Watu maarufu sasa mujifunze.

mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
626
Kuna mtindo au tabia za baadhi ya watu maarufu kuamini na kuzani kuwa
ukitaka kuwa DIWANI au MBUNGE nilazima ugombee nafasi hiyo kupitia chama
tawala CCM, na si vyama vingine vya upinzani. Hakika hizo ni fikra giza na potofu.

Katika kipindi cha mchakato wa kura za maoni za kupata wawakilishi au wagombea
ndani ya vyama kabla ya uchaguzi mkuu 2010,tulisikia na kuona baadhi ya majina ya
watu maarufu kama shyrose banji,Erick shigongo nk,waliomba kugombea ubunge kupitia
ccm,na wengi wao kama si wote waliangukia pua.

Hivi tuchukulie mfano mdogo tu wa jimbo la kinondoni.Hivi pale mtu kama Shyrose banji au
Erick shigongo angegombea nafasi ya ubunge kupitia chama chochote cha upinzani'hasa
CHADEMA' Je asingeshinda? ukweli ni kwamba angeshinda tena kwa kishindo! sema hayo mawazo
yenu mgando na kutokuangalia alama za nyakati ndiko kumewaponza.

Mh.sugu wa mbeye amewaonyesheni na kuwaleteeni meseji mzuri sana kwenu kuwa INAWEZEKANA.
Ukweli ni kwamba watanzania wa leo si wale wa jana! siyo siri sasahivi watanzania wengi wamebadi
lika ki fikra na wanataka mabadiliko'hasa vijana wa kizazi hiki cha nyoka'.

Kwanza siku hizi watu wakisikia mtu maarufu au kijana wa kike au wa kiume anagombea nafasi ya
UDIWANI au UBUNGE kupitia CCM,basi watu walio wengi wanakushangaa sana! yaani unawaachia
mawazo ya pasua kichwa na hawapati jibu. Na hata ukifanikiwa kushinda kupitia hiyo ccm yako,Bado
jamii ya kizazi kipya watakutizama tofauti sana! utakosa mvuto ndani ya jamii na mwisho utaitwa fisadi hata kama si fisadi.

Hayo mawazo mgando ya kufikiria eti nikigombea CHADEMA au chama chochote cha upinzani nitaonekana msaliti kwa serikali ya ccm yameshapitwa na wakati! Au nikichangia pesa chama chocho
te cha upinzani eti serikali ya ccm itanifilisi si za kweli. na kama ilikuwa hivyo basi ni zamani sana na
si kwenye kizazi hiki cha nyoka. Acheni hizo na mubadilike ki fikra na kimtazamo!. Ahsante

Nawasilisha wandugu.
 
Hasa shy rose ananiuma sana ni mwanaharakati na kijana mzuri lakini ndo hivo tena mpaka anazeeka,
 
Hayo mawazo mgando ya kufikiria eti nikigombea CHADEMA au chama chochote cha upinzani nitaonekana msaliti kwa serikali ya ccm yameshapitwa na wakat
Nikweli kabisa kwa kuwa wanamadhambi yao wengine ni watumishi wanahofia serikali itakomaa nao.
 
Hao uliowataja ni balaa!Mmoja kwa 'mashoga' mwingine kwa 'shugadadi' na ndio umaarufu wao.
 
NATA,namjua haswaa,shy wa sasa sio wa 5yrs ago na hatakuwa wa 2015 kwisha habari yake
 
SHYROSE ameamua kuwa mpole anaogopa kuchukuliwa hatua na vyombo vya juu vya chama.
Wamemnyima hata viti maalum ilihali uwezo wa kuongoza anao. lakini yeye bado anaendelea kulalia kitanda cha misumari
 
Hivi Shy Rose kumbe ni kijana?
Mi nilifikiri ni mtu mzima flani hivi..
Wakuu wenye kujua umri wake hebu nisaidieni...
Manake wazee wetu siku hizi hawataki kuzeeka...
Rais wa nchi ana miaka 60+ lakini anajiita kijana bado..

:disapointed::disapointed::disapointed::disapointed:
 
wakati yupo na yule Dj wa mwanza hotel(D....go.da),anielza alikuwa na miaka 29,hiyo ilikuwa 91 sasa piga hesabu utajua atakuwa na miaka mingapi?,kusema ukweli ni kibibi fulani!!!!!!!!!!!!!!
 
kwa kifupi bi mdada 'aibu ya Rose' Shyrose ana miaka 48... Vp kuhusu kaka yetu 'nipo bize' Jafarai
 
Back
Top Bottom