Watu waliokufa kipindi ambacho hata dini ya ukristo na uislam hazijaanzishwa wako wapi kama tunajiaminisha kwa kusema dini humfanya mtu kuona pepo?

Kabla ya ustaarabu na ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano haijakuwa, hapa namaanisha kusoma na kuandika pamoja na usafiri wa nchi kavu na majini, Mungu aliweka wateule wake kwenye kila jamii ya mwanadamu ili wawaongoze binadamu hao kulingana na vile Mungu anaona inafaa.
Ndio maana kila jamii ina kitu inachoamini ni Mungu. Mungu hajawahi kumuhukumu mtu kulingana na dini isipokuwa yale aliyomuagiza binadamu ayafanye.
Agreed Sir.
 
Hakika Mkuu Mm Naamini Kabisa Katika Mungu Ila Sio Katika Dini,kitakachokufanya Uone Pepo Kipo Katika Mfano wa Mizania Jitahidi sana Katika Mizania Yako Mambo Mema Yayazidi Mambo Mabaya.
kwa hiyo kumbe ni matendo mema yamfanyayo mtu kwenda mbinguni na si dini...sasa kwa nini watu warumbane kisa dini?
 
Kaka, ndugu yangu katika imani hapa tuchukue nafasi hii tueleweshane na watu wengine wapate fursa ya kujifunza kutoka kwetu, wajifunze yake mambo yanayokubaliana na akili, kwani Allah ndani ya Qur'an anauliza; afalaa taaqiluun, je hamtumii akili??, na zipo aya kadhaa ndani ya Qur'an zinatutaka tutumie akili katika kutafakari mambo.

Kaka, Sasa nije kwenye hoja zako;

(1) Unasema inawezekana tuzaliwe pamoja (baba na mama wamoja) halafu DNA ziwe tofauti?!!------ kaka, nakuomba anza kujifunza juu ya somo la DNA, DNA hivi sasa ndiyo nyenzo muhimu ya inayotumika kutambuana udugu wa watu nayo ni "the most reliable means todate in that case", kaka unajua tumepata msiba jana tu huku Morogoro, watu zaidi ya 60 wameteketea kwa moto wa petroli miili yao huwezi kuitambua kwa kuiangalia kwa macho njia pekee itakayotumika ni DNA, wazazi au ndugu wa karibu wa marehemu ndio watahusika kuchukuliwa sampuli kwa ajlii ya upimajii. (Inna lillahi wa inna ilaihi rajiuun, Mungu awasamehe makosa yao na awapumzishe kwa amani marehemu wote.)

(2) Kaka, Unasema "kesi ya kuzaa ndugu kwa ndugu, inategemea kwani wapo walioteleza mtu na kaka ake walizaa na watoto wamekuwa"----- mimi sizungumzii juu ya KUKUA ninazungumzia juu ya nafasi kubwa ya madhara yanayoweza kujitokeza endapo mtoto atajaaliwa kuishi kwa sababu watoto wa aina hiyo hufa au mimba hutoka kabla hawajazaliwa kutokana na mfanano "Genes" za wazazi, hivyo mimi ninazungumzia juu ya the high possibilities of inherent chances of a borne child to have lots of abnomalities in his/her entire life, na ndiyo maana Allah amekataza ndoa za aina hiyo kwasababu zinaharibu uzao na taifa zima linaweza kuangamia kama hali hiyo itatamalaki.
(3) kaka, unatoa yale madai yaliyozoeleka katika jamii kwamba Hawa alitokea ubavuni mwa Adamu??! Kaka haya madai sio madai ya kidhahiri ni madai ya kimethali tu, inaposemwa kwamba Hawa alitoka ubavuni mwa Adamu maana yake Hawa alikuwa na tabia, hulka na sifa zilizoendana na Adam kiasi kwamba akawa anafaa kuwa mke wake hii ndiyo maana ya kusema ametokea ubavuni kwake, kaka, na hata siku hizi utasikia watu wakiwaita wake zao; "wa ubavu wangu" ----- je hapo ina maana kuwa huyo mke katoka ubavuni kwake kidhahiri??, kaka, si kila neno la Mungu linaweza kuchukuliwa kidhahiri ama sivyo maneno ya Mungu yatakuwa hayafai kutuongoza bali kutupoteza, (Mungu apishe mbali). Hadithi ya Hawa kutoka ubavuni ni hadithi kutoka katika Biblia na waislamu wameibeba blindly bila tafakuri.

For the sake of arguments, tuseme Hawa alitokea ubavuni mwa Adamu kidhahiri, Wewe uliona wapi mwanaume anazaa kwa njia hiyo ya ubavuni??, nani alimpa hiyo mimba hadi akajifungua?? (tunajua Bi mariam alipata mimba kwa uwezo wa Mungu kupitia malaika)., je huoni kwamba Adam kwa kumuoa Hawa atakuwa alioa bintiye??!, genetic makeup za Hawa zilikuaje??, sababu kama Hawa alitoka ubavuni mwa Adam ni lazima Genetic makeup iwe ni EXACTLY the same na zile za mama-baba-mume wake Adam. Hii ni mumble jumble fantasy.

(4) Unazungumzia juu ya mufasirina kwamba wanatueleza kuwa pindi majini walipofukuzwa duniani hakukuwa na ukhalifa wa kuingoza neema za dunia;, kaka, ni mufassirina gani huyo muongo kiasi hicho??!, wapi imeandikwa ndani ya Qur'an kwamba majini walifukuzwa duniani??, kinyume chake Qur'an inasema; "Wa maa khalaqtunaa jinn wal inns illa lia'buduun", yaani hatukuumba majini na watu isipokuwa watuabudu.------ Majini wapo na watu wapo na Ibada inaendelea kama kawaida.

Shida hapo ni tafsiri ipi kuhusiana na majini, kuna majini Bakteria walioumbwa mwanzoni kabisa kwa moto na kuna Majini waliotajwa katika surah Jinn hawa walikuwa ni watu wageni (waisraeli kutoka Nasbin), kuna majini watu waheshimiwa katika jamii, kifupi ni kwamba Neno jinn, lina maana pana sana na maana yake mtu unaweza kuitambua kutokana na muktadha (context ) ya khabari yenyewe, lakini ni msingi wa maana ya neno "jinn" (kitu kisichoonekana kwa macho ya kawaida au kufikika kirahisi) ndiyo imebeba tafsiri zote hizo zingine.

Hata viongozi wakubwa na matajiri wakubwa ambao kuwafikia au kufungamana nao sio rahisi kwa tamathali ya lugha ya kiarabu wanaitwa "majinn".

Si kweli kaka, kwamba Adamu ndiye mtu wa kwanza kuumbwa na ndiye aliyetuzaa sisi sote,, kwani Allah ameisha sema; Ametuotesha katika ardhi kama mimea, na ndiyo maana kiasili tupo tofauti katika maumbile, tabia, nk, mfano chukua wa Khoisan kule Kalahari desert na Wa aborigines kule Australia au Wahadzabe au Red indians kule Canada na USA au Watwa kule central Africa (Burundi, Rwanda) au Congo pygmies (mbilikimo) au Mabedui (Bedouins) kule jangwani au Sentinels kule India nk, hawa ni wenyeji wa asili katika maeneo yao (untouched areas in earth), Genes zao ni za pekee kabisa hazija changanyika na genes za watu wengine, na hii inaonyesha ni watu wa hapohapo na haiwezekani kwamba walitokana na huyo Adam, na wakati huo dunia ilikuwa GIZANI katika teknolojia ya usafiri iliwezekana vipi watu kwa muda mfupi within 6000 yrs to spread so rapidly on earth??, kuna makabila yanayoishi juu ya milima ya Himalaya, wao maisha yao ni huko huko wala hawajashuka chini na wala hawajui kama kuna dunia nyingine mbali na hayo mazingira yao, sasa utasemaje na wao ni uzao wa huyu Adam??, maneno ya Allah ni kweli kwamba "katuotesha ardhini kama mimea"---- na kipindi hicho ni kipindi cha "Biotic soup" ndipo tulipooteshwa.

Kaka, Adamu hawezi kuwa mtu wa kwanza kuumbwa aslani, Yeye anabaki kuwa mtu wa kwanza kupokea utume/unabii kwa ajili ya umma wake, ndiye nabii wa kwanza kutumwa katika cycle yetu hii ya maisha yetu sisi Homosapiens.
Kaka hv umeisoma vema genetics???
DNA 100% ZIFANANIZO NI ZA PARENT AND OFFSPRING ILA OFFSPRING KWA OFFSPRING KUNA POSSIBILITY KUBWA SANA YA DNA ZAO KUTOFAUTIANA LICHA YA KUWA NA BABA NA MAMA MMOJA.
NGOJEA LEO SIKUKUU YA IDD WACHA NIRUKE VIWANJA MUJTAMAAN THEN TUTAELEWESHANA VEMA.
 
DNA hupimwa kujua mahusiano ya;

(1) Mtu na mama yake
(2) Mtu na baba yake
(3) Mtu na nduguye
(4) Mahusiano ya damu kati ya ndugu na ndugu waliozaliwa pamoja au ndugu wanaochangia wazazi nk,

Unapopima DNA unaangalia mahusiano ya damu, yaani kama kuna mahusiano yoyote ya damu basi DNA itaonyesha mahusiano yenu, Hivyo unaposema kwamba kuna uwezekano wa ndugu waliozaliwa baba na mama mmoja wasiwe na mahusiano ya DNA, huo ni uongo mkubwa wa mwaka, haijapata kutokea na hatotokea.

DNA inaitwa heteditary material, yaani ni material mtu anayorithi kutoka kwa wazazi wake, sasa haiwezekani watoto kutoka kwa mama na baba mmoja kila mmoja awe na "heriditary materials" tofauti.
 
Utapata tabu sana kwasababu ya kuamini zaidi sayansi ya mzungu kuliko maandiko ya mwenyezi mungu

Sayansi sio mali ya mzungu, sayansi ni elimu kutoka kwa Mungu na elimu hiyo haipingani na maneno yake.------ tofautisha kati ya sayansi ya uongo na sayansi ya kweli.

Sayansi inasema kuna nguvu za uvutano je hapo inasema uongo.??
 
Hivi kufia dini ni wendawazimu wa aina gani ? Unafia dini iliyotengenezwa na binadamu? Kuna watu wenye IQ kubwa waliofia dini ?
 
Hivi kufia dini ni wendawazimu wa aina gani ? Unafia dini iliyotengenezwa na binadamu? Kuna watu wenye IQ kubwa waliofia dini ?
Hiv ww na Dr.Zakir Naik nan ana IQ kubwa??
Wewe na wahajemi nan ana IQ kubwa??
Unajua kuropoka kalini hongera
 
DNA hupimwa kujua mahusiano ya;

(1) Mtu na mama yake
(2) Mtu na baba yake
(3) Mtu na nduguye
(4) Mahusiano ya damu kati ya ndugu na ndugu waliozaliwa pamoja au ndugu wanaochangia wazazi nk,

Unapopima DNA unaangalia mahusiano ya damu, yaani kama kuna mahusiano yoyote ya damu basi DNA itaonyesha mahusiano yenu, Hivyo unaposema kwamba kuna uwezekano wa ndugu waliozaliwa baba na mama mmoja wasiwe na mahusiano ya DNA, huo ni uongo mkubwa wa mwaka, haijapata kutokea na hatotokea.

DNA inaitwa heteditary material, yaani ni material mtu anayorithi kutoka kwa wazazi wake, sasa haiwezekani watoto kutoka kwa mama na baba mmoja kila mmoja awe na "heriditary materials" tofauti.
Huijui Genetics kasome vema genetics.
Ndugu na ndugu DNA zao ni ngumu sana ku match hata wa tumbo moja.
Ndio maana huwa inapimwa sana DNA ya mtoto na mzazi.
Kasome vema Genetics ukishindwa Nambie.
Usikariri nenda kasome mkuu.

Hayo ya Adam tutaendelea kukinzana mpk kesho maana Dini yenyewe inatuambia wanawake wametoka ubavuni kwa mwanamume kuanzia Hawa kwa Adam n.k.
Majini walikua wa kwanza kuitawala neema ya dunia wakafukuzwa ndio kisa cha kuja mtu kuanzia Adam mpk mimi na ww yote yameelezewa ktk dini hii hii na nukuu za ulamaau wakubwa tuuu.
Na nimekupa mifano mpk nashindwa kuirudia maana narudia nilichokieleza.
KHALIFA NI TOFAUTI NA RUSUL NA NABII.
KHALIFA MAANAKE KIONGOZI AU MTAWALA.
RUSUL NI MJUMBE AMA MTUME.
NABII NI MUONYAJI.
SASA BRO UTASEMAJE KHALIFA INASIMAMA KAMA MTUME AU NABII???!!!!
KAMA INGEKUWA NI KUPELEKA MTUME ALLAH ANGEMTEUA KULE KULE DUNIANI KWA HAO WATU UNAOWASEMA WALIKUWEPO KABLA YA ADAM KAMA ALIVYOTEULIWA MUSSA.
KWANN AUMBWE MTU MWINGINE ??
YANI BRO TUNACHEZEANA AKILI,ALLAH DUNIANI AUMBE WATU THEN SAMPULI YAO IPO DUNIANI AMTUME TENA MALAIKA AKACHUKUE UDONGO KUMUUMBA ADAM??
SI ANGEMWACHA AZALIWE NA WALE ALIOWAUMBA KABLA ????
THINK BRO
 
Huijui Genetics kasome vema genetics.
Ndugu na ndugu DNA zao ni ngumu sana ku match hata wa tumbo moja.
Ndio maana huwa inapimwa sana DNA ya mtoto na mzazi.
Kasome vema Genetics ukishindwa Nambie.
Usikariri nenda kasome mkuu.

Mkuu, inakupasa utafakari sana kabla hujaandika jambo, maelezo yako yanajipinga hata kabla sijajibu,

Hebu tukague huu mfano wako mwenyewe; Mama A, amezaa watoto B na C.

(1) Mtoto B anazo DNA zinazofanana na DNA za mama A.
(2) Mtoto C anazo DNA zinazofanana na DNA za mama A,

Kwahiyo Watoto B na C wote wanazo DNA zinazofanana na huyo mama yao, sasa utasemaje kwamba hao watoto B na C, DNA zao zisifanane ilhali wote wamerithi hizo DNA kutoka kwa huyo mama mmoja wanayechangia ??!, Kipimo cha DNA kinapimwa hata kwa ndugu wa damu wa mbali, mfano hata mama mdogo wa watoto B na C, DNA inamtambua kwamba anahusiana nao.

Kaka wewe ndiyo unatakiwa uende ukasome , genome DNA na Y DNA.

DNA ni heriditary material, Deoxyribose nucleic acid, zilizomo kwenye Genes (jinn), maana nyingine ya neno jinn (جن), ambalo lugha ya kiingereza imeliazima kutoka katika kiarabu.
 
Genealogical DNA tests often provide a profile that shows a person’s ethnic background. Many users are surprised to learn that their results can be slightly different from that of their siblings.
While this might seem strange or even impossible, it’s actually pretty common. It’s a consequence of the complex relationship between genetics, ancestry, and ethnicity.
How can siblings have different ethnicities when they have the same parents?
So the question becomes, do siblings have the same DNA or can they have different DNA?
The short answer is, yes. Siblings can and do have different DNA. Siblings share roughly 50% of their DNA with each other, but it depends on how their chromosomes randomly assorted. You should expect to share around 2,550 centimorgans (cm) with a full sibling (in consumer DNA test reporting). The shared centimorgans can range from 2,209-3,384 .
This article will dive into the science of how DNA is passed down from parents to children. But first, let’s consider a real-world scenario that illustrates how two siblings can end up with different ethnicity estimates from their DNA test results.

Nimekudokeza maana una smartfone lakini hutafuti vitu bro.
Mengine tafuta mwenyewe.
 
Kaka, ninayomashaka makubwa sana kwamba hujui lugha ya kiingereza, kama ungalijua kiingereza vizuri wala usingalileta hiyo post ambayo inaniunga mkono mimi na inakuponda wewe mwenyewe.

Rudia kusoma kile ninachoandika na rudia kusoma tena hiyo post yako ya kiingereza kwa umakini.🤣🤣🤣
 
Kaka, ninayomashaka makubwa sana kwamba hujui lugha ya kiingereza, kama ungalijua kiingereza vizuri wala usingalileta hiyo post ambayo inaniunga mkono mimi na inakuponda wewe mwenyewe.

Rudia kusoma kile ninachoandika na rudia kusoma tena hiyo post yako ya kiingereza kwa umakini.
Siblings can and do have different DNA.
BRO HIKO KIPANDE KIMETOKA KTK HIYO ARTICLE.
NILIKUA NIKIKWAMBIA SIBLINGS AMA NDUGU WANAWEZA KUTOFAUTIANA DNA UKAWA UNABISHA.
HII ARTICLE INAKWAMBIA SIBLINGS CAN AND DO HAVE DIFFERENT DNA.
BRO UNAKWAMA WAPIII???!!!!
KAKA NINA MASHAKA NA UELEWA WAKO.
 
Kumbuka ulinitolea mfano ukisema mtoto B NA C WAMEZALIWA NA MAMA A.
MTOTO B ANA DNA ZINAFANANA NA MAMA A.
MTOTO C ANA DNA ZINAFANANA NA MAMA A.
KIVIPI NISEME C NA B DNA ZAO HAZIFANANI??
KUMBUKA ULIZIPA MFANO HUU NA KUNIULIZA SWALI HIYO.
NIMEKUPA ARTICLE INAYOSEMA KUWA SIBLINGS (NDUGU ) CAN HAVE DIFFERENT DNA.
ASA BRO MM NA WW NAN HAELEWI KIINGEREZA ????
BRO UMEIMALIZAJE WEEKEND??
USIWE NA STRESS ZA KAZINI KAKA KESHO SIKUKUU.
 
Siblings can and do have different DNA.
BRO HIKO KIPANDE KIMETOKA KTK HIYO ARTICLE.
NILIKUA NIKIKWAMBIA SIBLINGS AMA NDUGU WANAWEZA KUTOFAUTIANA DNA UKAWA UNABISHA.
HII ARTICLE INAKWAMBIA SIBLINGS CAN AND DO HAVE DIFFERENT DNA.
BRO UNAKWAMA WAPIII???!!!!
KAKA NINA MASHAKA NA UELEWA WAKO.

Hiyo ni katika Ethinicity kaka siyo katika fratenity------ sisi tunazungumzia juu ya FRATENITY DNA.

Ni hivi mimi na wewe tunaweza kuwa sawa katika DNA za Ethinicity lakini hatuwezi aslani kuwa sawa katika DNA za fratenity,, tunakuwa sawa katika ethicity kwa sababu ya eneo tunalotoka East Africa, ethicity ni kabila au jamii kubwa ya makabila wanakuwa na DNA zilizokuwa common kwa wao wote.

Ndiyo maana nilikuambia Adam hawezi kuwa ndiye aliyetuzaa watu wote duniani kwa sababu DNA za Ethinicity zetu hapa duniani ni tofauti sana kuweza kusema kwamba dunia nzima ni "one Ethnic" na hivyo tunatokana na one source.

Angalia DNA za fraternity , DNA zinazotambua udugu katika hiyo post yako wameandika ni 50% , kwa watu ambao sio ndugu katika fraternity DNA utapata 0%, lakini hapo hapo katika Ethnicity unaweza kupata labda 5% au chini au zaidi.
 
Kuna baadhi ya watu huaminisha watu kuwa dini yao ni ya kweli na bila hiyo dini huwezi ona mbingu na ukiangalia dini na watu cha kwanza ni watu na dini zilikuja kwa baadae sasa je waliokufa kipindi dini hazijaletwa wamekwenda motoni au? tusaidiane kuwekana sawa hapa ila kwa mawazo yangu naamini kwa walio tenda mema wamekwenda peponi ila waovu ni motoni...vipi wewe unasemaje?
hata Adam na Hawa hadi kufikia kwa Ibrahim na Mussa - hawa wote hawakuwa Wakristo wala Waislamu lakini walimtumikia Mungu na kuna watakaiona pepo!
 
Hiyo ni katika Ethinicity kaka siyo katika fratenity------ sisi tunazungumzia juu ya FRATENITY DNA.

Ni hivi mimi na wewe tunaweza kuwa sawa katika DNA za Ethinicity lakini hatuwezi aslani kuwa sawa katika DNA za fratenity,, tunakuwa sawa katika ethicity kwa sababu ya eneo tunalotoka East Africa, ethicity ni kabila au jamii kubwa ya makabila wanakuwa na DNA zilizokuwa common kwa wao wote.

Ndiyo maana nilikuambia Adam hawezi kuwa ndiye aliyetuzaa watu wote duniani kwa sababu DNA za Ethinicity zetu hapa duniani ni tofauti sana kuweza kusema kwamba dunia nzima ni "one Ethnic" na hivyo tunatokana na one source.

Angalia DNA za fraternity , DNA zinazotambua udugu katika hiyo post yako wameandika ni 50% , kwa watu ambao sio ndugu katika fraternity DNA utapata 0%, lakini hapo hapo katika Ethnicity unaweza kupata labda 5% au chini au zaidi.
Duh bro umesoma article vizuri.????!
Please kaka irejee tena.
Isome vema article.
How can siblings have different ethnicity with the same parents .
Kisome vema hiko kipengele.

Kuhusu Adam na Hawa ni Qudra za Allah bro.
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom