Watu wananiomba sana pesa..wajuzi wa mambo hii inaashiria nini

Wu-Ma

Senior Member
Dec 1, 2017
113
277
Nimekuwa nikipata changamoto ya kuombwa hela na watu wa makamo mbalimbali kuanzia watoto, vijana na hata wazee, nikiwa mtaani hata barabarani natembea utastukia mtu anakuja kwa sura ya upole akikuelezea matatizo yake na anahtaj msaada wa pesa.

Hata watoto wa shule hunikimbilia wanionapo njiani na kuniomba hela ya nauli tsh 200 au pesa ya kalamu, hali hii ilikuwa imeniandama sana jijini Mwanza na hata nilipokuwa Dsm hali hii ilinitokea pia pale ubungo mara anatokea dada anakueleza matatizo yake na anaomba msaada wa fedha kdogo.

Ukitembea njiani unakutana na baba anakuketisha pembeni anakuelezea shida yake na anahtaji msaada nimetembea Iringa, Mbeya, Tanga, na Manyara hali hii imekuwa ikinitokea sana...naweza kuwa hata katikati ya kundi la watu utashangaa mtu usiyemfahamu ananikimbilia na kuniomba msaada wa pesa..mara nyingi nimekuwa nikitoa msaada huo.

Imefikia hatua nimeanza kuingiwa na waswas.....naomba wajuzi wa mambo haya wanisaidie hii inaashiria nini.

ahsante
 
Unaandamwa Na ALAYE.


Malaki : Mlango 3

11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema BWANA wa majeshi
 
Mkuu naomba unipe channel za kutoka kimaisha, mimi ni jobless kwa sasa.
 
Imeanza zamani tangu nikiwa mdogo ila imeshamiri hasa nilipomaliza form six 2012
ALAYE yuko busy kuharibu mipango yako. Hiyo ni roho ya shetani yenye mipango mahususi ya kukurudisha nyuma.
Sadaka ni ibada Na inataratibu zake. Baraka zinapatikana kwa utoaji wa sadaka Na sio ufanyaji wa HISANI.
Unapo ombwa ukatoa, hiyo siyo sadaka ni hisani.
Sadaka ni msukumo wa kutoa ambao kwa dhati huanzia moyoni.
Sadaka hunenewa kabla ya kutolewa Na hurejesha majibu.
 
Uso wako una mafuta, si bure.

Sasa ni lazimauwe na hela, maisha yashakupa changamoto kwamba unanukiahela hela tu.

Mimi nilifikirini vyuma vya Magufuli tu vinabana. Kumbe tangu Kikwete na kabla?
Hivi USO ukiwa na mafuta hii hali inaweza kutokea et boss? Maana mm pia kuna karespect flan nakapataga mtaan ambako si kakawaida kwa hali yangu,
 
Mkuu nataka nikuambie kitu ambacho nimekishuhudia baba yngu mdogo yeye Mara kwa mara anaombwa pesa na watu wenye uhitaji toka akiwa mdogo kabisa kuanzia miaka 2 alikua nimtu mwenye roho nzuri na moyo wakutoa,Marehemu bibi alimwambia mwanangu endelea na moyo huo utakuja kua mtu mwenye Mafanikio na kweki leo nimtu mwenye mafanikio so nimejifunza kujitoa kwa ajili ya wenye uhitaji ni ibada kubwa sana
 
Watu wanaweza chukulia utani ,hii issue ya mleta Uzi.....ila mambo haya yanatukuta na kututokea binafsi ni mimi mmoja wao...mpaka huwa nawaza why me kuombwa hela?? Twaweza kuwa watatu njiani ,lakn nikawa appointed Mimi na sura yangu ni ya kibandidu haswa mpaka namuonea huruma wife kwa kunipenda....
So plz tunaomba USHAURI..
 
Watu wanaweza chukulia utani ,hii issue ya mleta Uzi.....ila mambo haya yanatukuta na kututokea binafsi ni mimi mmoja wao...mpaka huwa nawaza why me kuombwa hela?? Twaweza kuwa watatu njiani ,lakn nikawa appointed Mimi na sura yangu ni ya kibandidu haswa mpaka namuonea huruma wife kwa kunipenda....
So plz tunaomba USHAURI..
Haya mambo mm naamini yanategemea moja appearance ya MTU, km una appearance nzur yan mavaZ nk mtu ni rahis sana kukueleza shida yake, pili wanaangalia sura ya mtu , kuna sura zngne huwa znamvuta mtu kujieleza bila hofu , tatu unavyojiweka kwenye kund LA watu , yan hata km kuna kitu kmetokea ktk hilo kund cha kukuudh but inakichukulia cha kawaida tu , yan sio mtu Wa kuonyesha hasira zako hadharani,,, pia kuish kuendana na mazngra uliyopo , yan ukiwa na watoto unajishusha , ukiwa na vijana unachangia kwenye mada wanazojadl , ukija kwenye kund LA wazee unajishusha na kufwata kile wanachopenda wazee,,,
Pia maongez ya mdomon , unaongea kwa busara na point tupu
 
Uso wako una mafuta, si bure.

Sasa ni lazimauwe na hela, maisha yashakupa changamoto kwamba unanukiahela hela tu.

Mimi nilifikirini vyuma vya Magufuli tu vinabana. Kumbe tangu Kikwete na kabla?
Apunguze kupaka mafuta ya nazi usoni
 
Back
Top Bottom