Watu wa Kigoma mbona hamuutendei haki mkoa wenu?

Bzimana

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
551
156
Wiki iliyopita nilimsindikiza rafiki yangu dereva kupeleka mzigo Kigoma.

Kusema ukweli barabara yenu ni mbovu sana wala hata haifai, kuanzia nyakanazi hadi maeneo fulani kasulu panatisha yaani barabara yenu ni ya vumbi tupu mashimo njiani, miji yenu huwezi kupiga kiwi kiatu wala kuvaa nguo nyeupe, kumbe ndio maana watu wa kigoma mmezagaa ovyo miji ya watu.

Mnavyakula vya kutosha, niliulizia pande la muwa futi kama 6 nikaambiwa 150, ndizi 6 tsh 200 nilishangaa, kigoma nini mliitendea serikali ya CCM Mimi naona Kigoma bado hamjapata uhuru na sijui wabunge wenu wanafanya nini bungeni.
 
watu wa Kigoma, Ruvuma na Rukwa wamepumbazwa na mafisadi ccm,.

Hawana ujanja,. Mtwara wameamka sasa
 
JK alisema itakuwa dubai ya Afrika, Tunasubiri

Kigoma ushirikina mkuu. kuna mzee anasia mchicha asubuhi jioni anavuna. pia kuna wazee maarufu wa mvua (wavulati) ndo miungu mvua. kibondo ndo hatari zaidi.
 
Hata dubai kuna ushirikina mkuu
 
Wewe Bizmungu (Bizmana) ni mtu wa kigoma acha kuyeyusha wana kigoma wenzako Tola ndadaye,crispin ntayamira,abelimana(abelimungu),piere buyoya na nkurunzinza ni ndugu zako.
 
kijana kumbuka hii ni ID haina uhalisia na jina langu kamili..
 
Tutafanyaje na CCM wameamua? Karibu Mjini Kigoma unywe maji ya nyakageni
 
Wiki iliyopita nilimsindikiza rafiki yangu dereva kupeleka mzigo Kigoma.

Kusema ukweli barabara yenu ni mbovu sana wala hata haifai, kuanzia nyakanazi hadi maeneo fulani kasulu panatisha yaani barabara yenu ni ya vumbi tupu mashimo njiani, miji yenu huwezi kupiga kiwi kiatu wala kuvaa nguo nyeupe, kumbe ndio maana watu wa kigoma mmezagaa ovyo miji ya watu.

Mnavyakula vya kutosha, niliulizia pande la muwa futi kama 6 nikaambiwa 150, ndizi 6 tsh 200 nilishangaa, kigoma nini mliitendea serikali ya CCM Mimi naona Kigoma bado hamjapata uhuru na sijui wabunge wenu wanafanya nini bungeni.

Wewe wacha kuropoka nchi hi sehem nying ndozimeanza kubadilika hiv karibun hebu mgepitia barabaraya tabora kgm halafu ukifika sehem moja inayo itwa NGURUKA utazame LAMI toka hapo mpaka kgm uilinganishe na lam yahuko kwenu wacha zako
 
Rangi ya udongo wakibondo nakasulu ndio ilivyo umbwa utafanyaje utaweka lami mpaka choon hiyo barabara nikweli niyavumbi mbovu sasa nani ajenge zaidi ya serikali yako au wachangishane
 
Wewe Bizmungu (Bizmana) ni mtu wa kigoma acha kuyeyusha wana kigoma wenzako Tola ndadaye,crispin ntayamira,abelimana(abelimungu),piere buyoya na nkurunzinza ni ndugu zako.

Msiwe mnavamia lugha za watu bila kufanya maandalizi. Sasa ABELIMANA ndo nini maana yake? Kwa taarifa yako, jina hilo kwa usahihi ni HABYARIMANA,(kwa kirundi na kinyarwanda) au HAVYARIMANA (kwa kiha na kihangaza). Next time, kuwa makini, shenz type!!
 
mbona pamechoka sana huko, hata wanakijiji wakikuona ni sura mpya wanakimbia nini tatizo kigoma
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom