watu michosho

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,877
2,758
huwa nawasikiliza sana, hasa wasanii wetu na baadhi ya watangazaji. utawasikia wanasema, "hii nyimbo yako..." wanachanganya wingi na umoja hadi wanakera. waseme, "huu wimbo wako..." kitu "chengine" ni hilo neno. waseme kitu kingine. pia kuna neno, 'hichi' badala ya 'hiki'. watu wanakera sana. kuna mengine ili muwafundishe lugha hawa watu??
 
Uko sawa kwenye nyimbo.

Lakini "chengine" na "hichi" ni Kiswahili safi, sana sana lahaja ya Unguja ambayo ndiyo nzee kuliko zote za Kiswahili na wachunguzi wa Kiswahili wanaitambua kama ndiyo "bona fide" swahili.

Kiswahili ni kipana kuliko lahaja yako unayozungumza, ukienda Ngazija huko utakataa kwamba wanachozungumza ni Kiswahili, vile vile Katanga.

Kwa hiyo "hichi" na "chengine" ni Kiswahili sawa.
 
Kiranga,

Heshima yako mkuu!

'Nzee'?- 'hichi' nacho ni kingazija au kiunguja?

"Hichi'", "chengine" inawezekana kweli ni suala la lahaja tu. Lakini katika lugha rasmi ni lazima kuzingatia upatanisho wa kisarufi. Tazama ninavyotumia maneno hayo mawili katika sentensi zinazofuata:

1. Hichi ni kitu chengine ambacho ningependa kukufahamisha...
2. Hiki ni kitu kingine ambacho ningependa kukufahamisha....

Ni wazi sentensi ya kwanza inakosa upatanisho wa kisarufi (hata ulimi unatamani kutamka neno 'chitu' badala ya 'kitu'!).

Sentensi ya pili imezingatia upatanisho wa kisarufi.

Unaweza kutuandikia sentensi moja au mbili kuonesha namna ambavyo maneno 'hichi' na 'chengine' yanavyoweza kutumika na wakati huohuo kuzingatia upatanisho wa kisarufi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom