Watu wanaodhaniwa kuwa ni Polisi, wazingira nyumba ya askofu Gwajima

Kwa maelekezo ya Askofu Dr Josephat Mathias Gwajima; Taarifa kuhusu tukio lililotokea leo Tarehe 28th February 2017 nyumbani kwake Salalasa, Kinondoni, Dar es Salaam.

Mnamo majira ya saa 7.45 za mchana walifika nje ya geti lake watu wapatao 9, ambao walikuwa katika gari ambalo lilionekana kama la Jeshi la Polisi. Mmoja wao alimpigia simu Askofu Gwajima na kujitambulisha wao kama Askari kutoka kituo cha Polisi Kati (Central Police Station) na kumuomba afungue geti/aelekeze geti lifunguliwe ili waweze kuingia kwa shughuli za ki-Polisi. Walijitambulisha zaidi kwamba wamekwenda kwa Askofu Gwajima kwa maelekezo ya Uongozi wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam.

Askofu Gwajima akawaomba awasiliane nami Wakili wake kwanza ili kufahamu haki na wajibu wake katika mazingira yale. Maelekezo niliyompa ni kwamba wajitambulishe bila shaka wao ni kina nani, na kama kweli ni Polisi basi wamfahamishe iwapo wanahitaji kumkamata au kumfanyia upekuzi, na iwapo wana nyaraka husika za kisheria kuhusiana na mojawapo ya mazoezi hayo. Pia wamfahamishe tuhuma husika. Alichojibiwa ni kwamba 'wana nyaraka zote', na wakasisitiza awafungulie geti ili wafanye kile walichokiita 'Observation'.

Askofu Gwajima alisisitiza kwamba ni muhimu afahamishwe kinagaubaga zoezi husika, na iwapo zoezi hilo linaambatana na nyaraka husika, hasa kwa kuwa walijitambulisha wanatoka Kituo cha Polisi Kati; mwendo mrefu kutoka nyumbani kwa Askofu Gwajima na umbali unaoletelea dhanio la maandalizi ya kutosha.

Baada ya stand-off iliyotokana na hayo hapo juu, watu hao waliondoka eneo husika mnamo majira ya saa 9.15 hivi za alasiri.

Askofu Gwajima anaendelea na shughuli zake, na kama kuna zoezi lolote la kisheria linalokusudiwa kufanyika, basi atashirikiana nalo bila kusita kama raia mwema; mradi tu liwe katika kiwango cha ufuataji wa sheria za kichunguzi, na utawala wa sheria.
Ewe mungu mbariki wakili Peter Kibatala pamoja na cdm famili popote pale walipo
 
Huku Gwajima, kule Bashite, hapa Mama Salama Kikwete. Lazima tusahau mambo yote muhimu, mtaani siku hizi wanakula chapati asubuhi, mchana na jioni kisa mahindi yamepanda. Nchi hovyo kabisa.
 
Cheti kile cha Daudi Bashite alichojipatia Zeroooo je anacho home?? Kuharibu evidence ili tukupeleke mahakamani ni muhimu.
Hakika kama hujailipia ile treni uloagiza, utakiona kilichomfanya kuku asikojoe. Hii ni Bongo yetu ya mwendo kasi
Inawezekana ulikuwa ni mpango wa Bashite kwenda kuchomoa hivyo vyeti
 
d8b1e7b29a0c08cb991cc13b9d2a1476.jpg
Duuu ni miswaki tupu
 
Najitahidi kuipenda serikali yangu ila nayo inajitahidi kunichukiza!!

Mheshimiwa rais, tenda haki bhana. Mbona tunao vijana wasomi wengi. Achana na Bashite
 
Inawezekana ulikuwa ni mpango wa Bashite kwenda kuchomoa hivyo vyeti

Mkuu;
Huo ndo mpango mkakati wa Daudi. Akiisha kukiharibu, aweze kumpeleka mahakamani amfidie hela yoote ya treni. Wadhani sote tunamkenulia meno Gwaji??
 
Namuonea huruma bashite maana amempa wakati mgumu mkuu wakaya lafiki yake kipeeeenziiiii.
 
Nilipoisikia clip ya Gwajima anasema Vyeti vya Bashite anavyo nikajua muda wowote Polisi watamfanyia ambush. Bado Ofisini kwake lazima wataenda tu.
 
Najaribu kuona mbele..Naona kuna mtu kabla ya 2020 Atakuwa yupo Ndani kwa mashataka Ya Kubabikiwa..Serikali zetu za Afrika uwa azipo Fair kwa watu TYPE ya Gwajima
 
Back
Top Bottom