Watu wa itifaki hapo Ikulu naombeni mpeni Rais wetu mapumziko sasa

Teko Modise

JF-Expert Member
May 20, 2017
1,911
6,001
Rais wetu tunampenda sana, na kwa muda mfupi amechapa kazi sana tena iliyotukuka. Ila kama ilivyoada kwa binadamu wote, ukifanya sana kazi kuna wakati unachoka na mwili unahitaji mapumziko ya kutosha.

Kuna video inasambaa kuke twitter imepostiwa kwa Maria Sarungi Ikimuonesha Rais Samia almanusura adondoke akiwa pale Lugalo tena katika vazi la kombati, inaonekana wazi kabisa mama amechoka kutokana na majukumu kuongozana.

Hivyo kama itawapendeza nawaomba mumpe likizo walau ya wiki mbili avute nguvu ili aendelee kututumikia sisi Watanzania kwa nguvu zote!
 
I agree
Binafsi namsifu sana Mama
Ana energy sana ya kuchapa kazi
But still after kazi kubwa u deserve a lil rest
walau wiki moja mama apotee machoni kwetu apumzike japo kidogo
 
Kwani akisema anahitaji kupumzika Kuna mtu atamlazimisha?
Kwa kweli Mh Rais na PM wanafanya kazi sana inabidi wakati mwingine wapumzike. Mh Rais ana mori ya kuwatumikia Watanzania hivyo haoni kwamba kupumzika ni muhimu anaona ni kupoteza muda. Hapo ndipo wanatakiwa hawa wasaidizi wake waingilie kati na kumlazimisha apumzike.
 
Ni kweli likizo muhimu. hata "mwendazake" alikuwa akishapiga mzigo kwa muda alikuwa anaenda likizo Chato, hivyo Mama yetu naye ajipe wasaa wa kupumzika,
 
Mama siku moja amehutubia Mara 3 kwa mavazi tofauti na hotuba tofauti na kukutana na sura tofauti.
Kiafya sio good kabisa.
Awe anaandaliwa matukio maalumu.Mengine awaachie mawaziri wake.
Mfano hai;
Jana kafanya tukio la jeshi.
Leo tukio la jeshi.
Pia waliomwandalia hotuba wawe makini
Mfano
Rais amesema Tumepeleka wanajeshi mtwara.
Siyo jeshi limpe taarifa yeye
 
yah kiukweli anahitaji mapumziko maana toka zile purukushani za msiba kuapishwa mpaka leo mama bado anapambana...

Mama tumekuruhusu chukua lidilimu laina hapo chap mpaka NYC kimyakimya kapumzike na bata kidogo uje ukiwa full charge tena....achana na hizi bata za kidimbwi zakina Paulo na jamaa zake wale wa lile geti...
 
Kweli kabisa apumzike. Yaani kiukweli mpaka sasa ameonesha uwezo na Afya kubwa Sana. Hivyo tuilinde hiyo Afya yake. Apumzike Rais wetu kipenzi.
 
Mama siku moja amehutubia Mara 3 kwa mavazi tofauti na hotuba tofauti na kukutana na sura tofauti.
Kiafya sio good kabisa.
Awe anaandaliwa matukio maalumu.Mengine awaachie mawaziri wake.
Mfano hai;
Jana kafanya tukio la jeshi.
Leo tukio la jeshi.
Pia waliomwandalia hotuba wawe makini
Mfano
Rais amesema Tumepeleka wanajeshi mtwara.
Siyo jeshi limpe taarifa yeye
Kwan ni uongo jeshi halijapelekwa mtwara mkuu?
 
Halafu alipokuwa pale,kulikuwa na taarifa rais anapokea kifimbo cha Malkia Cha Commonwealth.
 
Back
Top Bottom