Wabunge wa Kagera wapinga Mkoa wao kumegwa na kupelekwa Chato

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Wabunge wa Mkoa wa Kagera, Wamepinga kitendo cha kuendelea kuumega Mkoa wa Kagera. Hii imekuja baada ya Kuanzishwa Mchakato wa kufanya Wilaya ya Chato iliyopo Geita kuwa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule, alisema Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Geita (RCC) ilipendekeza wilaya tano, Chato na Bukombe mkoani Geita. Biharamulo na Ngara mkoani Kagera na sehemu ya Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma zichukuliwe kwa ajili ya kuanzisha Mkoa mpya wa Chato.

Kwa mujibu wa takwimu za sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Chato ilihesabiwa kuwa 365,127. Chato ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na maeneo ya Wilaya ya Biharamulo, Mkoa wa Kagera, mwaka 2012 ikasogezwa katika mkoa mpya wa Geita.

Pia soma:

1). Madiwani Buchosa wakubali kuhamia Geita ili kutoa fursa kuanzishwa mkoa mpya wa Chato

2). Kuunda Mkoa wa Chato ni kupoteza historia ya Wahaya, Mkoa wa Chato hauna maslahi kwa urithi wa utamaduni wa Mtanzania

3). Prof. Tibaijuka: Chato haina sifa kuwa Mkoa

4). Kwanini Chato iwe Mkoa kutoka kwenye Mkoa mchanga wa Geita ulioundwa 2012?

5). Geita yakubali kuundwa Mkoa wa Chato; Kakonko, Biharamulo na Ngara kumegwa. Sengerema kwenda Geita..

6). Geita: Baraza la Madiwani laukataa Mkoa mpya wa Chato

7)). Rais Samia Suluhu: Mkikidhi vigezo, Chato tutaifanya kuwa Mkoa

8). Rais Samia anaweza kuanzisha mkoa mpya wa Chato endapo haya yatazingatiwa…

HOJA YA WABUNGE KUPINGA KUMEGA MKOA WA KAGERA.

1. UTANGULIZI
Sisi wabunge wa Mkoa wa Kagera kupitia Wilaya ya Muleba na Wilaya ya Bukoba Vijiiini, Mhe Charles John Mwijage wa Jimbo la Muleba Kasikazini, Mhe. Dkt, Oscar Ishengoma Kikoyo wa Jimbo Ia Muleba Kusini, na Mhe. Dkt. Jasson Samson Rweikiza tumepokea wito wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Kagera cha tarehe 29/10/2021 tukiwa tayari tumerudi Dodoma kwa ajili ya vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge. barua za wito wa Kikao, zimeambatishwa na agenda za RCC. Agenda namba 4 ya kikao tajwa inahusu mapendekezo ya Wilaya za Biharamulo na Ngara kupelekwa mkoa pendekezwa wa Chato.

Hoja ya kuumeumega mkoa wa Kagera, inatualika kujadili faida na hasara zake kwa mkoa wa Kagera kwa kuzingatia masuala ya kijamii, kisiasa na kiuchumu. Tukiongozwa na uzalendo wetu kwa mkoa wa Kagera na utaifa wetu kwa taifa letu, kwa hali yoyote ile, pendekezo la kumega mkoa wa Kagera lina athari kubwa sana kuliko faida kwa usitawi wa Mkoa wa Kagera kihistoria, kijamii, kisiasa na kiuchumi. Kwa sababu hizo, na nyingine zitakazo tolewa hapa chini, hatukubaliani na hoja ya kuumega mkoa wa Kagera.

2. CHIMBUKO LA MKOA MPYA WA CHATO
Chimbuko la kuomba mkoa wa chato halina mashiko kisiasa, kiuchumi wala kisheria. Chimbuko la mkoa wa chato linatokana na muombolezaji mmoja aitwaye Bigambo wakati wa msiba wa Hayati Magufuli. Mwombolezaji huyo alidai kusikia Hayati Magufuli akitaka Chato uwe mkoa jambo ambalo halina uthibitisho wowote kisiasa. Vigezo vya kuunda mkoa mpya hutokana na mkoa mama kutokana na ukubwa wake na/au jiografia yake kuomba kumegwa i1i kusogeza huduma kwa watu wake.

Kwa ombi hili ni tofauti sana, Wilaya ndogo na changa ya Chato iliyoanzishwa mwaka 2005 inaornba kuwa mkoa ili maeneo mengine yamegwe kuisadia kutimiza adhima yake ya kuwa mkoa jambo ambalo ni kinyume na dhana na falsafa ya uundwaji wa mikoa katika historia ya taifa hili lililoasisiwa na viongozi wetu mahiri. Geita mkoa mama, nao ni mchanga ulioanzishwa mwezi Machi mwaka 2012 ukimegwa kutoka mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Kagera.

Pamoja na uchanga wake, Geita ni moja ya mikoa midogo ikiwa na kilomita za rnraba 20,054. Ukichukua ukubwa wa rniina wa Geita (20,054Km2) na Kagera (35,686Km2) kwa pamoja haifikii ukubwa wa Mkoa wa Tabora wenye ukubwa wa kilomita za mraba 76,150 au Morogoro wenye ukubwa wa kilomita za mraba 70,624. Ipo mikoa mikubwa na mikongwe iliyostahili kuleta ornbi kama hili, slyo wilaya ya Chato wala mkoa wa Geita. Kwa ukumbwa wa mkoa wa Kagera na/au Geita kuenendelea kuumega, mikoa ya Kagera na Geita itakuwa mkoa mdogo sana.

3. FAIDA
Kwa tathmini za kiuchumi, kijamii na kisiasa na kwa kuangalia jiografia ya mkoa wa Kagera kwa sasa na wilaya zinazolengwa kupelekwa hakuna faida yoyote kwa mkoa wa Kagera inayoweza kushawishi wananchi wa Mkoa wa Kagera kuridhia whlya za Biharamulo na Ngara kupelekwa mkoa pendekezwa.

4. ATHARI
Kwa kutumia vigezo vilivyotajwa hapo juu, athari kwa mkoa wa Kagera bila wilaya zake hizo mbili na kwa taifa zima la Tanzania ni kubwa sana.

4.1 KIJAMII:
(i) Mkoa wa Kagera ni muunganiko na mshikamano wilaya sabwa (7) za utawata zenye halmashauri nane. Pamoja na kuwa na wananchi wanaoweza kuhesabika kuwa makabila yanayojionyesha manne na koo nyingi sana, mapito ya mkoa huu katika historia ya kuwepo kwake yanaufanya mkoa huu kuwa jamii iliyoshikamana na imara kijamii, kisiasa na kiuchurni. Mkoa wa Kagera kwa kupakana na kuwa karibu na nchi nyingi umekuwa ukifikiwa na wageni wengi wa aina mbali mbali lakini wakati wote wana-Kagera walijiona wamoja na katika umoja huo wameweza kuhimiti matokeo yote hasi yaliyoletwa na wageni hao.

(ii) Kwa kuomba kuondoa wilaya za Ngara na Biharamulo kutasababisha mgawanyiko katika jamii na kufufua tofauti za kikabila na kikanda na koo zilizokwisha zikwa kwa siku nyingi za uhai wa mkoa huu. Pamoja na sababu nyingine, hii inatokana na ukweli kuwa wananchi wa Wilaya tano zinazobaki hawakukubaliana na hawatafurahia wilaya za Biharamulo na Nsciwa kumegwa.

(iii) Kwa taifa kuna athari kubwa za kijamii, kisiasa na kiusalama kwani mpangilio wa Wilaya tatu (3) zinazopendekezwa kuunda mkoa pendekezwa, zinawingi wa watu wenye nasaba na ushawishi wa mataifa ya jirani ambayo hayajatulia kiusalama. Mshikamano wa mkoa wa Kagera uliojengeka kwa muda mrefu uliweza kudhibiti na kumaliza nguvu athari hiyo.

4.2 KIJIOGRAFIA:
(i) Kuondoa wilaya za Biharamulo na Ngara kuna itenga Kagera inayobaki na kuinyima nafasi ya "location advantage" ya mipaka ya Kabanga na Rusumo. Ustawi wa Mkoa wa Ziwa Magharibi u;itokana na hiyo "location advantage". Katika zama hizi ambazo biashara kati ya mkoa wa Kagera na nchi jirani unaendetea kukua na kuimarika, kuzimega wilaya hizo kutaunyima mkoa wa Kagera fursa hizo za kibiashara.

(ii) Mgawanyo au kumegwa huku kunapunguza eneo la mkoa wa Kagera. Mkoa wa Kagera una ukubwa wa eneo la mraba 35,686 (KM2 35,686) ikijumuisha nchi kavu na eneo la maji ya ziwa victoria. Eneo la maji ni kilomita za mraba 10,173 na eneo la nchi kavu ni kilomita za mraba 25,513. Wilaya ya Biharamulo na Ngara ambazo ni maeneo ya nchi kavu ni kilomita za mraba 9,371. Hivyo, kumega wilaya hizo mbili, Mkoa wa Kagera utakuwa umebaki na kilomita za mraba 16,142 zinazofaa kwa kilimo utalii. ikumbukwe, Kagera si mkoa
unaotawaliwa na shughuli za huduma (Service industry) hali ambayo eneo dogo linaweza kuwa na watu wengi na shughuli nyingi za kiuchunii zinazohalalisha uwepo wa eneo la kiutawala kiasi cha mkoa. Huu ni mkoa wa wakulima, wafugaji na wavuvi hivyo kupunguza eneo Iake ni kuudhohofisha kijamii, kihistoria na kiuchumi.

(iii) Katika uhai wa mkoa huu na hasa rniaka 15 mpaka leo tumepigana sana kuwa karibu k\Ara kujenga miundombinu ya barabara. Kwa kazi inayoendelea kwenye ujenzi wa barabara mzunguko wa ndani kwa ndani kwenye mkoa itakuwa si tatizo. Kimsingi suluhisho si kumega wilaya bali kujenga na kuboresha miundombinu ya barabara, reli, afya, na uchumi.

4.3 KISIASA:
(i) Kagera bila Ngara na Biharamulo kisiasa siyo Kagera tunayoiona leo. Kufikia hatua hii ya kuwa na jamii tulivu na inayoelewana yenye mshikamano na mtazamo wa kimaendeleo haikuwa kazi rahisi, Wapo watu walihangaika kwa adhi na nyadhifa mbali mbali nao kwa kutambua mchango wao kwa Kagera si busara kuumega kila uchao.

(ii) Siasa ya Kagera ni zaidi ya mtazamo wa chama cha siasa na chama au vyama vingine. Tunazungumuza siasa kama hali au mtazamo wa jamii iliyoshuhudia na kuhimili kuanguka kwa uchumi baada ya kuvunjwa Chama cha Ushirika (BCU), Kuanguka kwa bei ya kahawa, jamii iliy()!itangulia taifa katika Vita dhidi ya Nduli ldd Amin Dada, jamii iliyopokea wimbi la wakimbizi toka nchi jirani, lakini pia jamii ambayo ilikuwa ya kwanza kupigwa na janga hatari la ukimwi.

Pia jamii hii iliyokumbwa na tetemeko kubwa la ardhi lililoaribu miundombinu na mali za watu, jamii ambayo wajasiliamali wake wengi na raia wengine walizama kwenye Mv Bukoba, ugonjwa wa Mnyauko wa r-nigomba kwa kutaja baadhi tu. Kimsingi, tafakari ya mapigo haya yaliyopata Kagera, Serikali inapaswa kuja na Mpango Maalum wa Kuikarabati Kagera (Special Economic Rehabilitation Program) ili ipone kwa ujumla wake na si kuumega vipande vipande kama inavyokusudiwa.

(iii) Athari nyingine kisiasa ni kufanya n-)aamuzi ya kumega mkoa kwa kufuata kilio cha mwombolezaji wa mkoa mwingine Bwana Bigambo alikuwa anaomboleza kama watanzania wote walivyoumia na kila mtu kusema lake kabla ya kutulizwa

1635996331925.jpeg
1635996357245.jpeg
1635996378371.jpeg
1635996393935.jpeg
1635996416216.jpeg
1635996434391.jpeg

1
 
Ila wahaya ni kiburi, nyie....

Nimesoma maneno machache sana hasa hapo kwenye CHIMBUKO LA MKOA MPYA WA CHATO na naomba kunukuu:-

"Chimbuko la kuomba mkoa mpya wa Chato halina mashiko kisiasa, kiuchumi wala kisheria"

Naendelea kunukuu....

"Chimbuko la mkoa wa Chato linatokana na muombolezaji mmoja aitwaye Bigambo wakati wa msiba wa hayati Magufuli."

"Muombolezaji huyo alidai kusikia kwamba Magufuli alitaka Chato uwe mkoa, jambo ambalo halina uthibitisho wowote wa kisiasa"

Mwisho wa kunukuu.

My take:
Yaani hawa jamaa (Wahaya) "wameikataa" kabisa Chato na wakafika mbali zaidi kwa kusema "zilikua ni hasira tu" za kufiwa (za msiba) za bwana Bigambo.
Lakini pia wametanabaisha kwamba alichokisikia bwana Bigambo hakina uthibitisho wowote, kwahiyo huenda Bigambo alikua "anatujaza tu".
 
Nimefika Chato. Ile wilaya JPM aliijaza miradi mikubwa sana ya kitaifa.
Uwanja wa ndege.
Miradi kibao ya NHC.
MABANKA MAKUBWA.
IKO MIRADI MINGI SANAAAAAA.

HII MIRADI ISIPOTENGENEZEWA MIKAKATI YA KUITUMIA ITAKUFA NA SERIKALI ITAPATA HASARA.
KUIGEUZA MKOA NI SOLUTION ILIYOPO.

SABABU ZA WAHAYA KUUKATAA MKOA WA RUBONDO ZIMEKAA KIHUNI TU.
 
Nimegundua kumbe wabunge wa kagera ndo wanazidi kupafanya kagera kuwa maskini...

Wanamawazo mgando na wako conservative.

Mimi naomba biharamulo na ngara ziundiwe mkoa wake ili ziangaliwe zaidi maana ndo maskini zaidi katika mkoa wa kagera.

Poor you wabunge
 
Nimefika Chato. Ile wilaya JPM aliijaza miradi mikubwa sana ya kitaifa.
Uwanja wa ndege.
Miradi kibao ya NHC...
Cha ajabu hao ni wabunge wa muleba, bukoba vijijini tu... Sio wabunge wote.

Mimi sijaona point ya msingi zaidi ya ubinafsi ya kuzikatalia biharamulo na ngara kutoka kagera ambazo zina umaskini wa kutisha.

Wabunge wa ngara na biharamulo wao wanasemaje
 
Wabunge wa mkoa wa Kigoma nao wajitokeze hadharani pia, kupinga kumegwa kwa wilaya ya Kakonko kwenda kuunda mkoa wa Chato.

Kama Chato inakidhi vigezo basi iombe kuwa Jiji la Chato ili mikoa mingine isiingizwe kwenye mgao huu usio na tija.
 
Wabunge wa mkoa wa Kigoma nao wajitokeze hadharani pia, kupinga kumegwa kwa wilaya ya Kakonko kwenda kuunda mkoa wa Chato.

Kama Chato inakidhi vigezo basi iombe kuwa Jiji la Chato ili mikoa mingine isiingizwe kwenye mgao huu usio na tija.
Hao hawawezi. Wengi hawana ushupavu wanasubiri mpaka Ofisi Na.2 aseme
 
Mka wa Ziwa Magharibi (uliopewa jina la Kager kwa heshima ya ushindi wa vita vya nduli) umekaa vizuri hapo ulipo. Kwa sababu za kiuchumi (access, critical mass, economic viability) ungebaki kama ulivyo.

Sababu za kikabila hazina mshiko, sababu aliyetoa pendekezo Bigambo na Mhaya. Isitoshe, Ngara si nchi ya Wahaya ni ya Wahangaza na Biharamulo ni pori mostly la wafugaji Wasukuma.

Pia naona Mbunge wa Ngara na wa Biharamulo hawajashiriki. Ukabila na mila etc etc etc hazina mshiko, sababu za kiuchumi ni muhimu zaidi. Kabila has never been a serious issue in Kagera or anywhere else in Tanzania: vimebaki vijembe vya Wahaya na Wanyambo; Baziba na Wakara; alizokuwa nazisema Nyerere kupinga ukabila.
 
Back
Top Bottom