Mwl Razaq Mtele Malilo
Member
- Sep 29, 2016
- 34
- 83
Ameandika Mohammed Ghassani
WATU WASOJULIKANA
Usiombe wakujuwe, watu wasojulikana
Wala wasikutambuwe, kwa sura wala kwa jina
Wawe mbalimbali nawe, kwa usiku na mchana
Sababu wakikujuwa
Watakuja kuchukuwa
Kipoloni wakutie
Chatu wakamrushie
Nyamunyamu akakule
Nyafunyafu akumeze
Hao watu wasojulikana!
Kisha tutatangaziwa, watu wasojulikana
Ndio waliokutwaa, kwenda pasojulikana
Uchunguzi waendelea, kwa lisilojulikana
Kisha jalada la kesi
Lipotee kama moshi
Liyeyuke
Litoweke
Lende kusojulikana!
Mohammed K. Ghassani,
16 Disemba 2016
Bonn
WATU WASOJULIKANA
Usiombe wakujuwe, watu wasojulikana
Wala wasikutambuwe, kwa sura wala kwa jina
Wawe mbalimbali nawe, kwa usiku na mchana
Sababu wakikujuwa
Watakuja kuchukuwa
Kipoloni wakutie
Chatu wakamrushie
Nyamunyamu akakule
Nyafunyafu akumeze
Hao watu wasojulikana!
Kisha tutatangaziwa, watu wasojulikana
Ndio waliokutwaa, kwenda pasojulikana
Uchunguzi waendelea, kwa lisilojulikana
Kisha jalada la kesi
Lipotee kama moshi
Liyeyuke
Litoweke
Lende kusojulikana!
Mohammed K. Ghassani,
16 Disemba 2016
Bonn