Watu waadilifu hawahitajiki kwenye ofisi za umma?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
6,049
8,411
Baadhi wamedhihirisha kwa vitendo kuwa hawayajui majukumu yao. Inawezekana ndiyo wale walioingia ofisini kwa vimemo vya akina "unanijua mimi?" Dhuluma na uongo ni kama sehemu ya "job descriptions" za watumishi wengi wa umma.

Kama mpaka wasomi wanadhulumiwa haki zao huku wakiona, hali ikoje kwa wananchi ambao hawajabahatika kusoma?

Isingelikuwa na mimi nimepita chuoni, kwa yanayotendeka katika ofisi za uma, ningeweza kuamini kuwa moja ya mambo wanayofundishwa wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu ni uongo, utapeli na dhuluma.

Lakini najua hayo hayafundishwi vyuoni, labda vyuo vilivyopo ndani ya ofisi za uma ambavyo mtumishi hupitia baada ya kuajiriwa kwenye ofisi husika.

Ninahisi, ukiwa mwadilifu, ni vigumu kumudu kufanya kazi kwa amani kwenye ofisi za uma nchini. Inawezekana watumishi waadilifu ndiyo wanaoongoza kwa kuchukiwa na watumishi wenzao kazini.
 
Uko sahihi 80% ya watumishi wa umma, kama sio 90% ni wezi. Hii ni ofisi zote, yaani zote.
 
Kama kila mkuu wa Mkoa angefanya kama Makonda, na kila Waziri angefanya kama Jerry Slaa, na kila Jaji/Hakimu angesimamia taaluma yake kikamilifu, hii nchi ingebadilika haraka sana.
Hakika,nchi hii kama ni maskini na ukapata tatizo ndio utajua umhimu wa viongozi kama makonda.Kuna mwaka wakati najitafuta niliwahi dhulumiwa 2ml na kila mnakoenda mwenye pesa anapendelewa.
 
Ndicho alichopigania JPM, ni tatizo hasa ulimwengu wa tatu, mtu akijitokeza kuweka mambo sawa wanaondoka nae mbio mbio.
 
Hakika,nchi hii kama ni maskini na ukapata tatizo ndio utajua umhimu wa viongozi kama makonda.Kuna mwaka wakati najitafuta niliwahi dhulumiwa 2ml na kila mnakoenda mwenye pesa anapendelewa.
Mkuu kuna Viongozi wengine wako kama bidhaa,huna pesa hawana habari na wwe,wao wanaangalia nani mwenye pesa tu, ndiyo wanamuhudumia,tena anavyotaka yeye muhudumiwa ndiyo anatoa maelekezo! Mungu azidi kutuletea Viongozi wazalendo kama kina Makonda na Silaa ili wazidi kuokoa wanyonge!!
 
Back
Top Bottom