Watu waliowaponda vijana wetu waliopo China ndiyo wamekuwa wa kwanza kulia kwenye mitandao

Tajiri Mapesa

JF-Expert Member
Feb 26, 2020
707
695
Huu uzi ni maalumu kwa watu wanao laumu viongozi ili hali na wao pia ni wa binafsi.

Watu wengi walijitokeza facebook, Instagram na watsap kuwakebehi na kuwaponda vijana wa watu na hata wazazi wa vijana hao. Yalitolewa maneno ya dhihaka. Lakini pia hata msaada wowote haukutolewa.

Na wengi walionekana kuishinikiza serikali isifanye chochote kwa vijana wale. Sasa hao hao tena na wao wakataka serikali iwafungie iwagawie na chakula. Sasa ndio tujaribu kuwaza wale wa China walipo fungiwa China walikuwa wanakula mawe sio. Je walipewa huo msaada ambao nawewe leo unauhitaji huku ukiilaumu serikali?

Wale vijana wa China walipo kuwa wanaomba msaada warudishwe Tz nyie ndio mlikua kimbelembele kuwakemea na kuwa kebehi leo ndio wa kwanza kulia kulia. Kama mliwaacha wale vijana wakomae na hali yao bila msaada wowote na wewe komaa na hali yako acha kulaumi viongozi.

Acha kulaumu viongozi komaa na hali yako, piga kazi, chukua tahadhari. Maana hata wewe huo msaada unao utaka huwezi kuutoa na hiyo imedhirishwa tangia mwanzo kabisa kwa wale vijana wetu wa china. Maana ulifurahia sana wabakie kulekule bila msaada.

Ukiuamua kuweka lockdown unaweka tu ni maamuzi yako hata leo unaweza kuanza. Ila sisi acha tupige kazi tujitafutie ridhiki.
 
Kwaiyo umeumia kias icho kuusina na Kesho ya baadh ya watu after 2025 umeamua kufungua na uzi? 😅😅😅😅😅
 
Back
Top Bottom