Watu watano wafariki dunia baada ya Lori kufeli breki kwenye mlima Mbalizi, Mbeya

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,353
Watu watano wamefariki Dunia na wengine wanne kujeruhiwa mkoani Mbeya baada ya Lori la Mizigo kufeli breki kwenye mteremko wa Mlima Mbalizi na kuyagonga magari madogo matatu, Bajaji na watembea kwa mguu.

==========================

Akizungumzia kuhusu taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema: “Tukio lililotokea ni Machi 27, 2022 baada ya Scania kufeli breki ikaenda kugonga Bajaji kisha ikagonga mwendesha pikipiki na kusababisha vifo vya watu wawili.

“Waliofariki ni Jermiah Mwasega na Suza Mbwiga ambaye alikuwa ni dereva wa bodaboda.”

Kuhusu madai ya watu watano kufariki amesema anachojua yeye waliofariki ni wawili na ndiyo ripoti aliyonayo.


==============================================

AJALI YA GARI KUACHA NJIA KUGONGA MAGARI 02 BAJAJI NA PIKIPIKI NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI.

Mnamo tarehe 27.03.2022 majira ya saa 21:18 usiku huko katika Barabara ya Mbeya – Tunduma, Kata ya Utengule Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya na Mkoa wa Mbeya.

Gari yenye namba za usajili T. 909 DQC na tela namba T.205 DSF aina ya Scania likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la ABDULRAZACK HASSAN alishindwa kulimudu gari hilo akiwa anashuka Mlima Lwambi baada ya kufeli break na kwenda kugonga Bajaji yenye namba ya usajili MC.999 CUD aina ya TVS King iliyokuwa uelekeo mmoja ikiendeshwa na SHUKRANI PAUL na kusababishia majeruhi.

Baada ya hapo ikagonga Gari yenye namba ya usajili T.128 ALE aina ya Nissan Double Cabin ikiendeshwa na EMMANUEL MAKONGANYA na kusababisha kifo kwa JEREMIAH MWASENGA ambaye alikuwa abiria kwenye gari hiyo, kisha kugonga Gari yenye namba ya usajili T.387 DBD aina ya Toyota Noah iliyokuwa ikiendeshwa na dereva ANYENGULILE MWAMULUKI na mwisho kugonga Pikipiki yenye namba ya usajili MC.205 ARK aina ya T-Better iliyokuwa ikiendeshwa SUSA MBWIGA na kumsababishia kifo.

Katika ajali hiyo watu wawili wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu Hospitali Teule ya Ifisi – Mbalizi.

Aidha, vyombo vyote vilivyohusika katika ajali hiyo vimeharibika. Chanzo cha ajali ni kufeli breki ya Gari Lori yenye namba ya usajili T.909 DQC/T.205 DSF Scania na kusababisha dereva kushindwa kulimudu Gari hilo.

Jeshi la Polisi mkoani hapa nilimshikilia Dereva wa Gari T.909 DQC/T.205 DSF Scania kwa hatua zaidi za kisheria.

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA


=======================================================

1.jpg


2.jpg
 
Daaah! Hizi ajali zimefululiza halafu haziondoki na mmoja ni 2+
 
Mbalizi kwenda kyela njia za huko bhana ni hatari sana

Bila kusahau kule chunya


R.I.p
 
Juzi pale mikumi, Morogoro, Lori limefeli brake na kuingia ndani ya nyumba iliyoko pembeni mwa barabara na kuuwa mtu mmoja..
 
Malori mengi yameoza oza. Yafanyiwe ukaguzi maalum. Yaani kea mbali tu unajua lile bovu ios linapita mbele ya trafiki
 
Trafik hawakagui vitu kama hivyo barabarani, hawahangaiki na mambo ya msingi hasa breki, taa kwenye malori na gari(nyingi jicho moja usiku na zingine hazina hata indicator lights/hazard lights) wanaangalia petty issues plus kuomba za chai, utasikia anahagaika na mbona huna fire extinguisher, mara reflector triangle utafikiri hata huko maporini wanazitumiaga wakati wanajazaga majani barabarani tu
 
Maskini Kamanda Mpinga aliyekua RPC Mbeya aliwahi kutolewa kafara na Mwendazake kwa kushushwa cheo. Kisa ni kwanini hakukagua gari lililotokea Tabora na kuja kupatia ajali Mbeya usiku mwingi kwa ku fail brake!!!

Marehemu alikua akitaka kula kichwa chako basi atakutafutia lolote la kukutosha na kukubandika nalo huku ukiwa huna pa kujitetea

R. I. P wote waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom