Watu wa Kigoma naomba mnipokee mgeni wenu.

Karot

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
1,159
1,308
Habari za usiku wakuu..
Napenda kuwajulisha ndugu zanguni wa mkoa wa Kigoma kwamba nitakua mgeni wenu mda simrefu kwa ajili ya kuja kufata mzigo wangu.

Kikubwa nawaomba muje munipe ushirikiano wenu, safari yangu itaanzia Dar, matembezi yangu nitafikia mpaka vijijini kama:

Kagunga, Mwamgongo na maeneo ya mjini ambapo ndo itakua ndo penye kitovu cha shughuli yangu. Naamini sitakosa kuja kupata mafuta ya mawese ya kumwaga na sabuni kede kede ambazo zitakuja kuwa kama zawadi kwangu.
 
dondoo kuhusu Kigoma..


Mkoa wa Kigoma uko kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 47000.

Umepakana na Burundi na Mkoa wa Kagera upande wa Kaskazini, mikoa ya Shinyanga na Tabora upande wa mashariki na Mkoa wa Rukwa upande wa kusini. Magharibi umepakana na Ziwa Tanganyika penye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo .

Wilaya 8.

Makao makuu Kigoma Ujiji

Serikali -

Mkuu wa Mkoa Emmanuel Maganga.

Mkoa una eneo la km² 45,066 (sawa na 4.8% ya eneo lote la Tanzania) ikiwa km² 8,029 ndizo maji ya ndani (hasa Ziwa Tanganyika ) na km² 37,037 ndizo nchi kavu.

Takriban robo ya eneo la mkoa wa Kigoma hutumika kwa kilimo na ufugaji, karibu nusu ni misitu.

Kwa ujumla eneo la mkoa ni tambarare ya juu inayoanza kwenye mita 800 juu ya UB karibu na Ziwa Tanganyika na kupanda hadi mita 1,750. Mito ya kudumu ndani ya mkoa wa Kigoma ni Malagarasi, Luiche, Ruchugi na Rugufu.Mnamo Machi 2012 zimeongezwa wilaya mpya za Buhigwe, Kakonko na Uvinza.

Kabila kubwa ni
-Waha, likifuatwa na
-Wamanyema,
-Wabembe na
-Watongwe.

Kuna pia
-Wavinza,
-Wanyamwezi,
-Wasukuma,
-Wafipa

na watu wenye asili ya
-Kongo,
-Rwanda na
-Burundi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom