Watu wa mamlaka ya sanaa pigeni marufuku Bongo Star Search

Wewe na akili yako unakaa unawasikiliza Wahindi? Bora nimsikilize Mwijaku kuliko kukusikiliza wewe msikiliza wahindi.

Wale wavuta bangi wa Arusha waambiwe tu kweli hawajui mziki wakatafute shughuli zingine za msingi za kufanya haina kuremba.

Mwisho sio jukumu la serikali kuzalisha wasanii hata huko nje sio jukumu la serikali hilo. Popote pale mwenye hela ya kuingia studio anaingia studio ndio maana leo hii unawasikia kina lil lil kibao wa US redioni ambao hata mizungu wenyewe hawaelewi wanasema nini.
 
Wapo waliosema hawana vipaji leo ndio wanatafuna pesa hao BSS wapo kukatisha ndoto za vijana kwa asilimia kubwa..
 
Mimi ni mfuatiliaji wa AGT na The Voice, wale jamaa huwa wastaarabu sana hata kama unafanya ujinga kwenye stage.
Ni mara chache unaweza kuta washiriki ni wakorofi hivyo majaji hureact lakini sio kwa matusi bali huitwa security.

Pia kingine mara nyingi ni watu wenye elimu ya music au uzoefu kwenye hiyo sector hivyo wanajua wanchokifanya na wanachokitafuta.
Unaweza kuta mtu ata sauti ya kuongea haitoki, au akiimba sauti inatetema kama tractor lakini badala ya majaji kuwa mean wanakuwa mentor na kuwaambia nini cha kufanya na wapi wanakosea.
wafanye mazoezi zaidi pia warudi tena mwaka mwingine kuja kujaribu tena.

Kwenye The Voice utakuta jaji anamuambia mshiriki jinsi gani ya kuimba au asimame vipi na ashikilie chombo vipi.

Wako so professional na serious na wanachokifanya.

Huku kwetu BSS ni kama comedy au kipindi cha kuaibisha, udharirishaji na kubeza watu wanaojaribu na kuwacheka (humiliation tv show)
Maana ya kuwa jaji yes ni kukosoa lakini sio kukosoa kwa kumuaibisha mtu na kumbeza au kumgeuza kituko.

Mfano jaji anaingia chini ya meza makusudi, anacheka mpaka kuinamia meza, kumwambia huna kipaji unajisumbua bure.
Au kama walivyomwambia harmonize kwamba hana kipaji na anaharibu wimbo wa malaika (fvkthem sasahivi harmonize ana pesa na kipaji kushinda wao wala huyo muimbaji wa malaika haoni ndani hata kwa microscope wala hajulikani alipo)

Kuimba sio kipaji tu bali ni mazoezi mengi ili kujua uwezo wako na udhafu wako na uzeofu wa kutosha wa kuweza kucontrol vocal cords zako.
badala ya kumwambia mshiriki nini cha kufanya, wapi anakosea ili ajirekebishe badala yake wanamfanya ajione sio chochote na akate tamaa.
Wako so unprofessional ni kuuza sura na uswahili mwingi na mambo mengine ya kijinga.

Solution ni watokee watu wengine walio serious na wanachokifanya.

Uko mbele ndo wana majungu hatari, Muangalie Simon Cowel wa america got talent. Anatoa za chembe! salama akasome.
 
Habari zenu wakuu,

Nimeamua Leo kuleta mada hii haswa mamlaka pigeni marufuku shindano la BSS kwa sababu hakuna anaestahili kuwa jaji pale na ndio maana pamoja na serikali yetu haina mpngo mbdala wa kuzalisha wasanii ila ndani ya nchi yetu kila mwenye pesa anaenda studio.

Hebu tuangalie nchi za wenzetu jinsi wanavyotafuta waimbaji hakuna jaji hata mmoja anaemwambia mshiriki una sauti mbaya ila hapa kwetu jaji anatamka wazi anakwambia huwezi kuimba sasa ukiangalia huyo jaji wenyewe hata chombo kimoja cha muziki hawezi piga

Tujaribu kuangalie wahindi wanapotafuta waimbaji wale majaji ni watu walioshiba.

Ni wasanii wakubwa hata ukiangalia nyimbo zao youtube utapata ushahidi kwa mfano jaji awe Himesh Reshmiya

Au Sonu Nigam
Au Udit Narayan
Au Kumar Sanu

Hapo ikitokea MTU ameshinda hawezi potea sasa hawa majaji wetu sasa Sijui wametokea kwenye kitengo gani kuhusu Sanaa au uimbji au kwakuwa maarufu hapa kwetu
Labda ndio mbinu yao ya kupunguza msongamano

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Gayo tangu lini amekuw mtaalamu wa muziki
Hebu acha kuchekesha walionuna
Kuna msemo unasema hivi...
👇🏾
"No research No right to speak"

Kwa sisi waswahili tunao wetu huu...
👇🏾
"Usilolijua ni sawa na usiku wa giza"
 
Kuna mda ss wabongo hatuko serious achen tu majaji wawe wakali unakuta mshiriki amekuja kwenye stages kuchekesha tu nakujulikana unakuta amevaa hovyo haimbi kitu cha maana zaid ya matus au lugha yake s nzur kuna mda walikuja huku arusha ilikuwa n vituko tu
 
AGT na The Voice ina majaji wastaarabu na wengine huwa mpaka wanalia kubembeleza washiriki.

Sasa niambie Tanzania na Marekani wapi wanatoka waimbaji bora?
Hatuwezi kulinganisha Marekani na Tanzania. Nchi yenye GDP kubwa (uwezo mkubwa wa kifedha) mambo mengi huwa mazuri- makocha , waalimu, music systems, studio za kurekodi na kadhalika. Pesa inawezesha mambo mengi sana. Ongeza budget ya Bongo star search utashangaa mambo yatakavyokuwa mazuri zaidi. Unapata kile ulichowekeza.
 
Hii bongo star search sijai ona mshindi hata mmoja aliyekuwa kwenye peak, nasikia pia wanazulumiwa sana
 
Judge Salama anainterfere sana na anadhani kuwa rude ni sifa mbona yule judge wa season iliyopita mwanamziki wa kikongo alikua mkali lakini hakua rude ?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom