Watu wanaodhaniwa kuwa ni Polisi, wazingira nyumba ya askofu Gwajima

There comes a time when a man is gotta do what a man is gotta do, own up to one's misdeeds - confess the truth.
 
Wanaenda kuchukua ushahidi wa zero za bashite...natumaini mchungaji kazitunza mahala salama..
Mchungaji alikuwa jasiri akaenda Polisi mapema kuitukia mwito, kabla ya siku aliyoambiwa. Pia alisema mwenyewe kuwa baada ya kusikia habari ya kuitakiwa kuripoti Polisi, akikatisha safari zake za kuhubiri.

Inakuwaje awe na ushahidi wa kumtuhumu mbaya wake, akijazia maneno ya kashfa na dua baya, asitoe ushahidi huko huko madhabahuni alikofikisha hizo tuhuma, kama kuupeleta kwenye vyombo husika!
 
Wewe umeishia la ngapi? tangu lini ukipata zero unapata cheti? mchungaji wenu anawadanganya nyie , sijawai kuona.
Umewahi kupata zero?!? Nenda baraza utapewa...ukifika waambie "nimepata zero" utaona wataakachokupa...halafu urudi hapa..
 
Ha ha ha haaaa... Wanataka kuchukua vile vyeti vya Bashite! Ujingaje! Hivi wanadhani kwa akili ya kawaida vitakua hapo ndani? Hata kama vipo wanadhani hajapiga copy? Tunajua na maelekezo kutoka juu ila wanakurupuka sana, hata mini nawazidi technics za kiintelijinsia jamani?
watakutafuta Mkuu
 
Kwa maelekezo ya Askofu Dr Josephat Mathias Gwajima; Taarifa kuhusu tukio lililotokea leo Tarehe 28th February 2017 nyumbani kwake Salalasa, Kinondoni, Dar es Salaam.

Mnamo majira ya saa 7.45 za mchana walifika nje ya geti lake watu wapatao 9, ambao walikuwa katika gari ambalo lilionekana kama la Jeshi la Polisi. Mmoja wao alimpigia simu Askofu Gwajima na kujitambulisha wao kama Askari kutoka kituo cha Polisi Kati (Central Police Station) na kumuomba afungue geti/aelekeze geti lifunguliwe ili waweze kuingia kwa shughuli za ki-Polisi. Walijitambulisha zaidi kwamba wamekwenda kwa Askofu Gwajima kwa maelekezo ya Uongozi wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam.

Askofu Gwajima akawaomba awasiliane nami Wakili wake kwanza ili kufahamu haki na wajibu wake katika mazingira yale. Maelekezo niliyompa ni kwamba wajitambulishe bila shaka wao ni kina nani, na kama kweli ni Polisi basi wamfahamishe iwapo wanahitaji kumkamata au kumfanyia upekuzi, na iwapo wana nyaraka husika za kisheria kuhusiana na mojawapo ya mazoezi hayo. Pia wamfahamishe tuhuma husika. Alichojibiwa ni kwamba 'wana nyaraka zote', na wakasisitiza awafungulie geti ili wafanye kile walichokiita 'Observation'.

Askofu Gwajima alisisitiza kwamba ni muhimu afahamishwe kinagaubaga zoezi husika, na iwapo zoezi hilo linaambatana na nyaraka husika, hasa kwa kuwa walijitambulisha wanatoka Kituo cha Polisi Kati; mwendo mrefu kutoka nyumbani kwa Askofu Gwajima na umbali unaoletelea dhanio la maandalizi ya kutosha.

Baada ya stand-off iliyotokana na hayo hapo juu, watu hao waliondoka eneo husika mnamo majira ya saa 9.15 hivi za alasiri.

Askofu Gwajima anaendelea na shughuli zake, na kama kuna zoezi lolote la kisheria linalokusudiwa kufanyika, basi atashirikiana nalo bila kusita kama raia mwema; mradi tu liwe katika kiwango cha ufuataji wa sheria za kichunguzi, na utawala wa sheria.
 
Back
Top Bottom