Watu wa mikoani (Vijijini), badilikeni too much!

Habari za muda huu wana Jf.

Kuna katabia fulani wanacho baadhi ya watu waishio mikoani huwa inaudhi na kukera sana, mno yani. Tunafahamu, huko ndio chimbuko la uzao wa walio wengi umeanzia, tunaelewa umuhimu wenu, na tunapaswa kuwasaidia.
Aisee hii kwel kabisa toka nizamie mjini Sasa Kila nikiwaza kwenda kuwasalimu nikiwaza hili swala naahirisha😂
 
Aisee hii kwel kabisa toka nizamie mjini Sasa Kila nikiwaza kwenda kuwasalimu nikiwaza hili swala naahirisha
Halafu kuna watu wanawatete huku nilipanga kukaa wiki mbili kwa hali ninayoiyona siwez aiseee
 
Kuliko kuja kuandika hapa jukwaani ambako watu wa huko kijijini kwenu hawatakusikia ni kheri ungeenda kwa mwenyekiti akusanye wanakijiji wote uwaambie wenyewe, sisi huku hatuna msaada kwa hilo.
 
Huu ni uzi wa mwendelezo wa harakati za kuubomoa ujamaa mnakosa heri na baraka za wazee ndugu na jamaa wa kijijini kirahisi sana na mnaona ni vitu vya mjadala wa kuwashinikiza wengine waendelee kuubomoa ujamaa huo.

Nafurahi ninapofika kijijini ninavyokirimiwa na kila aina ya watu wanaonifahamu wengine hunipa mazao, mifugo (kuku) na kunionesha upendo wa hali ya juu Mimi ni nani hadi changu kidogo nilichonacho nisigawanenao ndugu zangu HAPANA TENA HHAPANA nawaoenda ndugu zangu wa kijijini mkiniona nimefika panapostahili kuniomba niombeni ninacho nitawapa kama sina zidini kuniombea kheri nipate. Nafahamu maisha ya kijijini.
 
Sina cha kukujibu ila ushauri wangu acha ushabiki zingatia maudhui
Ukifa hao ndo watakaokuja kukuchimbia kaburi, mambo mengine kama yanakera kutoka kwa ndugu zako wasitiri kwa kukaa kimya kuwatuhumu kwenye mitandao ya kijamii ni ushamba
 
Habari za muda huu wana Jf.

Kuna katabia fulani wanacho baadhi ya watu waishio mikoani huwa inaudhi na kukera sana, mno yani. Tunafahamu, huko ndio chimbuko la uzao wa walio wengi umeanzia, tunaelewa umuhimu wenu, na tunapaswa kuwasaidia.
Humu uliowaandikia wote wa mjini hakuna mtu wa aina ya unaowazungumzia. Awe JF halafu akusubiri wewe wa mjini umpatie 2000 au 1000? Hakuna. Umejisumbua. Rudi kijijini kwenu kawaambie uso kwa uso.

Hata hivyo mimi nikienda Bush kwetu Mwakaleli nahakikisha nina change za elfu mbilimbili za 40,000 au 50,000 ambazo ntawapa wasio ndugu wa karibu. Nikifika ni mwendo wa kusambaza upendo tu. Kuna furaha katika kutoa kuliko kupokea. Hayo ni maisha ya kawaida ya Mwafrika
 
Kuna mtu anaanza kazi mjini mshahara wa kwanza tu anataka kusafiri kwenda nyumbani😀😀😀😀
Mimi mwenyewe nina ndugu zangu wa hivyo.

Tena sometimes huwa hawana hela, wanapiga tu mizinga. Anakupigia tu simu dogo nisadie 20,000, akipiga mizinga hivyo watu 5 ana laki moja tayari. Anakimbilia kijijini kwenda kuuza sura.

Tena akifika huko anaanza kuwapondea, ooh madogo wamezamia tu town hawataki kurudi home, kumbe yeye mwenyewe hiyo nauli mmemsaidia nyie.
 
Kuna kitu kinahitwa "Black Tax". google utapata majibu. Hayo hatuwezi kuyakwepa kwa sasa labda kizazi kijacho.
Mzungu alioa binti wa kibantu na siku ya kwenda kijijini binti anashikwa huku na huko akiombwa pesa. Sasa baada ya kuishiwa akawa anamwomba Mzungu wa watu pesa. Yaani mzungu alishangaa sana. Afrika tuna shida nyingi wewe acha tu. Ukitoboa kuna msururu mrefu wa watu wanaokusubiri kuwasaidia.
 
Back
Top Bottom