Watu Mnashangaa Uteuzi Wa Dr Migiro,Mimi Sijashangaa Ng'o

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Watu wengi wameshangaa Dr Migiro kutoka naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa mpaka kukubali kuwa balozi,Binafsi sijashangazwa na uteuzi huu,Wala sijashangaa Mama kukubali uteuzi,
Hii ni mbinu ya Ccm kuziba penyo zote za Upinzani kutokea,Mtakumbuka Sitta alitoka kuwa spika na kukubali kuwa Waziri,Tena wa Africa mashariki.
Watu wote ndani ya Ccm waliopata heshima kwa jamii huwa Ccm haikubali wapate muda wa kufikiri"Mfano"Ni mama migiro,Wameona wakimwacha mpaka 2020 anaweza kufikiri na kujiunga na upizani,Hata kwa sitta ilikuwa hivyo hivyo.
Hapa wanaofaidi ni Ccm,Lakini kwa wale wateule humalizwa kisiasa na heshima zao kushuka kwa jamii.Ni vema wengine mjifunze na kutafakari kabla ya kukubali teuzi za staili hii.
Ndio Maana aliyekuwa katibu mkuu wa OAU Salim Ahamed Salim heshima yake imeendelea kuwepo,Inaonyesha jinsi alivyo na msimamo.Siamini kama hakuwahi kupewa ofa ya uteuzi,Itakuwa anapewa ila ni mtu wa kupima faida na hasara.Jifunzeni kutoka kwa huyu mzalendo.
 
Back
Top Bottom