Watu wanene sasa kulipa nauli za watu wawili kwenye ndege!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watu wanene sasa kulipa nauli za watu wawili kwenye ndege!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GAMBLER, Jan 20, 2010.

 1. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2010
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vibonge Kuanza Kulipishwa Nauli za Watu Wawili Kwenye Ndege
  [​IMG]
  Mwanaume huyu kibonge alipigwa picha wakati wa safari yake mwaka jana kwenye ndege ya shirika la ndege la Marekani la American Airlines na kusababisha mjadala mkubwa kuhusiana na usalama wake kwenye ndege.Wednesday, January 20, 2010 7:03 AM
  Mashirika ya ndege ya KLM na Air France yataanza kuwalipisha nauli za watu wawili, watu wanene ambao wanashindwa kujibana kwenye siti moja.Watu wanene ambao hawaenei kwenye siti moja ya kwenye ndege watalazimika kulipa nauli za watu wawili iwapo watasafiri kwenye ndege za KLM na Air France.

  Msemaji wa mashirika hayo, Monique Matze, alisema kuwa watu wanene sana ambao hawatoshi kwenye siti moja watalazimika kulipia asilimia 75 ya nauli ya siti ya pili.

  Matze alisema kuwa uamuzi huo unatokana na sababu za kiusalama.

  "Inatubidi tuhakikishe kuwa mtu anaweza kujisogeza vizuri na abiria wote wanafunga mkanda ipasavyo kwenye ndege", alisema Matze.

  Watu ambao hawaenei kwenye siti moja watalazimika kufunga mkanda kwa kuunganisha mikanda ya siti mbili.

  Watu wanene wasiotosha kwenye siti moja watahakikishiwa kutengewa siti mbili watakazotakiwa kuzilipia wakati wa kununua tiketi.

  Sheria hiyo mpya itaanza kutumika kuanzia februari moja mwaka huu.

  Kiti cha ndege kawaida huwa na unene wa sentimeta 43 na kwa ndege za masafa marefu huwa na unene wa sentimeta 44.
   
 2. Soulbrother

  Soulbrother JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2010
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 408
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  This is fat discrimination! WE HAVE A RIGHT TO BE FAT
   
 3. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  For your health "To be fat is not healthy!" Fat ur a**s!
   
 4. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  wembamba dili kumbe
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hapa ishu ni number of seats anazotumia.
  Kama ni mbili , automatically ni lazima azilipie zoe, short and clear!
   
 6. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2010
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Naisubiri sheria hiyo kwenye Dala dala bongo
  lazima pachimbike
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mh Mgana Msindai

  Mh John Komba

  Mh Dr Rev Rwakatare mpo?
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,451
  Likes Received: 5,700
  Trophy Points: 280
  jamani hii si kuadvertise gym's
  sasa tusio na uwezo ndege tusipande
  loh
   
Loading...