Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Watu sita wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kumuua askari polisi Abdala Chande kwa kumkata na mapanga baada ya kupita katika nyumba inayofanyika biashara ya pombe haramu ya gongo eneo la msaranga manispaa ya moshi.
Kamanada wa polisi mkoa wa Kilimanjaro ACSP Wilbrod Mutafungwa amethibitisha kukamatwa kwa watu hao na kusema kuwa ivigenge vingi vya pombe haramu ya gongo vinahifadhi wahalifu.
Amesema askari huyo alishambuliwa na mapanga baada ya watuhumiwa hao kumwona akipita karibu na nyumba hiyo akiwa kwenye shughuli zake ndipo walipo piga kelele za kumuita mwizi na kuanza kumshambulia na mapanga.
Katika tukio lingine Jeshi hilo linawashikilia watu 13 kwa tuhuma za mauji ya ya kumnyonga mwanamke Anita kimario na kisha kuufukia mwili wake katika mashamba ya miwa ya kiwanda cha sukari cha TPC Moshi.
Hata hivyo kamanda Mutafungwa amewataka wananchi mkoani Kilimanjaro kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkono na kwamba kwa sasa wameelekeza nguvu kwenye nyumba zinazojihusisha na utengenezaji wa pombe haramu ya gongo ambazo zinasadikiwa kuhifadhi wahalifu.
Chanzo: ITV