Watu wanapotea, wanakufa lakini wanasiasa na Viongozi wa dini kwao siyo agenda

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Kuna taarifa zakupotea vijana watano zinasambaa mitandaoni Lakini hakuna kiuongozi wa serikali aliyetia Beno, wote wapo kimya kama vile waliopotea siyo watu. Viongozi wa dini nao wapo kimya utadhani Hawa siyo waumini wao.

Ni lini mliopewa dhamana mtachukulia haya mambo kwa uzito wake? Six years same story na tunaamini tupo salama miyoyoni? Tunaposikia visa vya mauaji tukakaa kimya tunasubiri wafe au wapotee ndugu zetu?

Nani katufundisha kukalia kimya nafsi zinapopotea au kufa? Kwamba tunaamini wapo wanaolindwa waishi na wapo wanaotakiwa kutolindwa? Hawa siyo wanyama, ukimya huu unapanda chuki na ubaguzi kuhusu Haki ya kuishi Kwa watu waliopo Tanzania, tafakarini
 
Tanzania kuna wananchi au misukule tu!!yaani utegemee mwanasiasa atetee mtu asiyejitambua kweli? Angalia wanasiasa kwa watu wanaojitambua wanavyopata shida?

Mfano balaa analolipata Pm wa Uk, kwa afrika eti kiongozi kushiriki hafla wakati wengine wako ndani, nalo aambiwe ajiuzuru?!! Na hata wabunge wa chama chake baadhi wamkomalie?
 
Binafsi kilichoniboa zaidi ni kauli ya kamanda wa polisi jinsi alivyoichukulia hiyo taarifa kimzaha mzaha.

Kuna wasaa hawa makamanda wa polisi wanazungumza utumbo kweli.

We umeambiwa vijana watano wenye umri kati ya miaka 29-33 wamepotea zaidi ya mwezi; unafananisha na taarifa za watoto wadogo kupotea kwenye ngoma ya mdundiko kwa masaa.

Sometimes hawa watu wanakuwa very insensitive kwa familia za ndugu; very stupid.
 
Kuna taarifa zakupotea vijana watano zinasambaa mitandaoni Lakini hakuna kiuongozi wa serikali aliyetia Beno, wote wapo kimya kama vile waliopotea siyo watu. Viongoz wa dini nao wapo kimya utadhani Hawa siyo waumini wao...
The death of one person is tragedy,the death of many people is statistics.

Nchi ina watu milioni 55+wakifa watu 5!! It's none issue,unless Kuna ugonjwa wa mlipuko unawaua au Kuna kitu kisicho Cha kawaida kinawaua!!!
 
The death of one person is tragedy,the death of many people is statistics.
Nchi ina watu milioni 55+wakifa watu 5!! It's none issue,unless Kuna ugonjwa wa mlipuko unawaua au Kuna kitu kisicho Cha kawaida kinawaua!!!
Katika hao watano labda wawe wanao, ndo utaelewa kama ni issue au non issue........
 
Kuna taarifa zakupotea vijana watano zinasambaa mitandaoni Lakini hakuna kiuongozi wa serikali aliyetia Beno, wote wapo kimya kama vile waliopotea siyo watu. Viongoz wa dini nao wapo kimya utadhani Hawa siyo waumini wao...
Hivi kwanini ndugu wa watu wanaopotea au kupotezwa hawajitokezagi kuongea na vyombo vya habari?! Angalau jamii pana ijue tatizo. Hii itasaidia vyombo vya Dola kuona aibu Na kuchukua hatua.
 
Ingekua enzi za JPM yangetoka matamko ya kutosha...now wanaona aibu kuzungumza maana waliekua wanambebesha lawama hayupo tena. wanashindwa kusimamia haki, wanasimamia unafiki.

Kuna kamanda wa cdm nlisoma nae primary alipotea mwaka jana mwishoni akapatikana Mochwari sokotoure hospitali amefariki tukasafirisha kimya kimya bila zile purukushani za miaka iliyopita, which made me think sana, zile purukushani za enzi za JPM kila kamanda akipatwa na majanga zimeishia wapi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom