Watu walilia elimu imeshuka sasa mabadiliko yanafanyika vipi tena?...

Pangaea

JF-Expert Member
Jun 14, 2012
202
41
Nchi imegawanyika! Ukiliangalia tamko la hivi
karibuni la waziri wa elimu na ukiwasikiliza
baadhi ya wadau, utadhani kuwa waziri
katangaza uamuzi wa haraka unaominya haki ya
elimu kwa watu wa nchi hii.
Lakini kwa wengine huu ni uamuzi sahihi. Kwetu
sie ambao tunaujua mfumo wa elimu na matunda
ya elimu itolewayo kwa wananchi tunaweza
kukueleza kuwa uamuzi huo ni mzuri haswaa!
Sina desturi ya kuwafagilia viongozi lakini hapa
sina budi kukiri kuwa waziri kaamua sawasawa.
Binafsi, si kwamba nimesoma nao tu bali wapo
pia katika maeneo yetu ya kazi, sina shaka kuwa
kwa muda mrefu tulitakiwa kuchukua hatua hii.
Usimamizi wa Elimu umeachwa huria sana si kwa
vyuo vikuu tu bali hata vyuo vya ufundi maarufu
kama V-E-TA.
Kinachoangaliwa zaidi sio sifa bali chuo kitapata
mapato kiasi gani na ubora wa taaluma baadaye!
Kwa hivyo ukija watakutengenezea sifa kuanzia
cheti,diploma, mpaka shahada, utaratibu
usiompatia mlengwa maarifa yanayatarajiwa, hata wanafunzi wao wakati mwingine huhuzunika kwa kuwa
malengo yao ni kupata elimu iliyo bora lakini wanapofika vyuoni hukuta hali tofauti, hakika
utaratibu huu umeweka udhaifu katika taasisi
nyingi za umma na za binafsi.
Tunahitaji mfumo bora wa elimu ili taifa hili
lijipatie wataalam. Kwa mtazamo wangu utaratibu
wa "equivalent qualifications" siyo mbaya na
umekuwepo kwa muda mrefu tu ila ni lazima hizo
diploma na certificates vyuo visiwe na mamlaka
ya kutahini, mamlaka hiyo iachiwe NECTA. Hapo
tutadhibiti kupitishana kiholela!
Ingawa sijasikia kama waziri ametamka kuwa
hawa wasomi watanyang'anywa diploma ama
digrii zao, na kama huo ndio mkakati basi ni
dhahiri kuwa hatuwezi kuwatendea hivyo hawa
watanzania wenye shahada na stashahada kwa
kuwa hawajajitunuku wenyewe bali kuna mamlaka
iliyowatunuku kwa mujibu wa sheria hivyo
ninadhani ikiwa ni kweli hawakuwa na sifa za
kusomea shahada basi watunukiwe "Advanced
diploma" kwa wenye digrii na wenye stashahada
watunukiwe "Advanced certificate" na ajira zao
zilindwe, angalau tutakuwa hatujawatendea ukatili
wa kielimu.
Ni wakati sasa kuwa na sera ya elimu na wadau
wote washirikishwe ili kila mmoja aikubali na
kuwa tayari kuitetea, hii itaepusha mabadiliko kila
anapotokea waziri ama serikali kubadilika.
Mwisho maoni haya hayamlengi MTU ama taasisi
yoyote binafsi bali ni mtazamo wangu binafsi
kama mdau wa elimu.
 
Back
Top Bottom