Watu wa Dar es Salaam noma. Mama ana mtoto hamtaki kumpisha kiti!

renamaizo

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
2,118
3,004
Habarini wana JamiiForums

Leo ndio nimejua mjini shule. Asubuh majira ya saa 5 hivi nilikuwa nimepanda basi la G/MBOTO-KIVUKONI nikitokea G/MBOTO. Nilibahatika kupata siti kipindi safari inaendelea, ghafla akapanda mama mmoja hivi kabeba mtoto.

Mara ya kwanza nilitake easy nikijua kuna mtu atampisha, eeh maajabu watu wamekausha utasema hawajamuona vile. Na katika viti idadi kubwa ilikuwa ni akina mama na wadada baadhi, wanaume walikuwa wachache lakini wapi, wale wanawake wakaupiga kimya basi linaenda kasi huku linatikisika mama mkono mmoja kamshika mtoto mkono wa pili kashika bomba. Watu wamekausha, uzalendo ukanishinda ikabidi niinuke nimpishe, ikabidi nisimame safari nzima.

Sasa basi halijafika mbali kaingia mmama tena kabeba mtoto, watu wamekausha. Huyu hakupata kiti ata cha huruma mpaka tulipofika M/MMOJA kuna mtu akashuka ndio akapata nafasi.

Sasa kimbembe kikaja tena jioni kipindi narudi, kuna mmama kapanda basi na mtoto watu wamekausha mpaka nikaanza kusikitika sasa kipindi navuta gia kusimama nimpishe ndio ghafla yeye akamuomba mdada mmoja amshikie mtoto. Kwa bahati nzuri yule dada akaamua kumpisha kabisa.

WATU WA DAR MNAKWAMA WAPI?
 
Kati ya tabia zinazokera ni kumpisha "mtu mzima" kiti ndani ya usafiri wa umma then unakuta anashuka kituo cha jirani tu; wakati huo anashuka wewe umesimama jirani yake wala asante hakuna wakati kiustaarabu alitakiwa sio tu kusema asante bali kukurudishia siti yako ila ndio hivyo saa hizo wala hana habari na wewe uliyempisha kama aliiokota vile! So, unapoona watu wanakausha kuna mambo mengi; shukrani ya punda ...
 
Hayo mambo nimeshangaa zenji aio kumpisha mama mja mzito au mzee kama kuna msichana au mwanamke yeyote amesimama wanaume vijana wanawajibika kuwapisha akina mama ,wasichana,wajawazito na wazee.

Na kama gari imejaa mtu anaweza kujitolea kushuka kama wanapanda pamoja ili mama apate nafasi
 
Utaratibu wa kupisha siti angalau Dar upo ila mikoa mingine kadhaa niijuayo Hiyo habari ya kupisha siti haipo kabisa.
By the way Kama abiria walikuwa wagonjwa watapishaje?
 
Back
Top Bottom