Watu wa Simba SC na nyie mmekuwa kama Washamba wa Yanga SC kulalamikia Takwimu za Bodi ya Ligi?

Mightier

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
5,755
2,000
Hivi Yanga SC ikiongoza kwa Takwimu, Kujaza Watu au Kuuza Mijezi Misukule na Mikaragosi yao huku wakiwa hawachukui Vikombe na tunawafunga katika Mashindano muhimu nani mnadhani Kimantiki ndiyo anaonyesha kuwa na Tija hasa?

Yaani wana Simba SC leo hii mmesahau kuwa Yanga SC ni Washamba? Hivi kama Mtu leo hii pamoja na Kuusotea Ubingwa wa VPL kwa miaka Minne amesikia Takwimu ikiwataja Vinara halafu wanashangilia hao siyo Washamba?

Hivi kama Yanga SC ambao wameyasahau Matokeo yao ya Kufungwa nje ndani na Rivers United FC katika CAF CL na wakashangilia Kufungwa kwa Simba SC na TP Mazembe katika Mchezo wa Kirafiki wa Simba Day hao siyo Washamba?

Yaani wana Simba SC leo hii mmesahau kuwa kuna Tafiti ilifanywa na ikaja na Matokeo kuwa Mashabiki wa Simba SC ndiyo Wasomi, Werevu na wana Maendeleo makubwa hata Kimaisha na wa Yanga SC ni Washamba, Waswahili na wamezoea tu Wivu, Majungu na Fitna?

Binafsi kama Mightier nawafananisha Yanga SC na Mwanafunzi ambaye ni Msafi, ana Nidhamu, anasoma sana, si Mtoro na Darasani anakaa mbele kabisa na Kuuliza mno Maswali lakini katika Mtihani Yeye ( Mwanafunzi Yanga SC ) ndiyo huwa anafeli huku wale Watukutu wanafaulu na Kusonga mbele.

Tuwaacheni Yanga SC na Ushamba wao.
 

Mightier

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
5,755
2,000
Mimi hata sikuhangaika na hizo takwimu, cha muhimu makombe tunabeba likiwemo la jumamosi hii baaasi
Furaha ya Wanasimba wote inatakiwa iwe hapa katika Kubeba Vikombe na siyo Kushangilia Takwimu ambazo Logically sioni kama zina haja ya Kuumia nazo kivile.
 

Mightier

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
5,755
2,000
Hawa dao yao jumamosi tuwapige 2 au 3, waanze kushikana uchawi
Iwe ndani ya dakika 90 au 120 au Mikwaju ya Penati Jumamosi Yanga SC anakufa ( anafungwa ) na Simba Sports Club Mkapa Stadium.

Tunza / Tunzeni hiii Post yangu tafadhali kwani najiamini na hakuna Timu nyepesi na isiyonipa shida Kuiwazia jinsi ya Kuwafunga kama Yanga SC.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom