Watu wa namna hii hawana tija kwenye nchi yetu

Nkobe

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
2,161
3,157
Watu wanaofikiria kupata pesa kwa kufikiria kufungua duka hawana tija katika nchi/tija yao ni hafifu.

Nasema hawana tija kwa sababu wao si wazalishaji, (wanachukua ready made), wao ufikiria kufungua duka na kujaza bidhaa kama simu, computer nk. Kimsingi ni mawakala wa nchi za nje kwa kuchukua vitu kutoka China nk. Pia hawa ni mawakala wa kulipa kodi kwa serikali, kodi kidogo. Watu wa aina hii hawaleti fedha za kigeni nchini maana wao hawana cha kuuza nje. Hiyo nayo ni moja ya sababu ya nchi kuwa masikini. Watu wa aina hii hata shughuli zao hazikui kwa haraka maana ni creativity ndogo sana inatumika.

NB: Watu wa aina hii wanahitajika kwa kiwango kidogo, lakini wakizidi wanalitia taifa umasikini maana hawazalishi

Watu wenye tija ni awa.

Watu wenye tija ni wale wanaofikiria kuzalisha vitu vyao, haijarishi ni kitu gani. Mfano mtu anaefikiria kufuga Ng'ombe, kuku nk ana tija kwa nchi. Mtu anaefikiria kulima pia anatija kwa nchi. Iko mifano mingi hapa. Nasema wana tija kwa sababu wanazalisha kitu kipya ambacho mwanzo hakikuwepo. Watu wa aina hii wakiwa wengi chini utanua wigo wa ajira, pia wana export bidhaa zao nje ya nchi na kuleta pesa za kigeni. Watu wenye tabia hii wanatakiwa kuwezeshwa, mfano upande wa kilimo wanaweza kuuza nchi zenye ukame sehemu kubwa kama Kenya, Sudan, Ethiopia, Uarabuni nk

Nimehamua kuandika hii mada baada ya kuona vijana wengi wanafikiria maduka, wanafikiria kwenda China kufuata bidhaa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom