Watu wako walilie msaada mpaka wakati gani?

SHADOWANGEL

JF-Expert Member
Sep 15, 2014
528
349
Biblia inaonyesha Tangazo ambalo Habakuki nabii aliona katika maono: kwa kusema Ee Yehova, nililie msaada mpaka wakati gani, nawe usisikie? Nitakuomba msaada kutokana na jeuri mpaka wakati gani, nawe usiokoe? Kwa nini unanionyesha jambo lenye kudhuru, nawe unaendelea kutazama taabu tupu? Na kwa nini kuna uporaji na jeuri mbele yangu, kwa nini kugombana hutokea, kwa nini mzozo huendelezwa? Ni jambo lililo wazi leo hii linapotokea jambo katika nchi yoyote duniani watu kulalamika kwa wakubwa wao ili kupata haki juu ya kitu au jambo ambalo linaonyesha kuumizwa wanaanchi?

Tunaona ata katika vitabu vya dini vinasema kwamba mhakikishe mambo yaliyo ya maana zaidi, ili muwe bila kasoro na msiwe mkiwakwaza wengine mpaka siku ya Kristo, Hakika vitabu vya dini vinaonyesha tuishi kwa amani bila kukwazana wenyewe kwa wenyewe kwa kusema Kila mmoja na aendelee kutafuta, si faida yake mwenyewe, bali ile ya yule mtu mwingine. Na Mtu mwingine ni nani? Mtu mwingine ni yule mwananchi unayemuongoza na pia ni yule jirani yako unayeishi naye. Je ivyi ndivyo ilivyo kwa viongozi wetu wanaposikia jambo au kuambiwa jambo na watu wanao waongoza?

Kuna mambo mengi ya kujifunza katika vitabu ikiwamo mungu kuwakatalia ata wale aliowapa uongozi wa kuongoza katika israel walipotaka kuwamwagia mafuta viongozi waliozani wao watafata badala yao, Mungu aliwapa muongozo tofauti na mawazo yao.

Katika imani tunajifunza wana wa israel walikaa utumwaki miaka mingi wakimlilia mungu kuwaokoa katika tabu na dhika zao kwa kuwapa kiongozi atakayewaongoza kwa kuwapeleka nchi ya ahadi, Ni wazi kabisa katika kila kundi la jamii furani lazima atokee kiongozi wa kuwaongoza hao watu katika haki ila kuna wakati mwingine kama binadamu tunaenda katika hali ya kibinadamu tunaposikia mambo tofauti kwa wale watu wa chini ambao viongozi hao walipewa na mungu si kwa bahati wala nguvu zao ila kwa wakati mungu alikusudia kwao..

Vitabu vya dini vinahaasa kwa viongozi hao kutenda haki katika watu ambao wanaowaongoza kwa kuwa ikumbukwe kuwa kiongozi wetu ni mmoja. Kwa kusema "Lakini ninyi, msiitwe Rabi, kwa maana mwalimu+ wenu ni mmoja, lakini ninyi nyote ni ndugu. 9 Zaidi ya hayo, msimwite mtu yeyote baba yenu duniani, kwa maana Baba+ yenu ni mmoja, Yule wa mbinguni. 10 Wala msiitwe ‘viongozi,’+ kwa maana Kiongozi wenu ni mmoja, Mungu."

Jambo la kujiuliza WATU WAKO WALILIE MSAADA MPAKA WAKATI GANI?
 
Jambo ambalo nimelishika kwako ni ili "Whoever loves money never has money enough; whoever loves wealth is never satisfied with his income. This too is meaningless"

:):):):):)o_Oo_Oo_O
 
Back
Top Bottom