Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 139
Kumbuka miaka ile bingwa huyu wa utabiri alifanya kazi zake sana nchini Kenya na nchi nyengine kadhaa za kusini mwa Afrika. Akiwa maeneo yote hayo alihakikisha kuwa Polisi wa siri wa Nyerere(mashushushu) walipata taarifa zote wanazozitaka na huyu Mwijage (Jamaa wa Kihaya kule Bukoba sijuwi yupo wapi siku hizi aliishi uhamishoni siku nyingi) alikumbana naye nchini Swaziland alipokuwa anamkimbia Nyerere na wauwaji wake, Bingwa wa utabiri huyu akajifanya kumsaidia na yaliyofuata hapo, ni kuishi kizuizini mwaka mmoja na ushee bila ya kufunguliwa mashitaka na mateso juu ya mateso.Hii Maneno?? alisalitiwaje? ebu tupe Habari yake imekaaje?