali zinaonyesha madereva wote wawili akiwemo dereva wa Coaster aliyemiongoni mwa waliofariki, akielezwa kuendesha kwa mwendo kasi na kutaka kulipita lori lililokuwa mbele yake na kusababisha kugongana uso kwa uso na basi la Kyela Express.

Ajali hiyo imetokea leo Jumanne Oktoba 11 majira ya saa 2.30 za asubihi katika kijiji cha Ibula Kata ya Kiwira iliyohusisha gari aina ya Costa iliyokuwa ikisafirisha msiba kutoka Dodoma kwenye Kyela mkoani hapa.

Hapa inaonyesha kama dereva wa Coaster aliendesha usiku kucha na alikuwa amechoka (fatigue) na akawa anafanya maamuzi yasiyo sahihi. Hivi kwa nini watu wanapenda kusafirisha misiba usiku? Madereva wengi wanakuwa hawajalala kabla ya safari, ajali zinazotokea sio balaa la kusafirisha msiba

Nililiongelea hili suala la ku-overtake, kwamba ajali nyingi sana za kugongana zinatokana na overtake mbaya, uzi huu hapa chini

Tahadhari kali kwa nyote mlio na magari binafsi; chunga sana na waambie wengine!

Nafikiri tuelewe kuwa tatizo si kusafiri usiku.
Tatizo ni kuhakikisha hata coaster inakuwa na madereva wawili au kabla ya safari lazima dereva awe amelala masaa zaidi ya nne.
Imagine safari inaanza baada ya kuaga saa 9 au 10, then safari haisimami hadi saa za asubuhi.
Dereva mchana wa siku iliyopita kabla ya safari mchan mzima yuko na mishe mishe zake.
Hapo hatuwezi kumlaumu mtu yeyote maana hayo ni majaribu yasiyo na tija, huwezi kulindwa mkiwa na dereva anasinzia barabarani.
Pole wafiwa.
 
Hio ibula ipi ? Katikati ya Katumba na KK hicho ni kijiji gani ibula, Au kibumbe na uwanja wa Ndege ndio ibula yenyewe? Daah au Ibula katikati ya ndulilo na KKK ?
 
Nafikiri tuelewe kuwa tatizo si kusafiri usiku.
Tatizo ni kuhakikisha hata coaster inakuwa na madereva wawili au kabla ya safari lazima dereva awe amelala masaa zaidi ya nne.
Imagine safari inaanza baada ya kuaga saa 9 au 10, then safari haisimami hadi saa za asubuhi.
Dereva mchana wa siku iliyopita kabla ya safari mchan mzima yuko na mishe mishe zake.
Hapo hatuwezi kumlaumu mtu yeyote maana hayo ni majaribu yasiyo na tija, huwezi kulindwa mkiwa na dereva anasinzia barabarani.
Pole wafiwa.
Mkuu, tatizo ni kusafiri usiku, kwa kuwa kama ulivyosema, mchana dereva anakuwa na mishe mishe ambazo haziepukiki - check gari sijui, akaage kule sijui. Mkisafiri asubuhi itamlazimisha kulala usiku. Hata ukilala mchana ukaendesha usiku kucha utasinzia tu. Mental clock inakuwa bado inajua kulala ni usiku. Ndio maana kuna kitu kinaitwa jetlag kwa wale wanaosafiri kwenda sehemu yenye masaa tofauti na walikotoka
 
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya, Diodes Ngaiza amesema, watu watano wamethibitika kufariki kutokanana na ajali kati ya basi la Kyela Express na basi dogo aina ya Toyota Coaster, huku majeruhi wakifikia 31.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu leo Jumanne Oktoba 11, Dk Ngaiza amesema kuwa kati ya majeruhi hao, 14 walikimbizwa katika hosptali ya Mission Igogwe, huku 17 katika hosptali ya Wilaya ambapo watatu walipoteza maisha wakipatiwa matibabu na wanne wamepewa Rufaa katika hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya (MZRH) kwa matibabu zaidi.

Chanzo: Mwananchi

View attachment 2383708
r.i.p junkiz
 
Msimu wa ajali za makafara umeanza
 
Mkuu, tatizo ni kusafiri usiku, kwa kuwa kama ulivyosema, mchana dereva anakuwa na mishe mishe ambazo haziepukiki - check gari sijui, akaage kule sijui. Mkisafiri asubuhi itamlazimisha kulala usiku. Hata ukilala mchana ukaendesha usiku kucha utasinzia tu. Mental clock inakuwa bado inajua kulala ni usiku. Ndio maana kuna kitu kinaitwa jetlag kwa wale wanaosafiri kwenda sehemu yenye masaa tofauti na walikotoka
Mkuu kusafiri kunahitaji discipline, na si kukurupuka na kuondoka kwa safari ndefu.
Mimi mwenyewe katika misiba na majnga kama hayo huwa tukiaga, naenda kulala kabisa kuanzia sa 122 hadi saa nne au tano usiku,
Hapo ingalau umepata kuondoa uchovu wa mchana.
Mara zote nawakuta waliotangulia pale Uyole asubuhi, kabl hawajaanza kupandisha milima ya Rungwe.
 
Back
Top Bottom