Watu wa Mza, Mara, Shy, Geita, Kagera na Simiyu mpo tayari? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watu wa Mza, Mara, Shy, Geita, Kagera na Simiyu mpo tayari?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by EasyFit, May 17, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kuna siku tuliahidi kuanzisha blog kwa ajili ya kubadilishana habari kwa watu wa mkoa mpya wa SIMIYU. Blog Ilichelewa kutokana na maombi ya watu mbali mbali ya kuongeza wigo wa eneo. Maombi yao yamezingatiwa na sasa itarusha habari za eneo lote la kanda ya ziwa, yaani mikoa ya MWANZA, MARA, SHINYANGA, KAGERA na mikoa mipya ya SIMIYU na GEITA.

  Badala ya kuitwa Simiyu Jamii blog sasa itaitwa Lake Jamii Blog, Mungu akipenda kesho itakuwa hewani, website yake itawekwa hapa hapa, karibuni sana.

  Kesho website yake itawekwa kwenye hii hii thread, kama una maoni zaidi kabla unaweza kutushauri.

  Natanguliza shukrani.

  ============================== ============================== =
  UPDATES TODAY 8/6/2012
  ============================== ============================== =

  Kama tulivyoahidi tuko kwenye majaribio ya Safari Forums tembelea Safari Forums utoe maoni yako.


   
 2. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Mbarikiwe sana kama kweli mtafanikisha hayo.
   
 3. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Asante mkuu unakaribishwa sana, lengo letu ni kuhabarishana kutoka engo zote za Lake victoria, toka Ngara Rosumo maeneo ya Rulenge hadi Ukerewe kisiwani na Ukara bila kusahau Tarime kwa wanaume wa shoka.
   
 4. Sunday Ngakama

  Sunday Ngakama Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pongezi kwa wazo zuri, nadhani soon wana mwanza tutakuwa na social media yetu. tatizo nililoliona mimi ni hapo kwenye jina. halina mvuto kabisa( Lake Jamii Blog ), najua aliye suggest hilo jina alitaka lionekane cool kwa kuweka umombo, ila kusema kweli ni ushamba wa hali ya juu kuchanganya lugha na hii nimeiona sehemu nyingi tu, vitu hivi mbona Lugha yetu ya kiswahili inajitosheleza kila Idara!! mimi napendekeza badala ya hiyo Lake Jamii Blog, ungeiita mfano, Kanda ya Ziwa Blog ama Nyanza Blog. najua vitu hivi sio rahisi, ndio maana wakati mwingine inabidi ushirikishe watu.
   
 5. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Na mimi nimo nitaripoti tokea hapa Musoma!
   
 6. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu EasyFit kwanza nikupongeze kwa niaba ya watu wote mnaoshiriki kuanzisha blogu ya lake zone.

  Lakini pia naomba mtilie maanani suala la watu kujisajili, ni muhimu sana na faida zake ni nyingi. Sidhani kama itakuwa na uzito sana kama mnachukua maoni au malalamiko ya wadau na kuayapeleka kwa viongozi/ofisi husika huku yakitajwa kutoka kwa anonymous.
  Kujisajili pia itaongeza ufanisi kwa wachangiaji na itasaidia kudhibiti nidhamu kwakuwa watu tumetofautiana kimtazamo na uelewa kwahiyo tusitarajie kwamba hakutakuwa na watu watakao abuse fursa hiyo. Ili kuweka nidhamu pamoja na kutambua mchango wa kila mwanajamii ya kanda ya ziwa atakaye visit blogu yetu na kuweka mawazo yake ni muhimu tukajisajili, hata kama si lazima kutumia real name.

  Mimi hayo ndio mawazo yangu, nawatakia kila la kheri.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Lake Nyanza Blog?
  Lake Zone Blog?
  Lake Victoria Blog?
   
 8. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,015
  Likes Received: 2,663
  Trophy Points: 280
  Wazo zuri sana.
   
 9. Lenana

  Lenana JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 422
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Na sisi mashemeji zenu tutawahabarisha yanayotokea ukweeni pasipo kufukwa na swala la ukanda! With due respect mashemeji!
   
 10. M

  Masuke JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Tuko pamoja kaka, nitahakikisha nafungua hiyo blog ili tupeane uzoefu juu ya ukanda wetu wenye mali ya asili nyingi.
   
 11. sexologist

  sexologist JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 2,296
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 135
  Vp na 'jamii forums' ushwahi kuwashauri?
   
 12. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Asante Sunday Ngakama kwa wazo lako, tulikuwa na wazo kama lako, tulianza na Nyanza blog wajumbe wakasema itakuwa kama blog ya watu wa Mwanza pekee ingawa tunajua kwa historia ya Mwanza Lake = Nyanza, hata hilo la Kanda ya Ziwa lilijadiliwa likaonekana lina ujumbe wa kujitenga zaidi. Hata hivyo bado kuna nafasi ya kubadili (jina la site) maana liko ndani ya uwezo wetu kuliko kubadili jina la website. Asante ngoja tusubiri mawazo mengine kabla hatujaipeleka hewani.
   
 13. sexologist

  sexologist JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 2,296
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 135
  We na we ni disaster.. Sasa unashauri vizuri ila unashndwa kupendekeza.. We unasema watu wajisajili ili kuepuka matusi na pia wajulikane in case kuna mtu anazunguzwa na anataka atambue watu waliomzungumza ”kwa uzuri” halafu hapo hapo unasema hata watu wakitumia fake names ni poa, sa ndo nini.. Mbona ujumbe haujakaa poa.. Labda kama uniambie lengo ni kujua idadi ya wanachama kama jf! Zaidi ya hapo, nakupinga.. Bora tu iwe kama fb!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Asante Kiganyi tutakuhitaji zaidi kwa maeneo hayo najua, pande hiyo tuna wanasiasa nguli kama kina Mkono, Wassira, Makongoro, Vincent Nyerere na wengine.
   
 15. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mkuu Mwita Maranya, tumekusikia na tumekuzingatia ni wazo zuri, kila kitu kina uzuri na ubaya wake. Lengo letu ni kupata mawazo na wachangiaji wengi kadri iwezekanavyo tukianza moja kwa moja na kujisajili tutawakimbiza wengi. Tutaona michango itakavyokuwa tunaweza kuanza kwa mchangiaji kuandika jina na email yake kama yanavyofanya magazeti mengi bila kujisajili, then next step itakuwa kujisajili (LOG IN). Asante Mwita wa bande ya ile, mang'ana yakoje, nyie ni shemeji zangu dada zangu wameolewa huko.
   
 16. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Pamoja sana Mkuu yaani unapiga humo humo ngoja tusubiri michango mingine, tunajiuliza kwa nini hatukuanzisha thread kama hii mapema kupata mawazo kama haya, big up. Sunday Ngakama kasema tusipende majina ya lugha zilizoletwa na meli unashauri nini hapo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Asante Masuke siku zote huwa vizuri kuwa wa kwanza.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Karibu shemeji, usiwe na wasi wasi hapa hakuna suala la ukanda lengo ni kupata habari kutoka kwenye eneo husika. Kama ni criticism mtu anatoa angali anayajua maeneo husika na hata watu waliohusika. Mfano wakulima wa pamba wa Bariadi wagomea bei mpya kwenye ginneri ya Lugulu (Bariadi) au matokeo ya uchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji cha Kyamnyorwa Muleba ni haya. Utakaposikia habari kama hizi na ikisingatiwa unayajua maeneo husika au unauwezo wa kufika pale inapendeza na utajihisi kuguswa zaidi na hata mchango wako utakaotoa utakuwa wa hisia chanya.
   
 19. V

  Visionmark Senior Member

  #19
  May 18, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza kabisa napenda niwape pongezi za dhati kabisa toka ktk kirindi cha moyo wangu kwa wazo lenu hili zuri na ktk huu muda mwafaka. Na nimatumaini yangu kuwa wazo hili litasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza na kuendeleza kanda husika ktk nyanja zote za kimaendeleo, kiuchumi, na kiutamaduni pia na hata mimi ninakitu ambacho takianzisha ili kubusti maendeleo ya eneo husika hv karibuni. Binafsi naunga mkono ushauri wa Mwita Maranya khs jina la blog, mnaonaje kama ikiitwa Lake Victoria Blog?! Well done guys!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Sasa mbumbumbu mbona unataka kuharibu mjadala, mimi nilidhani wewe ni mbumbumbu mjanja!!:peace:

  Majina ni muhimu for the good purpose of moderation.:poa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...