Watu elfu 43, 000 ndio wamepiga kura kinondoni wengine 225, 000 waliojiandikisha wamekata tamaa na kupiga kura?

uchaguzi wa marudio uliopita, si mlisema kuwa hao ambao hawakupiga ni wengi hvyo chadema ingeshiriki ingeshinda! nlitegemea kwa kuwa chadema inapendwa sana na wananchi basi wengi wangejitokeza kuwasupport
yes ukweli ndio huo hao wengi ambao hawajajitokeza ni lazima wangepigia upinzani.tatizo linakuja pale mtu anapojiuliza hata nikipiga kwa upinzani bado serikali+CCM+polisi watatumia kila njia kupora ushindi,ndipo hapo mtu anaamua bora akae zake nyumbani
 
Jimbo la kinondoni waliojiandikisha ni 270 000 waliopiga kura ni 43 elfu tu hawa wapiga kura wako wapi je wamejikatia tamaa
Mwaka juzi alieshinda alipata kura elfu 70
Wa pili elfu 66 ina maana kura zote zilizopigwa hazijafikia hata za mshindi wa pili mwaka juzi
Tatizo ni nini
Je watu wamekata tamaa kupiga kura
Au watu hawana muda na swala la kupiga kura nchi hii
2015 pesa ilitembea sana kwa wapiga kura.BAA za ukawa watu walinyweshwa bure kwa siku nyingi mfululizo .Siku ya kuamkia kupiga kura watu walikuwa na mikesha ya kulewa wakisubiri kuche wakapige kura,kadi ya kupigia kura ilipewa jina la kichinjio.Kunywa bure baa ya mwana ukawa ilikuwa wewe sifia tu kuwa UKAWA na Lowasa watashinda.Boda boda walipewa pesa na kujaziwa mafuta.Makanisani na misikitini ndio usiseme maburungutu ya pesa yalimwagwa na CHADEMA KUPITIA lowasa kama njugu kuchangia harambee hewa na kuhamasisha watu kupiga kura.Makundi mbali mbali yakiwemo ya wapiga kampeni yalimwagiwa pesa nk Wapiga kura WENGI wa chadema hawajazoea kupiga kura bure bila pesa au kupewa kitu.Wamesusa sababu wanaona viongozi wamebadilika hawatoi pesa tena wakati hela wanazo za ruzuku.Kifupi chadema wengi wamesusa kujitoa kwa uzalendo wakati viongozi wao si wazalendo hawafanyi kwa uzalendo.Ndio maana Jimbo la Siha lilifurika sana siku ya mkutano wa kufunga kampeni uliofanywa na Lowasa wakitarajia kuwa baada ya kufungwa mkutano wangepewa hela na mafuta kuwafidia muda waliokaa mkutanoni bila kufanya biashara.Lowasa alipomaliza huyo akaondoka zake.Kuonyesha hasira zao vijana wa chadema na boda boda chadema hawakwenda kupiga kura
 
Si kuna kama nyinyi mnataka ID ya kupigia kura ili iwasaidie kwenye kusajili line lakini kwenye kupiga mko home tuu kuanzisha mijadala ya kukinukisha mkiwa JF, FB na IG

Hiyo inaonyesha hakuna jambo la kipuuzi kama kupiga kura nchi hii. Kwa maneno marahisi mtu anayeheshimika nchi hii ni mwenye line ya cm na sio anayekwenda kupiga kura!! Kweli ccm mmeifikisha nchi pabaya. Sasa ndio muda muafaka wa kuongeza ile miaka 7 maana wananchi wameshapuuza huo ushenzi unaoitwa kupiga kura.
 
Idadi ya waliojiandikisha ni ile ya 2015 period!!
wengine wamehama wengine ni wafu wengine wamesafiri.kwani 2015 walipiga asilimia ngapi ya waliojiandikisha?

Bado mpo kwenye denial stage
Nasikia huyu kada wa ccm alikua wakala wa usimamizi wa uchaguzi pale kino vipi sheria inaruhusu kada wa chama fulani kuwa wakala?
045eb24ce9c3bb37121dcfa3cd627ce3.jpg
39251a5f320da7c71611d0cd914ffcd5.jpg
843a4e03bdaa35b254a903d877337a77.jpg
 
Ndiyo maana hakuna shamra shamra za ushindi!
CCM ushindi tumeuzoea ni kitu cha kawaida kwetu.nyie ambao hamjazoea ndio kaushindi kadogo tu mfano ka diwani mtakesha usiku kucha kwa shamra shamra na kurusha fataki angani
 
Ikipigwa forensic auditing, lazima yatakutwa madudu ya kutisha kwenye takwimu za tume. Kazi ya tume ni kuhakikisha maCCM yanashinda. Hawawezi kuwa na takwimu sahihi.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom