Watu wanne wakamatwa kwa kutaka kuvuruga Mkutano wa Dk Slaa - Kata ya Mabamba Kibondo

Mabunu

Member
Oct 17, 2012
33
13
Jeshi la Polisi wilayani Kibondo limewakamata watu wanne kwa kosa la kutaka kuvuruga mkutano wa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk Wilbrod Slaa unaoendelea muda huu katika kata ya Mabamba wilayani Kibondo

Mwandishi wa Redio Kwizera Fm James Jovin amesema kuwa watu hao walikuwa na mabango yenye maneno yanayoonesha kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya CHADEMA ya kuwavua madaraka Zitto Kabwe na wenzake, lakini hata hivyo wameelekezwa sehemu ya kukaa ili mabango yao yaweze kusomwa vizuri na Dk Slaa, wamekaidi malelekezo hayo ambapo imebidi Dk Slaa aliagize jeshi la Polisi kuwakamata watu hao kwani mkutano huo ni kwa mujibu wa sheria

Watu hao ambao majina yao hayakujilikana papo hapo wamepelekwa kituo cha Polisi na Dk Slaa amemuagiza Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Kibondo kufuatilia kesi hiyo kwa ukaribu

Source;JAMES JOVIN, REDIO KWIZERA
 
Vijana watano wa CCM wamekamatwa baada ya kuleta fujo kwenye mkutano wa Dr Slaa unao fanyika kata ya Mabamba Mkoani Kigoma.

Mmoja wa vijana hao alikuwepo kwenye mkutano wa jana ambapo walipewa fursa ya kueleza wanachotaka na kuulizwa maswali, alijitambulisha kuwa ni mtoto wa katibu mwenezi wa CCM.

Nitawajuza zaidi.
 
Mhe. Zitto naamini wewe hakuwatuma na si hajabu hata sura zao uzitambui. Wanaccm watakuponza Mhe. na usipoangalia mmm!!!!.
 
Safi sana. Kamata hao wanaotumika na ZZK kwa ujira wa viroba.

Hakuna kuwachekea tena.
 
Kubishana na upepo wa mabadiliko ni kazi kubwa sana…yaani watu wanaoshindwa kusoma alama za nyakati nawaonea huruma sana!
 
Ha ha ha kwi kwi kwi kwi kwa hiyo ni watu watano wanne na sio luno la wananchi kama walivyotaka kutuaminisha mission aborted zitto jizike ungali mzima kwenu wamekukataa jana Kakonko watu wako wameshuhsuliwa na asa kibondo pole zitto mwisho wako kisiasa MACCM wamekuponza umeadhirika umesawajika,itakuchukua miaka kurudisha political respect tuliambiwa wana kigoma nzima hawataki ugeni wa katibu mkuu kumbe ni bra bra bra bra bra bra bra
 
Vijana watano wa ccm wamekamatwa baada ya kuleta fujo kwenye mkutano wa Dr Slaa unao fanyika kata ya Mabamba Mkoani Kigoma.

Mmoja wa vijana hao alikuwepo kwenye mkutano wa jana ambapo walipewa fursa ya kueleza wanachotaka na kuulizwa maswali, alijitambulisha kuwa ni mtoto wa katibu mwenezi wa CCM.

Nitawajuza zaidi.

Kinachofurahisha kwamba ni vijana wasio tosha wakati tuliaminishwa kuwa Kigoma nzima mara kutakuwa na maandamano makubwa ,ooh mara hiki na kile mwisho wa Zitto Kabwe amefurahi kwamba kuna watu wanaingiakwenye mgongano na polisi jambo maccm hataamrisha watolewe
 
Mkuu zote zile zilikuwa ni propaganda tu na hakuna chochote cha kuizuia Chadema kufanya siasa zao za ukombozi wa mara ya pili.
 
Jeshi la Polisi wilayani Kibondo limewakamata watu wanne kwa kosa la kutaka kuvuruga mkutano wa Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk Wilbrod Slaa unaoendelea muda huu katika kata ya Mabamba wilayani Kibondo

Mwandishi wa Redio Kwizera Fm James Jovin amesema kuwa watu hao walikuwa na mabango yenye maneno yanayoonesha kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya CHADEMA ya kuwavua madaraka Zitto Kabwe na wenzake, lakini hata hivyo wameelekezwa sehemu ya kukaa ili mabango yao yaweze kusomwa vizuri na Dk Slaa, wamekaidi malelekezo hayo ambapo imebidi Dk Slaa aliagize jeshi la Polisi kuwakamata watu hao kwani mkutano huo ni kwa mujibu wa sheria

Watu hao ambao majina yao hayakujilikana papo hapo wamepelekwa kituo cha Polisi na Dk Slaa amemuagiza Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Kibondo kufuatilia kesi hiyo kwa ukaribu

Source;JAMES JOVIN, REDIO KWIZERA

kwani mkutano wa chama cha siasa unafanyika wakati wa saa za kazi?
 
Vijana watano wa ccm wamekamatwa baada ya kuleta fujo kwenye mkutano wa Dr Slaa unao fanyika kata ya Mabamba Mkoani Kigoma.

Mmoja wa vijana hao alikuwepo kwenye mkutano wa jana ambapo walipewa fursa ya kueleza wanachotaka na kuulizwa maswali, alijitambulisha kuwa ni mtoto wa katibu mwenezi wa CCM.

Nitawajuza zaidi.

Mbona hueleweki wewe? kwani hakuna wapinzani wa DR SLAA na CC ambao ni wafuasi wa CHADEMA?
 
Tuntemeke hayupo katika hao??
ngoja aje ajibu hapa

Wewe nawe? hivi hujui TUNTEMEKE ni ID inayotumiwa na Masalia yaliyotimuliwa Chadema?
Kwa taharifa yako hao watu wako hapahapa Dar na wanashinda na keybord za computer from morning hadi majogoo
kwa kazi maalumu na malipo yao yanatoka Lumumba
 
Samahani kwa Kuchelewa kuwaletea taarifa ya Mkutano unaoendelea hapa Mabamba Kigomba wa Dr.slaaa,Kabla ya Kuanza kwa Mkutano Watu sita wameshakamatwa hapa,Vijana walioongoza maandamano ya Kupinga kung'olewa kwa Zitto kabwe.
Na taarifa zinasema Vijana wanne wamekamatwa jana Pale kakonko kwa Tuhuma za kubeba Mabango ya kupinga hatua za Kamati kuu ya CHADEMA kuwavua vyeo ZItto na Kitila kwa sababu yamejaa chuki,Ufamilia na Mchezo mchafu kuelekea uchaguzi wa ndani ya CHAMA.
Mwenyekiti wa Tawi hapa Mabamba yupo jukwaani muda huu anajiandaa kumkaribisha Dr.slaa

MORE UPDATES TO COME,

Dr.slaa amepanda jukwaani sasa anazungumzia kuwa Vijana wote wanaandamna na mabango yao ni walevi,Nitaagiza polisi aje akusanye wote wenye mabango hapa.Tuna vijana hawa wanaipa Nguvu CCM iliendelee kuongoza nchi na si jambo lingine.

TAAFIRA KUHUSU ZITTO,
Ni kweli taarifa mliosikia kuwa Zitto amechukuliwa hatua ni kweli amechukuliwa hatua,Kamati kuu nzima imekaa na kumvua vyeo,amepewa siku 14 za kujibu tuhuma alizoambiwa,Siku 14 kamati kuu itakaa tena na kujadili nini Zitto anastahili kufanyiwa,naomba mjue kuwa Zitto sio kwamba amefukuzwa CHADEMA,Zitto anaweza kurejea tena kwenye uongozi wa chama,hatujamfukuza,CHADEMA tunaiogopa katiba ya chama.

MKUTANO UMESIMAMA KWA MUDA KUPISHA ADHANA YA WAISLAMU,MSIKITINI IMESHAANZA KULIA HAPA.

Wakati adhana imetulia,Nipo nyuma ya jukwaa hapa nakutana na Tumaini Makene akiagiza vijana wa CHADEMA wasogezwe kwenye eneo la mkutano,watu wamekaa mbali na jukwaa kutokana na Jua kali,Hivyo wanahitaji kubembelezwa kusogea eneo la Mkutano.Vijana wengine wanang'ang'ania wenzao waachiwe ndipo wasogee kwenye mkutano wa slaa,Hali ya Ulinzi imeimarishwa sana hapa,Polisi wamejipanga na zana za kupambana na Vurugu zozote,gari la maji lililokuwepo jana Kakonko na leo wamelileta hapa.Watu ni wachache sana tofauti na mkutano wa jana ambao haukuwa na watu zaidi ya 50.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom