Watu hawa ni adui wa uchumi wetu tusiwape nafasi

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Aug 28, 2020
2,204
2,083
Watu hawa ni adui wa uchumi wetu tusiwape nafasi

1. Mijitu inayojipenyeza kwenye ajira kwa kutumia vyeti feki ili ipate mshahara ambao ndio kodi zetu

2. Mijitu inayoiba twiga na tembo wetu kisha kwenda kuuza na kujipatia fedha.

3. Mijitu inayouza madawa ya kulevya na kujipatia fedha.

4. Mifisadi na fedha za serikali na fedha zetu za miradi

5. Mijitu inayotaka kufanya biashara bila kulipa kodi. mfano Kupitisha mizigo bandarini bila kulipa kodi kisa inafanya kazi serikalini. Kushikiria zile biashara kubwakubwa peke yao nchini tena bila kulipa kodi utadhani hili taifa ni la tuu peke yao.

6. Kwenye madini, mijitu inayotuibia madini yetu na kuuza, na kujipatia, mifedha kiulaini huku wananchi wanateseka na maisha magumu tena bila kuona miundombinu ikijengwa.

7. Mijitu inayoingiza wafanyakazi hewa kwenye malipo ya mishahara serikalini na kujiingizia hiyo mishahara wenyewe. Kodi zetu ndio zinatembea hivyo. Pesa yote tunaishia kulipa mishahara kumbe bwana kuna mijitu ina mkono mrefu.

8. Mijitu inayoiba madawa yetu hospitalini na kusababisha hospitali zetu kukosa, madawa ukienda kutibiwa unaandikiwa ukanunue madawa paleeeeee.

9. Daaaaaaaaaaaa nimechoka ngoja, niishie hapa uzi tayari labda wakuu mnisaidie.

Lakini hivi mnajua hayo mambo yapo wakuu. Japo nilikua najiandikia tu.
 
Hao uliowataja law Tz ndo watu pendwa mnoo. Uiiwagusa tu imekula kwako.
 
Ukitaka kuugua ugonjwa usio julikana kagea vyeti wabunge waccm,na waleeeeeeeeeeeeeeee jamaaa wanaotulinda , Wakuuu wa mikoa na wilaya!!!
 
Back
Top Bottom