Watu wanne akiwemo mama wa miaka 80 mbaroni kwa dawa za kulevya kete 7447 Pemba

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Jeshi la Polisi mkoa wa kusini Pemba, linawashikilia watu wanne, akiwemo mama mwenye miaka 80, kwa tuhuma za kupatikana na bangi nyongo 554 na unga kete 7,447 zinazoaminika kuwa ni za dawa za kulevya, ndani ya nyumba wanayoishi eneo la Msingini wilaya ya Chake Chake kisiwani Pemba.

Akizungumza na pembatoday ofisini kwake Madungu Chake Chake, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ahmed Khamis Makarani, aliwataja wengine kuwa ni Haji Rashid Khamis, Naima Rashid Khamis wanaoaminika kuwa ni ndugu pamoja na Asia Luciano.

Alisema, baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema, walianza kuzifuatilia taarifa za kuwa nyumba hiyo inahusika na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Kamanda huyo, aliiambia pembatoday kuwa, baada ya kupata taarifa hizo, walitega mtego na juzi August 15 waliivamia nyumba hiyo na kukamata nyongo na kete hizo na kuwakamata watuhumiwa.

“Ni kweli kila siku huwa tunawataka wananchi watusaidie kutupa taarifa za kihalifu na walipotupa ndio tulikwenda na kufanikiwa kupata dawa hizo za kulevya,’’alieleza.

Alifahamisha kuwa, baada ya kuwapata waliwaweka chini ya ulinzi na kisha kuwafikisha kituo cha Polisi na tayari wanaendelea kuwahoji juu ya tuhuma zinazowakabili.

Kamanda huyo, alisema kazi iliyobakia baada ya hapo, ni kuyafikisha majalada yao ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka na baada ya wao kujiridhisha ni kuwafikisha mahakamani.


bangii.jpg
dawa-300x149.jpg


Hata hivyo Kamanda huyo wa Polisi, alisema kama kuna wananchi ndani ya mkoa wa kusini wanaendesha biashara hiyo haramu, waelewa kuwa hawako salama na iko siku watakamatwa.

“Kila anaefanyabiashara hii haramu aache mara moja na afanye iliohalali, maana hayuko salama atakamatwa tu na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria,’’alieleza.

Katika hatua nyingine, Kamanda huyo wa Polisi, aliendelea kuwanasihi wananchi kutoa taarifa za uhalifu katika maeneo yao, ili Jeshi la Polisi lifanye kazi yake.

Baadhi ya wananchi wa Chake Chake, waliokataa kutaja majina yao, walilipongeza Jeshi la Polisi, kwa kufuatilia taarifa walizozitoa wiki moja iliyopita.

Walisema Jeshi la Polisi la namna hiyo, ndio ambalo wanalihitaji katika kumaliza uhalifu ndani ya mkoa wa kusini Pemba, na kulishauri kuendelea kutotoa siri kwa wanaopeleka taarifa.

Matukio mengine yanayofanana na hayo ni yale yaliojiri Januari 28, mwaka huu, ambapo askari wa mji wa Bengaluru nchini India, walimkamata mtanzania mmoja mwanamke akiwa na vidonge 600 vya dawa za kulevya, zenye uzito wa gramu 250.

Aidha tukio jingine ni la Januari 20, mwaka 2017 ambapo Jeshi la Polisi mkoa wa Kaskazini Pemba, lilimkamata mwanamke mmoja miaka 50 wa Micheweni akiwa na mabunda 15 ya majani makavu yanayosadikiwa kuwa ni ya bangi.

Septemba 22 mwaka huo huo pia, Jeshi la Polisi kusini Pemba lilimkamata mwanamke mwengine akiwa na kete 969 zinazosadikiwa kuwa ni madawa ya kulevya, zilizokuwa zimehifadhiwa ndani ya mashine ya DVD.

Tukio jingine ni la Septemba 20, mwaka 2018 Jeshi la polisi mkoa wa kaskazini Unguja, lilimshikilia mwanamke mmoja kwa tuhuma za kukutwa na kete 218 za unga unaosadikiwa kuwa ni dawa za kulevya.
 
Back
Top Bottom