Watu kama Ole Sabaya inabidi Kesi zao Mahakama iwe "LIVE"

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,791
3,360
Ni wazi kuwa vitendo vya viongozi hawa dhidi ya raia vilikuwa ni vya kidhalimu sana. Nchi ilitikisika na kupata doa la Kimataifa hata baadhi ya misaada ikasitishwa!

Ili Serikali ionekane haikuwatuma,kuwepo na mahakama huru na ya wazi. Kama ambavyo serikali ya Marekani ilijivua kidunia kuwa haijatuma Askari wake kuua mtu mweusi.

Wananchi wanajiuliza iweje uteue mtu, umsimamie wewe, pia useme ni mchapakazi Bora, ghafla ubadilike tena kwa kushinikizwa kuwa huyo ni jambazi? Vyombo vyote vya dola vilikuwa wapi?

Hakika hii kesi ya huyu jamaa itauweka uongozi wa juu kwenye mtihani mkubwa. Wananchi wanataka uwazi.
 
NDIPO UTAJUA KATIBA YA CCM HUWA JUU YA KATIBA YA NCHI KWA AMRI YA MATAKWA YA BASHIRU.

DAI KATIBA MPYA!
ONDOA KINGA ZOTE!
FUTA VITI MAALUMU!
SPIKA AWE LAYER asitokane na chama
 
Hivi kila mkuu wa wilaya ana walinzi wote hao?
 
Na vyombo vya habari hata vikiambiwa kurusha mubashara shurti ulipie vitaigombania hiyo haki ya kuonesha hii kesi kama mpira wa kona. Kinaweza kuwa chanzo cha mapato hiki!
 
Msikimbilie kesi. Acheni kwanza mahabusu ichukue nafasi yake kwa muda wa kutosha. Si hakuna dhamana?
 
Back
Top Bottom