Watu Kuzimia Baada Ya Matokeo Kutangazwa 28, Oktoba

youngsharo

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
2,491
500
Uchaguzi mwaka huu unapressure kubwa sana, uchaguzi wa mwaka huu unanguvu ya ajabu ambazo nathubutu kusema haijawahi kutokea tangu tanzania ianze kujitawala yenyewe

Tumekuwa tukishuhudia watu wanaozimia pale uwanja wa taifa mechi za watani wajadi Simba Vs Yanga, pengine inaweza kuwa timu iliyoshinda ndio watu huzimia kutokana na kulewa furaha, au timu iliyofungwa ndio watu wakazimia kutokana na kwamba waliingia na matokeo yao binafsi wakiamini wanashinda, hali hiyo ina nafasi kubwa ya kuwakumba wengi siku ya kutangazwa kwa mshindi wa Urais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania, na hili halina kizuizi.

Cha msingi ni kuwa; watanzania tujiandae kisaikolojia, tuwe tayari kuyapokea matokeo katika hali ya kawaida iwe ni mabaya kwa upande wako ama mazuri, usijiamini sana kwamba unashinda kwani ukishindwa ndo yanakupata haya, au usijishushe sana kuwa huwezi kushinda[usife moyo] kwani ukishinda yanaweza kukupata haya.

Nawasilisha youngsharo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom