Watu wanaoogopwa sana

Jmujun

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
965
525
HABARI wana JF,
Hapa duniani kwa sisi binadamu inasemekana tumeumbwa kwa nguvu sawa. Nguvu ambayo inaonekana wakati mwingine ni uwezo kwa mtu yoyote wa kufanya kitu japo chochote na kila mtu ana kipaji chake, lakini inatokea baadhi ya watu kutofahamu vipaji vyao ambayo ndo nguvu pekee waliyopewa.

Kwa mfano kuna watu huwa wanaogopwa sana katika jamii, si kwa uchawi, si kwa imani zao za dini, wala si kwa matendo yao kiujumla, hawa watu hupewa heshima, staa, uhuru, wadhifa, upendo kuliko watu wengine.

Mimi binafsi sielewi huwa ni kwanini inatokea hivo. Kwanini watu hao wapewe vipaumbele kwenye maisha yao ya kila siku kuliko watu wengine na ilihali watu tumeumbwa sawa na tumepewa nguvu sawa?

Kama wakuu mna chochote juu ya hili share na mimi nipate hiyo elimu.

Asanteni.
 
Mkuu ungeweka na mifano ya watu wanaojulikana kuwa na hiyo rangi ili tuweze kweli kuthibitisha unachokiamini
 
simaanishi rangi mkuu, hiyo title nilitaka iwe pink but imeshindikana, soma post nzima pengine unaweza nielewa nachokimanisha
 
Hauwezi kupata heshima au kuogopewa bila ya sababu flani. mfano
1) Magufuli anaogopwa kwasasa mara anakutumbua
2) Mtaa wa Temeke wanawake wanaogopa kupita peke zao kwasababu mateja mara wanaiba kila walichonacho.
3) Mabosi wa ofisini wanaogopwa wanaweza kukufukuza kazi au hutembea na wake za watu.
4) Mhuni wa mtaani(Deebo) anaogopewa hachelewi kumpa mtu kichapo.
 
Back
Top Bottom