Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,684
- 149,887
Hii ni sehemu ya maoni ya Dk.Bana kuhusu matokeo ya uchaguzi mdogo wa madiwani kama yalivyochapishwa na gazeti la Mtanzania la siku ya leo tarehe 25/01/2017.
Dk. Bana na udhaifu
Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Benson Bana, alisema ushindi waliopata CCM ni dhahiri kwamba upinzani umekwisha nguvu.
Alisema ushindi huo ni njia mojawapo ya mwaka 2020 kwa CCM kuwa na njia nyeupe ya kushinda uchaguzi bila upinzani kupata viti.
Dk. Bana alisema CCM bado ina nguvu, wananchi bado wa imani na ni ushahidi tosha Ukawa wameishiwa nguvu.
“Nilitegemea baada ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 Ukawa wangejipanga na kusajili chama kimoja, lakini wameshindwa kufanya hivyo basi wataendelea kugawana kura.
“Tatizo la Ukawa kwa sasa pia ni kushindwa kufanya kazi na matokeo yake wanamkumbatia mtu mmoja aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
“Lowassa kwa sasa ana mvuto yeye ndani ya Ukawa na sio Ukawa kuwa na mvuto na wananchi na mbaya zaidi hawawezi kufanikiwa kutokana na mparaganyiko uliopo kati ya Zanzibar na Tanzania Bara,’’ alisema Dk. Bana.
Chanzo:Mtanzania
Viongozi wa UKAWA kuweni waangalifu sana na wala msiwasikilize watu mkafanya maamuzi ya pupa.
Kushindwa kwa UKAWA kuna sababu nyingi tu na wala si Lowassa au Sumaye au wana-CCM wengine waliohamia upinzani.