Watu wanaangamia kwa kula vyakula vyenye sumu kwa sababu wakulima hawana taaluma ya kilimo bora

G-Mdadisi

Member
Feb 15, 2018
43
95
KATIKA kuhakikisha lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao bora ya Viungo, Mboga na Matunda yenye kuzingatia matumizi madogo ya pembejeo za kemikali, wataalam wa kili mo kupitia mradi wa Viungo Pemba wameshauriwa kutumia zaidi mbinu za viwango endelevu vya hiari kwa wakulima ili kufikia malengo hayo.

Rai hiyo imetolewa na afisa anayeshughulika na biashara na masoko, Omar Mtarika wakati wa mafunzo kwa wataalam wa kilimo kisiwani Pemba kupitia mradi huo yenye lengo la kuwapatia wataalam hao taaluma ya mbinu bora za kutumia kuwafundisha wakulima juu ya mbinu bora za uzalishaji wa mazao hayo.

Alisema ni jukumu la wataalam wa kilimo kupitia mradi huo kutumia taaluma yao kwa kutoa taarifa sahihi kwa wakulima kuhusu matumizi bora ya ardhi pamoja na pembejeo za kilimo ili kuzalisha bidhaa bora na salama kwa walaji.

“Lengo la mradi wa huu ni kuhakikisha unawawezesha wakulima kuzalisha mazao bora, kwa wingi na kwa uendelevu, ili wakulima waweze kufikia malengo haya ni lazima waelimishwe kuhusu taaluma hii ya viwango endelevu vya hiari kwa wakulima ili kusudi wazalishe kwa kuzingatia misingi ya kibiashara,” alisema.

Aidha alibainisha kuwa ufikiaji wa malengo ya mradi huo ni lazima wakulima wawe na uwezo wa kulima kilimo endelevu chenye kuzingatia uhifadhi wa mazingira pamoja na masuala ya kijamii.

Aliongeza kwamba, ufikiaji wa malengo ya mradi yatapatikana kupitia wataalam hao kuwaelimisha zaidi wakulima kuhusu mbinu za kupunguza matumizi ya sumu yasiyo ya lazima katika mazao kwa kuzingatia vigezo vya haki za kibinadaam, mabadiliko ya tabianchi, uhifadhi wa maji na nishati.

Alisema, “Kufanya hivyo kutasaidia sana malengo ya mradi kukuza masoko endelevu ya biashara za wakulima zinazozalishwa kufanikiwa kwa haraka kutokana na wateja wengi duniani wako tayari kununua bidhaa zilizozalishwa kwa ubora wa hali ya juu bila kuwa na chembechembe za sumu katika uzalishaji wake.”

Meneja wa mradi huo kanda ya Pemba, Sharif Maalim Hamad alisema kutokana na muundo wa mradi kuhitaji upatikanaji wa matokeo chanya kwa wakulima kiuzalishaji na masoko, mafunzo hayo yameandaliwa ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha elimu ya kilimo hicho inawafikia wakulima wengi kwa wakati kupitia wataalam hao katika shehia zao.

“Mafunzo haya tumeyaandaa kwa lengo moja tu kuhakikisha tunawaomgezea taaluma wataalam hawa ili wakatoe elimu ya vigezo bora vya kilimo kwa mjibu wa malengo ya mradi huu kutokana na kwamba wataalam hawa wanatoka katika kila shehia ambazo mradi unatekelezwa,” alisema.

Katika hatua nyingine alibainisha kwamba mafunzo hayo yamejikita zaidi katika utoaji wa taaluma ya kilimo chenye kuzingatia mabadiliko ya tabianchi, vigezo bora vya kilimo, bustani ya jikoni pamoja na viwango endelevu vya hiari kwa wakulima.

Mafunzo hayo ni mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa Viungo, Mboga na Matunda unaotekelezwa Zanzibar na taaasisi za People’s Development Forum (PDF), Community Forests Pemba (CFP) na Chama cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA Zanzibar) kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya.

VIUNGO.jpg
 
Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
6,366
2,000
Siku hizi kupata chakula original ngumu sana. Tunalishwa ma hybrid hadi sio vizuri.

Nashangaa siku hizi wali unapikwa jikoni wewe upo sebuleni ata harufu hauisikii. Enzi me nakua nyumba ya jirani wakipiga ubweche huku nyie mnateseka tu na harufu.
 
G-Mdadisi

Member
Feb 15, 2018
43
95
Siku hizi kupata chakula original ngumu sana. Tunalishwa ma hybrid hadi sio vizuri.

Nashangaa siku hizi wali unapikwa jikoni wewe upo sebuleni ata harufu hauisikii. Enzi me nakua nyumba ya jirani wakipiga ubweche huku nyie mnateseka tu na harufu.
Tatizo kubwa linaanzia kwa wataalamu wa kilimo tulionao wengi wamehodhi majukumu yao na kuyafanya kuwa majukumu ya ofosini na kuacha kuwafikia wakulima kuwapa taaluma ya uzalishaji bora wa mazao bila kutumia dawa zenye sumu.
 
Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
7,742
2,000
Mkulima anajali kupiga hela, suala la afya yako ni jukumu lako mwenyewe.
 
t blj

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
2,800
2,000
Tunalaumu wakulima bila sababu, food demands za ulimwengu haziwezi tena kuwa sustained na natural products . Ili kupunguza hiyo gap ndo hizi hybrids products zinapoingilia Kati Ili walau kuokoa , na ndo humo tunakula na sumu pia .

Mazao Siku hizi yamekuwa engineered kutoa maximum yield na ku resist hata magugu na shida ndo zinaanza hapo.
 
G-Mdadisi

Member
Feb 15, 2018
43
95
Tunalaumu wakulima bila sababu, food demands za ulimwengu haziwezi tena kuwa sustained na natural products . Ili kupunguza hiyo gap ndo hizi hybrids products zinapoingilia Kati Ili walau kuokoa , na ndo humo tunakula na sumu pia .

Mazao Siku hizi yamekuwa engineered kutoa maximum yield na ku resist hata magugu na shida ndo zinaanza hapo
Well... na hapa ndipo tatizo linanzia. Wakulima wanauziwa mbegu, mbolea, dawa zenye sumu pasipo kuelekezwa vya kitosha namna gani waweze kuvitumia kwa ulinzi wa afya ya mlaji.

Bado shida kubwa ipo kwa wataalam wa Kilimo hawatekelezi majukumu yao ya kwenda shambani.
 
t blj

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
2,800
2,000
Tatizo kubwa linaanzia kwa wataalamu wa kilimo tulionao wengi wamehodhi majukumu yao na kuyafanya kuwa majukumu ya ofosini na kuacha kuwafikia wakulima kuwapa taaluma ya uzalishaji bora wa mazao bila kutumia dawa zenye sumu.
Maafisa kilimo mikono yao ipo tied . Mbegu za mazao zinauzwa kutokana na umaarufu wake wa kutoa mavuno na sio ubora.
Unaanzaje kumshauri mkulima alime mbegu safe 'x ' huku akijua genetic mbegu 'y' itampa mavuno mengi?
 
t blj

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
2,800
2,000
Well... na hapa ndipo tatizo linanzia. Wakulima wanauziwa mbegu, mbolea, dawa zenye sumu pasipo kuelekezwa vya kitosha namna gani waweze kuvitumia kwa ulinzi wa afya ya mlaji.

Bado shida kubwa ipo kwa wataalam wa Kilimo hawatekelezi majukumu yao ya kwenda shambani.
Mkuu nakushauri angalia documentary ya "Food inc" huu mchezo ni complex sana kumlaumu tu afisa kilimo haitoshi maana yeye ni mtu mdogo sana na yupo kubeba lawama
Watu wangefanya kazi zao vizuri kuna baadhi ya items zingekuwa zinaishia pale bandarini ,
 
G-Mdadisi

Member
Feb 15, 2018
43
95
Maafisa kilimo mikono yao ipo tied . Mbegu za mazao zinauzwa kutokana na umaarufu wake wa kutoa mavuno na sio ubora.
Unaanzaje kumshauri mkulima alime mbegu safe 'x ' huku akijua genetic mbegu 'y' itampa mavuno mengi?
Kabisaa, wakulima kutokana na ufinyu wa taaluma ya kilimo wanajali zaidi wingi wa mazao na wala sio ubora wa mazao ndio maana mkulima yupo tayari kumwaga dawa shambani ili tu azuie wadudu waharibifu bila kujali je dawa hizo zinatakwenda kumuathiri vipi mlaji hasa mkulima mwenyewe ambaye kimsingi ndiye mlaji wa mwanzo
 
G-Mdadisi

Member
Feb 15, 2018
43
95
Mkuu nakushauri angalia documentary ya "Food inc" huu mchezo ni complex sana kumlaumu tu afisa kilimo haitoshi maana yeye ni mtu mdogo sana na yupo kubeba lawama
Watu wangefanya kazi zao vizuri kuna baadhi ya items zingekuwa zinaishia pale bandarini ,
Sahihi kabisa. Mfano items zinazotokana na Genetic Modified Organisms (GMO) ni moja ya items zinazozidi kuteketeza watu zaidi eidha kwa kujua au kutokujua. Licha ya kwamba items za aina hiyo haziruhusiwi lakini ukosaji wa uwajibikaji hupelekea kushindwa kuratibu vizuri
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom