Watu kama kina Mtambuzi huzaliwa na kulelewaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watu kama kina Mtambuzi huzaliwa na kulelewaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Nov 7, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Miongoni mwetu kuna wenzetu ambao kutokana na malezi, wanapokuja kupata umaarufu na fedha, wanakuwa kama nusu vichaa au vichaa kamili. Wanapopata umaarufu kidogo au wanapofuma fedha kutokana na juhudi zao au hata kwa wizi na rushwa, wanafumua kile ambacho kilikuwa kimefichwa kwenye malezi yao.

  Kuna idadi ya kutosha ya wenzetu ambao kutokana na fedha walizonazo, badala ya kuwa mfano wa binadamu bora na binadamu wa msaada, wanageuka kuwa wadhalilishaji na wapenda sifa, ambao huhangaika huku na huko kutafuta kununua umaarufu rahisi. Huingia kwenye baa hii na ile na kuonyesha kwamba wao ni kina nani, huwanyang'anya wanyonge wake zao, huwafungulia adui zao wasio na kitu kesi za kughushi na hutafuta kila njia ili watajwe na vyombo vya habari bila sababu.

  Ni kitu gani huwakabili watu wa aina hii ambao baadhi yetu ni marafiki au jamaa zetu? Hawa ni watu ambao walipata mkengeuko mkubwa wakati wa malezi yao. Ni watu ambao, kwanza wametoka kwenye familia duni au za mzazi mmoja (hasa mwanamke). Lakini ni watu ambao walipokuwa wadogo walionyeshwa kwa kila njia kwamba hakuna wanachokijua na hawawezi chochote.

  Unaweza kukuta ni watu ambao walipokuwa wadogo walikuwa wakishukwa na kamasi muda wote na pengine hata kusoma walishindwa. Ni watu ambao utoto wao ulijaa shida, masimango na kejeli nyingi za udhaifu na mashaka ya kutomudu chochote.

  Kama tujuavyo malezi yetu na mazingira tuliyokulia hutuathiri sana tuwapo wakubwa. Mawazo yetu ya kina hunakili kila jambo ambalo sisi tumeliona ni muhimu, ambapo jambo hilo huja kutumiwa ukubwani hata kama sisi hatujui. Kwa kuambiwa kwamba, sisi ni watoto wajinga, watoto tusiojua kitu na ambao hatutakuja kuweza kitu maishani, tunakuwa tumejengewa hasira dhidi yetu wenyewe. Tunapokuja kuwa wakubwa na kama tukipata mafanikio tunaweza kuwa kwenye hali au tabia za aina mbili. Tunaweza kuwa ni watu tusiojiamini au kuamini kwamba uwezo tulionao hautadumu.

  Muda mwingi tunaweza kuutumia kwa kuhofia kupoteza na kurudi mahali pagumu ambapo patadhihirisha kwamba ni kweli hatujui kitu, kama tulivyofanywa kuamini tukiwa watoto. Tunakuwa ni watu wa mashaka wakati wote na hata mahusiano yetu na wapenzi wetu au wake zetu yanakuwa yamezingirwa na mashaka makubwa.

  Ni vigumu kumwambia mtu mwenye mkengeuko huo kwamba, ana athari za kimalezi na akakubali kwa sababu, kwake yeye haoni tatizo lake. Anachokiona yeye ni kutenda yale ambayo anaamini ni haki kuyatenda kwa sababu dunia haimfahamu alivyo. Kwake dunia anayojaribu kuionyesha alivyo ni ile ya utotoni, ingawa mwenyewe hajui.

  Ni kwa sababu kama hizi ambapo wazazi tunaambiwa kwamba, badala ya kuwavunja moyo watoto wetu wanapoonyesha udhaifu fulani, tuwape moyo sana. Tunapowaonya na kuwaambia kwamba, ni mabwege, wajinga na kuwaita majina yote mabaya tunayoyafahamu, tunakuwa tunawatengenezea mazingira ya kuja kujihami wakipata fedha ukubwani au umaarufu fulani. Kujihami huku siku zote ni kwa hasara zao.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Siku zote naamini, ukiwa mpumabvu halafu ukawa na pesa, pesa hizo huukuza upumbavu wako. Na ukiwa na hekima halafu ukawa na pesa, basi pesa itang'arisha hekima yako.

  Ila umeeongelea watoto wanaolelewa na single mothers, wanakuwa kama hao uliowaelezea hapo juu, mimi hapo natofautiana na wewe. Si kila single mother mtoto wake ataharibikiwa kifra, wapo ambao wameweza kulea watoto wao na kuwa watu responsible. Kuharibikiwa kwa mtoto aliyelelewa na mama peke yake itategemea tabia na misingi ya mama mwenyewe kama ilivyo kwa familia zenye baba na mama. kama baba na mama hawana misingi mizuri watoto huharibikiwa wakiwa hapo hapo wote wawili. Its 50/50 kulingana na malezi ya mzazi.

  Unapozaliwa naamini unakuwa kama plain paper, utaanza kurithi tabia kulingana na kitakachoandikwa kwenye paper yako na jamii inayokuzunguka. Kwa mtoto under 5yrs anatakiwa sana kulelewa na wazazi hasa mama. Mzazi anatoa inconditional love, kwa hiyo anamfundisha mtoto to love others unconditional, trust and the like. Kwa hiyo wazazi tunaotelekeza watoto tunawasababisha kuwa waoga mental, hii husababisha kuwa defensive kupita kiasi na kisasi kwao ni cha kugusa tu. Hapa ukisoma historia ya Adolf Hitler unamkuta anaangukia hapa maana inasemekana baba yake alikuwa Jewish halafu akamkataa na kumtelekeza

  Umaskini wa kupindukia unasababisha unamfanya mtoto kukua akiwa na low self esteem, sasa atataka ku-prove yeye anatahamani kwa jamii. Atatafuta pesa. power na umaarufu kwa njia yeyote, pablo Escobar can fall on this category, hata Iddi Amin.
   
 3. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  KUNA WENGINE walizaliwa mapapai wakaja kuwa binadamu ukubwani!
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  mimi ninashindwa kuwaelewa wana-JF ambao habari ndefu na yenye virutubisho kama hii waweza kuichangia kabla hata ya kumshukuru aliyetumia muda wake mwingi kuiandika...............................utamaduni wa kutoa shukrani ni miliki yetu sasa huu ughaibuni sijui ulianzia wapi..................let us not take for granted others' productive works of art.....................
   
 5. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,669
  Trophy Points: 280
  Hii ni nzuri sana kwa wazazi na kila mmoja wetu!Inazungumza uhalisi na chimbuko la matatizo yetu!
   
 6. M

  Munira Member

  #6
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Naomba nimuunge mkonoRuta,thanks mtambuzi.
   
 7. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Kuna watu walistahili watengewe jukwaa la peke yao ili mawazo na hoja zao zisiwe zinachafuliwa kienyeji. AshaDiiiiii, Mtambuziiiiii na MwanaJamiioneeee, hongera zenu! Mniruhusu michango yenu niitolee kitabu, hahhahahahaaaaaaaaaaa!
   
 8. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu Thanks for the good posting,

  Kujua madhara ya hisia hasi kwa mtoto, kutamfanya Mzazi amlee mwanae kumlinda asifikie kwenye hisia hasi cha shaka, woga, misononeko nk. Hii ikiwa na maana kuwa Mzazi atamlea mwanae kwa ufahamu wa UPENDO wenye ujasiri na maonyo yasiyovunja Moyo na uasili wa mtoto.

  Lakini kama mzazi atakosa hekima na busara, iliyosehemu ya Upendo wa mtu mzima hataweza, kuelekeza na kutoa maonyo ya kimalezi kwa mwanae, bila shaka huyo mtoto atajikuta muda mwingi anatawaliwa na HISIA HASI. Na kila hisia hasi inabomoa UJasiri na Upendo wa kujiamini na kutokea Mtu timamu baadae kama mtu mzima. Ni Upendo toka kwa Wazazi na walezi unaonjeegea Mtoto UFAHAMU WA KIUTAMBUZI ... ulio upendo Kama dira na msingi wa maisha ya kujiamini,kujiheshimu na kujisimamia mwenyewe.!

  Lazima tujifunze kutoa Masahihisho, maelekezo na mafundisho kwa watoto wetu tukiwa hatuna hisa hasi za chuki,hasira, mashaka, woga, kinyongo na ukali usio na msingi. Uzazi sahihi ni ufahamu, ujasiri katika maonyo kwa upendo uiso na hisia hasi hata tone moja!

  Mtoto aliyekosa upendo huo, atautafuta kwenye Vitu na mazingira yake ...Kama mbadala wa UPENDO WA KUZAZI. Hilo litamfanya kuwa limbukeni wa Hela na vyote vipatikanavyo kwa hela Kama dawa ya kutibu kile alichokikosa kwa wazazi na wengine wanaweza wasirekebike hadi uzeeni. Ndio maana inabidi kulea Ufahamu na Utambuzi wa mtoto kwa malezi ya Upendo ili kumpta Mtu timamu ukubwani. Malezi sio Kuusimamia mwili na mahitaji ya mwili peke yake!!

  AJ
   
 9. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #9
  Nov 8, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Lol...wengine walizaliwa hawana vichwa wakawekewa nazi....
   
 10. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #10
  Nov 8, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mkuu hapo kwenye list ongeza mbu, nyamayao, RussianRoulete! Hawa pia nawakubali sana kwa michango yao humu jf!
   
 11. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #11
  Nov 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,069
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi asante kwa maelekezo yako,
  siku moja nitakuambia kwa ufasaha zaidi kuhusu hili.
   
 12. K

  KISABENGO Member

  #12
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Cjamuelewa kwa hiyo anatutukana cye tuliolelewa na mama!! Ckia busara hazijarishi umetoka ktk malezi gani! Na hekima alkadhalika haitambui umetoka malezi'bnadamu utakaoishi nao ndio wataijenga na kuibomoa hekima na busara'ckia mi na kaka na dada zangu tumelelewa na mama tumetoka ktk nyumba nambali moja kwa kuuza madawa ya kulevya,umalaya,gongo,ushoga na uchafu wote'unafikiri ukiwa na rafiki aliyelelewa kwenye nyumba kama mkapoteana baada ya miaka mingi unahisi utamkuta kwenye hali gani"ACHENI KUSOMA MAKALA ZA WAZUNGU MKATUPIA HAPA'fanyeni chunguzi zenu za kweli nyambafu.
   
Loading...