Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 648
- 1,459
Watu wanne wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa vipindi tofauti wakidaiwa kuhujumu miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Mara kadhaa TRC imekuwa ikieleza kuwapo kwa baadhi ya watu wanaokula njama za kuharibu miundombinu ili kuzorotesha usafiri wa treni ya kisasa (SGR).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkoa wa Kipolisi Rufiji, watuhumiwa wawili walikamatwa Desemba 13, 2024 wakiwa na vipande vya shaba 426 vyenye uzito wa kilo 7,728 na nyaya za shaba zenye uzito wa kilo 2,628.5 zilizotambuliwa kuwa ni mali zilizoibwa kutoka kwenye miundombinu ya Tanesco.
Pia wanadaiwa kukamatwa na nyaya za shaba za TRC zenye uzito wa kilo 430 na vipande vya shaba vilivyotengenezwa kutoka kwenye nyaya ambazo zimeibiwa Tanesco na TRC ili kuficha uhalisia wake.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa jana Desemba 14, 2024 watuhumiwa walipataikana baada ya kukamatwa gari aina ya Fuso lililobeba shehena ya vipande na nyaya za shaba walizotoa kiwandani kwao.