kitumbotala
JF-Expert Member
- Aug 6, 2015
- 516
- 623
Hodi humu ndani wananzengo.. Nimepata nyepesi hapa, kutoka mitandaoni kuwa polisi wetu wameizunguka nyumba ya Askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.
Mwenye habari kamili alete humu ukumbini...
=====
Update:
=====
=> Watu wanaodhaniwa kuwa ni polisi wamezingira Nyumba ya Askofu Mkuu wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima huko Salasala.
Bado haijafahamika wanatafuta nini.
1515hrs
=>Watu hao walitumia gari aina ya land cruiser, lakini wameondoka sasa hivi na haijajulikana kama watarudi tena.
2110hrs
=> TAARIFA YA WAKILI WA ASKOFU GWAJIMA PETER KIBATALA
Kwa maelekezo ya Askofu Dr Josephat Mathias Gwajima; Taarifa kuhusu tukio lililotokea leo Tarehe 01 Machi 2017 nyumbani kwake Salalasa, Kinondoni, Dar es Salaam.
Mnamo majira ya saa 7.45 za mchana walifika nje ya geti lake watu wapatao 9, ambao walikuwa katika gari ambalo lilionekana kama la Jeshi la Polisi. Mmoja wao alimpigia simu Askofu Gwajima na kujitambulisha wao kama Askari kutoka kituo cha Polisi Kati (Central Police Station) na kumuomba afungue geti/aelekeze geti lifunguliwe ili waweze kuingia kwa shughuli za ki-Polisi. Walijitambulisha zaidi kwamba wamekwenda kwa Askofu Gwajima kwa maelekezo ya Uongozi wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam.
Askofu Gwajima akawaomba awasiliane nami Wakili wake kwanza ili kufahamu haki na wajibu wake katika mazingira yale. Maelekezo niliyompa ni kwamba wajitambulishe bila shaka wao ni kina nani, na kama kweli ni Polisi basi wamfahamishe iwapo wanahitaji kumkamata au kumfanyia upekuzi, na iwapo wana nyaraka husika za kisheria kuhusiana na mojawapo ya mazoezi hayo. Pia wamfahamishe tuhuma husika. Alichojibiwa ni kwamba 'wana nyaraka zote', na wakasisitiza awafungulie geti ili wafanye kile walichokiita 'Observation'.
Askofu Gwajima alisisitiza kwamba ni muhimu afahamishwe kinagaubaga zoezi husika, na iwapo zoezi hilo linaambatana na nyaraka husika, hasa kwa kuwa walijitambulisha wanatoka Kituo cha Polisi Kati; mwendo mrefu kutoka nyumbani kwa Askofu Gwajima na umbali unaoletelea dhanio la maandalizi ya kutosha.
Baada ya stand-off iliyotokana na hayo hapo juu, watu hao waliondoka eneo husika mnamo majira ya saa 9.15 hivi za alasiri.
Askofu Gwajima anaendelea na shughuli zake, na kama kuna zoezi lolote la kisheria linalokusudiwa kufanyika, basi atashirikiana nalo bila kusita kama raia mwema; mradi tu liwe katika kiwango cha ufuataji wa sheria za kichunguzi, na utawala wa sheria.