Watu wangu wanaangamia kwa kukosa Maarifa

Mkuu hebu tupatie ushahidi wa maandiko iwe kwenye vitabu vya dini au kisayansi kuthibitisha haya uyasemayo.
Soma vizuri asili ya mnyama mbwa chanzo chake sio mungu. Ndio mana huwezi kwenda mwituni ukakuta mbwa. Je wametoka wapi asili yao?
 
Kh
point yako ni nini kwani? kwahyo nasisi tukaishi na simba huko porini maana kumbe sisi ni ndugu,......na simba analitambua hilo kuwa sisi ni ndugu hatoning'ata?......
Akhaa! Rudia basi kusoma mada uielewe.
 
Mengi tuliyoyakuta katika ulimwengu huu tumekuwa waendelezaji tu ila kuhoji kwanini lazima hiki au kile au kwanini iwe hivi au vile, wachache sana ndiyo huwa wanahoji na majibu yao hushtua wengi.

Wengi tunaishi maisha tuliyoyakuta na tunaendeleza maisha hayo na tunaamini yale tuliyoyakuta ni sawa kabisa.

Ila deep down ulimwengu una siri nyingi sana na wachache wanaoelewa siri za ulimwengu ndiyo wanaotawala wengine wasioelewa siri hizo na wao huonekana kuwa na akili sana kuliko wengine.

Jaribu kuwa mtafiti wa masuala ya ulimwengu wa nyama na ulimwengu wa roho utakuja gundua vingi vya kushangaza sana.
 
point yako ni nini kwani? kwahyo nasisi tukaishi na simba huko porini maana kumbe sisi ni ndugu,......na simba analitambua hilo kuwa sisi ni ndugu hatoning'ata?......

Point yangu ipo wazi kwa mtu mwenye kufikiri. Kuna kitu amekiona hapo ambacho kinaweza kumpa maarifa ya kumsaidia au kubadilisha mfumo wake wa maisha.
 
Mengi tuliyoyakuta katika ulimwengu huu tumekuwa waendelezaji tu ila kuhoji kwanini lazima hiki au kile au kwanini iwe hivi au vile, wachache sana ndiyo huwa wanahoji na majibu yao hushtua wengi.

Wengi tunaishi maisha tuliyoyakuta na tunaendeleza maisha hayo na tunaamini yale tuliyoyakuta ni sawa kabisa.

Ila deep down ulimwengu una siri nyingi sana na wachache wanaoelewa siri za ulimwengu ndiyo wanaotawala wengine wasioelewa siri hizo na wao huonekana kuwa na akili sana kuliko wengine.

Jaribu kuwa mtafiti wa masuala ya ulimwengu wa nyama na ulimwengu wa roho utakuja gundua vingi vya kushangaza sana.

Asante sana uneandika vema sana kwa mtu wa kawaida kuweza kuelewa.
 
Husomi neno la Mungu ndio maana hata unaogopa mchawi.
Mwanzo 1:24-25
24) Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo. 25) Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

Wakufuga usilazimishe kumkuta msituni.
Hayawezi maisha ya uko.
Mungu alifanya wa kufuga toka kuanza kwa Adamu
Mkuu labda hata Bible tumepigwa mkuu maana waandishi ni wao
 
Mkuu jenu yupatie ushahidi wa maandiko iwe kwenye vitabu vya dini au kisayansi kuthibitisha haya uyasemayo.

Kiongozi ushahidi upo hapo embu soma tena au jiulize swali moja kwanini kila siku kuna breed mpya za mbwa zinatoka? Wanazitoa wapi? Au fanya utafiti juu ya kitu kinaitwa dog breeding utaweza kuelewa hawa viumbe sio wazuri. Hata mavi ya mbwa ni sumu ardhini sio mbolea unalijua hilo? Mbwa akijisaidia kwenye majani yanakauka mkojo wake pia ni sumu
 
Mkuu badison hoja yako kwenye bandiko hili ni nini hasa mbona tupo waafrika wenye maisha sawa au zaidi ya hao wazungu kuanzia umri wa kuishi na aspects zingine zote pia kuna wazungu wana maisha mabovu sawa tu na ya baadhi ya waafrika walio wengi.

Kuhusu nyama pori nimekula sana nyama ya mbuni, swala, tembo, pundamilia na ngiri tena katika kipindi cha makuzi yangu lakin mpaka leo naona bado DNA hazijawa activated ama hapa kuhusu DNA ulikua unamaanisha nini.
 
WATU WANGU WANAANGAMIZWA,SIO WANAANGAMIA.REKEBISHA HIYO TITTLE MKUU.NA HONGERA UMEANDIKA MAMBO YANAYOFIKIRISHA.

Kuangamizwa inamanisha huna chaguo au umelazimishwa ( huna choice) lakini wanaangamia manake wamekubali kwa hiari yao kuangamia kwa kutojikomboa na nafasi wanayo.
 
Mkuu badison hoja yako kwenye bandiko hili ni nini hasa mbona tupo waafrika wenye maisha sawa au zaidi ya hao wazungu kuanzia umri wa kuishi na aspects zingine zote pia kuna wazungu wana maisha mabovu sawa tu na ya baadhi ya waafrika walio wengi.

Kuhusu nyama pori nimekula sana nyama ya mbuni, swala, tembo, pundamilia na ngiri tena katika kipindi cha makuzi yangu lakin mpaka leo naona bado DNA hazijawa activated ama hapa kuhusu DNA ulikua unamaanisha nini.

Maisha yetu na wao hayapo sawa. Point za msingi hapo zipo nyingi sana. Nimezungumzia wanyama na nafaka (mimea). Umesha wahi kuhisi kwanini kuna kitu hakipo sawa katika mazingira yanayo tuzunguka jamii zetu hasa afrika hasa umaskini na migogoro isiyokwisha kuanzia ngazi ya familia, mtaa, kata, wilaya, mkoa hata nchi na nchi?

Mathalan tungekuwa hatuli ugali na wali kama ilivyokuwa kabla ya utumwa na ukoloni tungekuwa tunakula nini sasa hivi? ( zingatia nipe ushahidi unaoonuyesha kabla ya wazungu kuja kulikuwa na watu weusi wanalima mchele na mahindi nk) Au kabla ya wazungu hawajaleta hao wanyama wa kufuga nyumbani kwanini tulikuwa tunaishi maisha ya kuwinda ( hunting and gathering).

Moja Point iliyo wazi hapo ni kwamba kuna siri kubwa kuhusiana na aina vyakula tunavyokula watu weusi na wanyama tunaofuga majumbani kila siku ndio vimetufikisha hapa. Na watakao elewa hapa ndio msingi wa kujua hatua ya pili ni nini baada ya hii..

Ulikula hivyo vitu kwa kuchanganya lakini ukila chakula cha mtu mweusi kamili ndani ya siku 14 utaona tofauti kubwa kwani vyakula tunavyokula sisi sio vya kwetu kiasili vimeletwa.

You are what you eat. Na akili za mtu mweusi zimefungwa pineal gland hatuli tunashiba tuu ndo manahatuoni wala hatugundui.

Vyakula vya mtu mweusi ni Alkaline based food lakini wengi tunalishwa acidic food bila kujua.
 
Kuangamizwa inamanisha huna chaguo au umelazimishwa ( huna choice) lakini wanaangamia manake wamekubali kwa hiari yao kuangamia kwa kutojikomboa na nafasi wanayo.

Kuangamizwa inamanisha huna chaguo au umelazimishwa ( huna choice) lakini wanaangamia manake wamekubali kwa hiari yao kuangamia kwa kutojikomboa na nafasi wanayo.
I thought hiyo tittle imerefer HOSEA 4:6"Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa...." na sio waanaangamia.
Kama tittle yako it has nothing to do or somehow not related to this famous verse,hapo sawa.
 
It has nothing to do with the verse but Hosea 4:6 is my favorite verse of all the Time
 
Na vipi kuhusu wanyama mkuu nao tuliletewa baada ya ukoloni??
Historia inatuambia zamani kulikua na jamii za kifugaji na zile za kilimo, tuachanene na kilimo kwanza twende kwenye ufugaji walikua wanafuga nini sasa wakati wazungu hawajaja au aliens walifika kabla ya wazungu wakawaleta??

Nawasilisha
 
Ndiyo kiongozi wangu wanyama wote wa nyumbani au wakufungwa tuliletewa na wazungu ndo mana hakuna mwindaji yoyote katika historia aliwahi kuwinda mbuzi au ngombe.

Amini kwamba kuna baadhi ya watanzania wenzetu waliopo katika nafasi za nguvu wamewahi kupitia historia ya mataifa ya afrika namanisha historia ya kweli kutoka kwa WAKUU WA DUNIA ukitaka jambo lipo hapa hii sehemu inaitwa Archivum Apostolicum Vaticanum kuna watu wameingia hapa na wapo wamekaa kimya.

Wamasai na kabila la wafulani na jamii zingine za wafugaji waliingia Secret Pacts na wazungu kutokujihusisha na uponzani wowote au kupinga utawala wa wazungu hapa Tanzania na kuzawadiwa ngombe ndo mana hakuna vita au resistance yoyote ulisoma wamasai wamefanya. Kabla ya hapo wamasai walikuwa kama wahazabe tuu.

Soma tena uniambie inamana ngombe mbuzi na kondoo wametoka wapi au wameisha porini? Hawa kuku watu wanakula kila siku sio kuku wa kawaida hawaliwi. Kuku wanaoliwa ni wale Kanga wapo porini wana madoamadoa meusi wale ndio Mungu ametupa hawa kuku wengine kanjanja tuu hawaliwi wala hawana faida.
 
Back
Top Bottom