Watu 9 waliohusika kutungua chopa na kumuua rubani wakamatwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Jeshi la Polisi Simiyu limewakamata watu 9 waliohusika kutungua helkopta ya kampuni ya Mwiba na kumuua rubani wa helkopta hiyo Rogers Gower.

Baada ya kuuawa kwa rubani Rogers Gower, familia yake imechangisha fedha ili kuendelea kupambana na ujangili nchini kuenzi kifo chake.
rubani.jpeg

rubani Rogers Gower wakati wa uhai wake

===================

Sakata la Kutungua Helkopta: Polisi Yakamata Watuhumiwa 9 Akiwemo Mhifadhi wa hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro Pamoja Na Bunduki 29
2jiachie Limitedabout an hour ago0 No comments

1.JPG

Siku chache baada ya kutokea tukio la majangili katika pori la akiba Maswa wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, kuitungua ndege (helikopta) iliyokuwa doria na kuaawa kwa rubani wake Rodgers Gower (37), watu 9 wamekamatwa kuhusika na tukio hilo.

Katika watuhumiwa hao mmoja niMhifadhi wa hifadhi ya taifa ya Ngorongoro kitengo cha Interejensia, ambaye alitajwa kuwa mhusika Mkuu wa kufanikisha tukio hilo sambamba na kukamatwa mganga wa jadi.

Akitoa taarifa mbele za waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa polisi Mkoani Simiyu Lazaro Mambosasa alisema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na jeshi hilo kufanya kazu usiku na mchana kwa kushirikiana na wananchi, pamoja na uongozi wa TANAPA.

Kamanda Mambosasa alisema watuhumiwa wote walikamatwa na kukiri kuhusika na tukio hilo, huku akieleza kuwa msako mkubwa uliofanywa na jeshi hilo mara baada ya tukio kutokea chini ya Mkuu wa upelelezi Mkoa Jonathan Shana.

Alisema katika msako huo baadhi ya watuhumiwa walibainika kuwa kiungo kikubwa kufanikisha tukio hilo kwa kutoa mbinu za uharifu, huku wakijihusisha na matukio ya ujangili kwa muda mrefu.

Aliongeza kuwa baadhi yao walibainika kuwa waganga wa jadi, ambapo walikuwa wakitoa dawa kwa majangili za kuosha silaha, ikiwa ni pamoja na kuosha na kusafisha miili yao ili wasiweze kukamatwa.

Mambosasa aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Shija Mjika (38), Njile Gonga (28) Mhazabe, Masasi Mandago (48) pamoja na Dotto Pangali (41) , ambao ndio walihusika kutungua helkopta hiyo.

Wengine niIddi Mashaka (49)ambaye Kamanda Mambosasa alimtaja kuwaMhifadhi wa hifadhi ya taifa ya Ngorongoro Kitengo cha Intelijensiana ndiye alikuwa kiungo Mkuu wa tukio hilo.

Aliwataja wengine kuwa ni Mapolu Njige (50) ambaye ni mganga wa jadi aiyekuwa anatumika kutoa dawa za kutokamatwa kwa majangili hao, Mwigulu Kanga (40) , Dotto Huya (45) , Pamoja na Mange Balumu.

Aidha Mambosasa alisema kuwa Mtuhumiwa Dotto Pangali alikamatiwa katika wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga mnamo tarehe 7/02/216 na kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake ambapo alikutwa na bunduki aina ya Riffle yenye namba .7209460 CAR Na.63229.

Mkuu huyo wa polisi alisema Mtuhumiwa huyo alikiri bunduki hiyo kutumika katika tukio la kuuawa kwa rubani huyo, ambapo ilibainika kuwa bunduki hiyo inamilikiwa na Mange Magima ambaye pia amekamatwa.

Alisema msako uliendelea nyumbani kwa Pangali na kufanikiwa kukamatwa kwa bunduki nyingine aina ya Riffle Na3478 CAR 458 ikiwa na risasi 6 ambayo ilibainika kumilikiwa na Nghomango Jilala ambaye mpaka sasa hajakamatwa.

Alieleza kuwa jeshi hilo liliendelea kupata taarifa ambapo mnamo tarehe 29/01/2016 walikamatwa Shija Mjika, Njile Gonga, pamoja na Masasi Mandago wakiwa na meno ya tembo 2 yakiwa na uzito wa Kilo 31 yakiwa yamefichwa chini ya daraja katika kijiji cha Itaba.

Aidha Mambosasa alieleza kuwa baada ya kukamatwa kwa wahusika wote ilibainika kuwa bunduki zilizotumika katika tukio hilo zinamilikiwa kihalali na watu ambao waliomba kuzimiliki kwa ajili kujilinda.

“Mbali na tukio hilo bunduki nyingi wamiliki wake wanawaazimisha majangili kwa ajili ya kutumika kwa uhalifu pamoja na kuua wanyama ndani ya hifadhi…lakini na hao wamiliki wanalipwa pesa baada ya uhalifu kufanyika”,alisema.

Alisema baada ya kubaini hilo kulifanyika msako mwingine kwa wanaomiliki silaha, ambapo alisema asilimia kubwa wanaishi karibu na hifadhi, na jumla ya bunduki 27 zimekamatwa na mara baada ya uchunguzi wamiliki watarudishiwa.

“Tunajiandaa kupeleka zuio la silaha mahakamani ili kubaini kama wana sifa za umiliki…lakini mbali na hilo sasa kutaanzishwa oparesheni kwa watu wote wanaomiliki silaha hasa maeneo ya hifadhi kwa ajili ya kuwanyanganya”,alisema.

Mkuu huyo wa polisi alisema kuwa upelelezi juu ya tukio hilo umekamilika na watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani leo Jumanne ili kujibu tuhuma zinazowakabili, ambapo alioomba mahakama kuharakisha hukumu kwa vile uchunguzi umekamilika.

Kwa upande wake Mhifadhi mkuu wa Serengeti William Mwakilema amelipongeza jeshi la polisi ambapo amesema tukio hilo lilipotokea liliwasikitisha sana kwani hasara ilipatikana kutokana na kutunguliwa kwa helkopta.

Mnamo tarehe 29/01/2016 saa 11:30 jioni katika eneo la Gululu lililopo ndani ya hifadhi ya Maswa kata ya Mwangudo wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, majangili waliipiga risasi ndege (helkopta) 88HFCG iliyokuwa doria na kusababisha kifo cha rubani wake Rodgers Gower (37) raia wa uingereza huku Mwenzake Nicholas Beste (43) raia wa Afrika Kusini akinususrika kifo.
2.JPG

6.JPG

7.JPG

 
Jeshi la Polisi Simiyu limewakamata watu 9 waliohusika kutungua helkopta ya kampuni ya Mwiba na kumuua rubani wa helkopta hiyo Rogers Gower.

Baada ya kuuawa kwa rubani Rogers Gower, familia yake imechangisha fedha ili kuendelea kupambana na ujangili nchini kuenzi kifo chake.
View attachment 321824
rubani Rogers Gower wakati wa uhai wake

Ni mategemeo yetu sheria itafuata mkondo wake na haki itatendeka.
 
Vita dhidi ya ujangili ni ngumu lakini ni muhimu sana. Haiwezekani utajiri tuliopewa na Mungu uwe ni faida kwa wachache tu. Aina hiyo ya utajiri ni laana kwa taifa zima. Nchi imechezewa sana na Rais Magufuli yupo sahihi kabisa kusema kwamba lazima irudi kwenye mstari ulionyooka. Upendo na uzalendo wa wananchi huanzia pale wanapomuona kiongozi mkuu wa nchi akiwa mzalendo na mwenye kuongozwa na nia za kubadilisha maisha ya walio wengi. Awamu ya tano inao mtihani mzito wa kuondoka ile dhana potofu kwamba wachache wameuimbiwa utajiri na walio wengi wameumbiwa umasikini.

Mapambano dhidi ya wote wanaowaua tembo wetu na wanyama wengine wengi tu, ni vita ambayo inahitaji watanzania kwa pamoja kuwa kitu kimoja, tufikiri kwa nia ya kutakia mema nchi, na sio tunakuwa wepesi kuwaunga mkono wale wanaotaka kutajirika kupitia ujinga wetu, kupitia ukosefu wa uzalendo wa baadhi ya wenzetu.
 
Jeshi la Polisi Simiyu limewakamata watu 9 waliohusika kutungua helkopta ya kampuni ya Mwiba na kumuua rubani wa helkopta hiyo Rogers Gower.

Baada ya kuuawa kwa rubani Rogers Gower, familia yake imechangisha fedha ili kuendelea kupambana na ujangili nchini kuenzi kifo chake.
View attachment 321824
rubani Rogers Gower wakati wa uhai wake
Masikini kawacha familia yake kwa kisa kufanya kazi tu tanzania?r.i.p
 
Nimesikia wametangaza watu 9 wakiwa na bunduki 32 na meno matatu ya Tembo wamekamatwa Simiyu.
Mtangazaji kauliza wana uhakika gani kwamba hao ndio waliohusika? Mhusika akajibu kwamba mtu mmoja alikamatwa akafanikisha wengine 8 kukamatwa. ..

Source : Capital radio.
 
Nakumbuka mwanzo kabisa wa tukio la rubani kuuwawa walisema wamekamata watu watatu. ..sasa sijui hao bado pia ni wahusika?
 
Unakumbuka wale waliokamatwa mapango ya amboni na wale wa morogoro?Teeeeeeeeeh teeeeeeeeh,
Akili za aina hii ni kielelezo cha watu ambao hawawezi kuja kuendelea, kila siku unahisi unadanganywa, unahisi unadhulumiwa, kila kukicha unahisi unatapeliwa. Matokeo yake huwezi kuwa na constructive mindset. Unaishia kuwa mdogo katika ujengaji wa hoja, unaishia kuwa mlalamikaji aliyejaa mifano mingi ya siku zilizopita ambayo unaitumia katika kujenga hoja dhaifu. January Makamba aliwauliza wapinzani "what would you have done differently?".
 
Akili za aina hii ni kielelezo cha watu ambao hawawezi kuja kuendelea, kila siku unahisi unadanganywa, unahisi unadhulumiwa, kila kukicha unahisi unatapeliwa. Matokeo yake huwezi kuwa na constructive mindset. Unaishia kuwa mdogo katika ujengaji wa hoja, unaishia kuwa mlalamikaji aliyejaa mifano mingi ya siku zilizopita ambayo unaitumia katika kujenga hoja dhaifu. January Makamba aliwauliza wapinzani "what would you have done differently?".
Naona wewe somo la historia hukulisoma ndio maana hutaki kujikumbusha au kulinganisha tulipo na tulikotoka
 
Back
Top Bottom