Watu waliokufa kipindi ambacho hata dini ya ukristo na uislam hazijaanzishwa wako wapi kama tunajiaminisha kwa kusema dini humfanya mtu kuona pepo?

Kuna baadhi ya watu huaminisha watu kuwa dini yao ni ya kweli na bila hiyo dini huwezi ona mbingu na ukiangalia dini na watu cha kwanza ni watu na dini zilikuja kwa baadae sasa je waliokufa kipindi dini hazijaletwa wamekwenda motoni au? tusaidiane kuwekana sawa hapa ila kwa mawazo yangu naamini kwa walio tenda mema wamekwenda peponi ila waovu ni motoni...vipi wewe unasemaje?
Unaongelea dini zote au hizo mbili tu?
 
Jibu nilishajibu kitambo sana,hapa nafanya ufafanuzi tu,kwa mtindo ulio bora.

Tatizo sijajibu unavyotaka wewe. Soma kauli zangu utaelewa,usiwe na papara.
sasa umejibu nini kama swali wasema ni lauongo? Tatizo na wewe umekurupuka tu kujibu bado hujaelewa nilichokuuliza
 
Asee umedanganya kasome surat maryam uondoe ujinga
mjinga huelimishwa ila mpumbavu hawezi elimishwa sasa mimi nataka we ulete walau kahabari kutoka kwenye hiyo sura uliyotaja kupinga maelezo yangu nipate jua walahu
 
Mtu wa mwanzo kuumbwa alikuwa Adam kisha akaumbwa Hawa kutokana na Adam, baada ya kuumbwa walipewa muongozi wa kuishi na muumba wao, waliteleza katika kufuata maagizo hayo lakini waliomba msamaha na walisamehewa.
Maana ya neno Islam maana yake ni amani, kujisalimisha kwa Mola mlezi, watu wanafikiri dini ya uislamu ilianzishwa na Muhammad bin Abdullah (S.A.W.) hapana bali yeye ni mtume wa mwisho wa Allah, uislamu ulikuwepo toka uumbwaji wa dunia, tunaamini kila mtu aliyeamini kuwepo kwa Mungu mmoja asiyezaa wala kuzaliwa na hafanani na kitu chochote ni muislamu.
Mungu alikuwa akiteremsha wajumbe wake kutokana na utashi wake, ikiwa kuna watu ambao hawajafikiwa na ujumbe huo basi hao Mungu hawezi kuwahukumu, kwa kuwa alisema hawezi kuwaadhibu watu mpaka awapelekee mtume.
Mkubwa embu tupe uthibitisho basi kuwa uislamu ulikuwepo tangu kuumbwa kwa dunia..
 
Kabla ya ustaarabu na ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano haijakuwa, hapa namaanisha kusoma na kuandika pamoja na usafiri wa nchi kavu na majini, Mungu aliweka wateule wake kwenye kila jamii ya mwanadamu ili wawaongoze binadamu hao kulingana na vile Mungu anaona inafaa.
Ndio maana kila jamii ina kitu inachoamini ni Mungu. Mungu hajawahi kumuhukumu mtu kulingana na dini isipokuwa yale aliyomuagiza binadamu ayafanye.
Tukumbuke utambuzi wa matendo mema na yasiyo mema unapatikana katka BIBLIA NA Q''RAN TUKUFU na hivi vitabu ndyo chanzo cha misingi ya dini na imani ya allah/mungu.
Je hawa watu walijua vipi ili jema na ili si jema?ili la faa kutenda na ili halifai kutenda? Au hawakuwa wanayajua haya?
 
Sijui kuhusu Quran. Lakini Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vingi pamoja aidha vilivyoandikwa na mitume/manabii wenyewe au waliowashuhudia matendo yao. Hoja hapa sio lazima kupata mwongozo wa vitabu Bali maono/maongozi ya Mungu
 
Ongea point kidogo basi acha kudanganya. Au Quraan inakuambia udanganye? Mwislam wa kwanza alikuwa Muhamad tena according to Quraan yako. Na alieshushiwa hiyo alikuwa Muhamad. Usiongee uongo
Kama hivyo ndivyo ulivyofundishwa ni sawa
Mkubwa embu tupe uthibitisho basi kuwa uislamu ulikuwepo tangu kuumbwa kwa dunia..
Ngoja tusherehekee Eid Al Fitr, Allah akipenda nitarudi.
Eid Mubarak.
 
Dini ilianza kabla ya mwanadamu.

Nabii Aadam Alayh salaam alikuwa muislamu na wote waliofuata walikuwa waislamu.

Ama kuhusu ukristo ni dini za watu hasa warumi ndio dini yao wala hata mungu haijui

Back
Top Bottom